Augustoons
JF-Expert Member
- Oct 31, 2007
- 409
- 31
Richmond:Ikulu yatoa tamko hatima ya Dkt. Hosea, Mwanyika
Na Timu ya Majira Jumapili
SIKU chache baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kuwasilisha Bungeni taarifa ya Serikali juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kufuatia kashfa ya kampuni tata ya Richmond na kubainisha kuwa vigogo kadhaa Serikali waliohusishwa na kashfa hiyo hatIma yao iko ngazi za juu, Ikulu imetoa tamko rasmi.
Miongoni mwa vigogo ambao Bunge liliarifiwa kuwa majaliwa ya ajira zao yako mikononi mwa aidha Rais Jakaya Kikwete mwenyewe au Katibu Kiongozi Ikulu, Bw. Phillemon Luhanjo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu, Bw. Johnson Mwanyika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Arthur Mwakapugi.
Ikulu jana imetoa msimamo wake kwa mara ya kwanza juu ya kinachoendelea baada ya kuachiwa dhamana ya uamuzi juu ya vigogo hao.
Bw. Luhanjo hata hivyo alikwepa swali lililomtaka athibitishe iwapo ofisi yake imekwishapokea maelezo ya utetezi kutoka kwa maofisa hao wote na hatua ambazo itazichukua.
"Kwani Waziri (Waziri Mkuu) alisemaje? Alisema wamewasilisha maelezo yao kwa kamati ya nidhamu."
Akiwasilisha ripoti hiyo Bungeni Alhamisi wiki hii, Bw. Pinda akizungumzia suala vigogo hao kwa nyakati tofauti katika ripoti yake alisema: "Ili kutekeleza Azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.
"...Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.
"Bwana Mwakapugi amekwishawasilisha maelezo yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye Mamlaka yake ya nidhamu katika muda uliotakiwa."
Bw. Luhanjo hakutaka kuingia kwa undani kuhusu muda ambao Ikulu itachukua kabla ya kutoa uamuzi wake juu ya vigogo hao.
*Habari hii imeandikwa na Said Mwishehe na Reuben Kagaruki. Wadau wangu hebu tujadili.
SWALI:Hivi ni watumishi wangapi wa serikali ambao wamekwisha fukuzwa kazi au kusimamishwa kazi pending investigation ambao serikali kwa kutumia mkigezo hicho hapo juu ilifikiria maisha yao na ya familia yao baada ya kupoteza kazi? Hivi wadau mlipofukuzwa pale udsm kwa kupewa masaa mawili muondoke hali hamjui kwa kwenda,wengine kwao tandahimba hawana hata ndugu dar,uukiachilia mbali nauli,je serikali ilipata muda wa kufikiria uamuzi wwake wa kuwatimua kwa masaa 2?Yule Mhasibu kule mbinga aliyehukumiwa miaka 240 jela je,uamuzi wa kumfikisha mahakamani ulifikiria athari zake kwa maisha yake na familia yake?Hivi kwa nini hawa wenzetu wanapata fursa hii ambayo ndugu zetu,wazazi wetu,rafiki zetu nk wanaikosa?Yaani hata kule kusema wasimamishwe kazi pending uthibitisho wa tuhuma zao nalo gumu?are these people very bright such that pale TAKUKURU au AG chambers hakuna mtu anayeweza kukasimu nafasi zao wakati wao wamesimamishwa pending investigation?Wanachi wangapi wamedhalilishwa kwa kusimamishwa kazi pending investigation na baada ya kuwa cleared na tuhuma wakarudishwa kazini?Endapo hii ni due process ya sheria kwa nini watendewe wale tu na wale wasitendewe?
Hali hii inaashiria nini?

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw. Luhanjo alisema Serikali haitaki kukurupuka juu ya hatima ya akina Hosea, Mwanyika na Mwakapugi akisema ni suala zito linalogusa maisha ya watu na familia zao.
"Suala hili tunalishughulikia, unaposhughulikia maisha ya mtu haustahili kutoa uamuzi wa kukurupuka...tunashughulikia, hatukurupuki," alisema na kuashiria kuwa kwa sasa kazi iliyoko mbele yao ni kupima uzito na athari za kila uamuzi utakaofanyika.
"Kabla ya kutoa uamuzi lazima upime kwanza na sio kukurupuka...Hebu fikiria ungekuwa wewe mtu anakuhukumu kufungwa kwa kukurupuka, familia yako na wewe mwenyewe mtaathirika kwa kiasi gani? alihoji.