Tunatafuta business partner atakayetoa 2.5 million

phidejoha

Member
Joined
Jun 23, 2017
Posts
52
Reaction score
26
*Habari wakuu,

Tunatafuta business partner(s) atakayeweza kutoa/kuwekeza angalau 2-2.5 million katika project ya mkaa*

*Raw materials za kuzalisha mkaa huu ni takataka aina zote kasoro makaratasi ya plastic so materials ni nyingi hasa katika miji mikubwa hasa hapa Dar utakapokuwepo huu mradi*

*Mkaa huu utakuwa ni mzito usio na moshi hatarishi na uwakao mara mbili zaidi ya huu tuliouzoea. Pia mkaa huu utakuwa na bei nafuu zaidi ya tuliouzoea hapa itawafanya watu wengi kuukimbilia huu na bei yake itakuwa chini kwa sababu ya urahisi wa upatikanaji wa mali ghafi*

*Masoko: hadi sasa soko la mkaa ni kubwa sana, ukiachana na watumiaji wa majumbani pia kwa nyakati tofauti tulikuwa tukipata oda au connection na kiwanda mojawapo cha kutotoleshea vifaranga kuhitaji nishati hii ila kukosekana kwa mashine yenye uwezo mikubwa basi tumekuwa tukipoteza dili nyingi*

*Tulipofikia na tulipokwama*

*Hadi sasa tupo business partners 5, tumeweza kupata eneo bunju kwa ajili ya ofisi na uzalishaji utafanyikia hapo na pia tumefanikiwa kupata mashine iliyo na uwezo wa kuzalisha takribani tani 3 kwa siku hapo unazungumzia si chini ya 500000 kwa siku baada ya kutoa costs of production*

Tulipokwama na
Tunapohitaji msaada

*Kwa sasa mashine ipo bagamoyo na gharama za kuileta bunju ni roughly 250000, gharama nyingine zitakazofikia/kukaribia 2.5m (including hiyo 250k) ni kwa ajili ya kuandaa kwa haraka miundombinu ya ofisi kuvuta na kufunga umeme wa 3 phase uliopo eneo la tukio*

*Ndugu zanguni nakaribisha partner atakayeweza kututoa tulipokwama na mwisho wa siku atakuwa sehemu ya sisi. Tutakaa, tutamwelekeza zaidi kisha akiona kuwa hii ni fursa kwake kama tuonavyo sisi basi tushirikiane*

*Kwa maelezo zaidi nicheki 0625649078, 0753245261*
 
Bado naona ni faida kwa makaratasi tu. Mmeshafanya utafiti wa masoko????

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumekwishafanya na hadi sasa tumekuwa tukiletewa ODA kutoka kwa wadau wetu wanaofanya hii project ila tatizo ni uwezo wa kuzalisha kiwango kikubwa cha mkaa unaohitajika sokoni.

Tunachojitahidi HAPA ni kujaribu kuongeza kiwango cha production kupitia MASHINE hii KUBWA ZAIDI ili dili au oda zote zinapokuja tuweze kumeet demand
 
je kampuni imesajiliwa?
nikitoa hizo pesa ntapewa asilimia ngapi za umiliki wa kampuni?
endapo pesa zitapatikana baada ya miaka mitano mnaiona wapi kampuni yenu?
je ipo kwenye eneo la makazi au?
 
je kampuni imesajiliwa?
nikitoa hizo pesa ntapewa asilimia ngapi za umiliki wa kampuni?
endapo pesa zitapatikana baada ya miaka mitano mnaiona wapi kampuni yenu?
je ipo kwenye eneo la makazi au?

Hatujafanikiwa rasmi kuisajili kampuni though tulianza hizo process, tuliambiwa gharama ni takribani 300000 wakati kipindi hikohiko tunafakiria namna ya kupata pesa ya mashine so unaweza kuimagine kwa nini zoezi LA usajili liliishia katikati.

Ndani ya 5 years or less tunajiona mbali sana kwa sababu kama tutakuwa na uwezo wa kuproduce 3 tone kwa siku means kwa mwezi tutaproduce si chini ya 60 tone hapo tunazungumzia kipato cha si chini ya 30m per month
KWA trend hiyo tulishapanga kuongeza mashine za kutosha na kufungua plants nyingine katika miji mingine yenye uzalishaji mkubwa wa taka, hapa tutahifadhi mazingira zaidi, tutatengeneza ajira zaidi na tutajiongezea kipato zaidi na serikali pia

Kwa sababu bado hatujakamilisha usajili wa kampuni so umiliki wa hisa utakuwa mgumu ila TULICHOKIPANGA NI KUWA INVESTOR ATAKAYEJITOKEZA ATAKUWA NA HAKI SAWA PAMOJA NASI, ATAKUWA SEHEMU YA SISI KWENYE KUSHAURIANA NK ILI OFISI IFIKIE MALENGO, KAMA TUKIAMUA KULIPANA KIASI FLANI CHA PESA BASI YEYE PIA ATAPATA HICHO, INSHORT ATAKUWA ONE OF THE OWNER OF A BUSINESS.

ENEO LA PRODUCTION SIO LA MAKAZI KUNA OPEN SPACE KUBWA TU.

KWA ALIYETAYARI TUNAWEZA KUKUTANA/KUWASILIANA BY CM/ FACE TUKAELEKEZANA TUKASHAURIANA TUKAFANYA KITU
 
Sajiri kwanza kampuni ili kuweka uaminifu

Thanks kwa ushauri japo naamini bdo linazungumzika hili kwa atakayepatikana tushirikiane kwa pamoja kukamilisha registration then tuje kwenye terms na awe sehemu ya sisi kama ulivyo mpango wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…