Haya mambo huwa mnayakaribisha wenyewe kwenye familia zenu. Mimi nina shida kidogo linapokuja hili suala la kurundika ndugu nyumbani kwa sababu yeyote ile.
Hivi kujifungua ni ishu saaaana mpk mama mkwe wako, mama yako, bibi wa mkweo na ukoo mzima ujae nyumbani kwako? Mimi navyofahamu, siku za kwanza za maisha ya mtoto ni very delicate, sasa kuchukua wabibi kijijini kuwajaza nyumbani wengine wana magonjwa ya kuambukiza wengine wana harufu za ugoro n.k huko ni kumnyima mtoto haki ya kupata pumzi safi.
Kwa kifupi huo ndio mshahara wa maisha ya kiswahili. Sio mtoto kazaliwa tu hata mwezi hajatimiza basi kila mtu aje kumtia mikono yake, wengine wanga, wengine wana TB, ah jamani, badilikeni. Wafukuze wote bakia na mkeo