Wape tu mkuu. Unaogopa nini? Unadhani/unaamini watakifanyia nini? To me, hicho kitovu kikishatoka kwa mtoto hakina tofauti na uchafu mwingine. Ukianza kuamini kuwa ati wanaweza kumdhuru mtoto kama watachukua huo uchafu basi na wewe unaanza kuwa mshirikina. Labda kama unaniambia unahisi hao ndugu wana mpango wa 'kumlisha' huyo mtoto hicho kitovu!Jamani l am not a witchman, I am only protecting my kid, dhidi ya wanaotaka niwape kitovu
Mkeo ndio yuko interested na mambo ya kiuchawiuchawi?Ndio maana mimi nashangaa habari za vitovu hapa, maana mimi mambo hayo nilishamwachiaga Mama mtoto, sina interest yoyote na mambo ya kienyeji.
Kama hujaielewa post yangu hapa hata nijaze ukurasa kukueleza hutonielewa na si lazima unielewe.Mkeo ndio yuko interested na mambo ya kiuchawiuchawi?
Labda tu hawa wanaoshabikia vitovu wangetupa Elimu kwamba je ni kweli mtoto wa kiume akiangukiwa na kitovu anakuwa si riziki, yaani Dushelele linakuwa mlenda? mwenye uelewa juu ya tetesi hizi naomba anijuze sina sababu ya kuanzisha thread nyingine, naomba lift hapa hapa.seriously,haya ni mageni kwangu kuhusu kitovu.sikujua kama mtu anaweza kufanyia ushirikina kuhusu kitovu
dogo, yamekuwa hayo??Dsm dili nyingi sana, sikujua kuwa vitovu ni biashara nzuri, ndio maana hospitali ya Mwananyamala haiishi vituko.......
Haya mambo huwa mnayakaribisha wenyewe kwenye familia zenu. Mimi nina shida kidogo linapokuja hili suala la kurundika ndugu nyumbani kwa sababu yeyote ile.
Hivi kujifungua ni ishu saaaana mpk mama mkwe wako, mama yako, bibi wa mkweo na ukoo mzima ujae nyumbani kwako? Mimi navyofahamu, siku za kwanza za maisha ya mtoto ni very delicate, sasa kuchukua wabibi kijijini kuwajaza nyumbani wengine wana magonjwa ya kuambukiza wengine wana harufu za ugoro n.k huko ni kumnyima mtoto haki ya kupata pumzi safi.
Kwa kifupi huo ndio mshahara wa maisha ya kiswahili. Sio mtoto kazaliwa tu hata mwezi hajatimiza basi kila mtu aje kumtia mikono yake, wengine wanga, wengine wana TB, ah jamani, badilikeni. Wafukuze wote bakia na mkeo
Umeambiwa Tanzania nchi ya kwanza kwa ushirikina, sasa unashangaa nini? Mtoto wa kwanza mara nyingi husababisha ugomvi sana kwenye familia miongoni mwa nduguna mwenyewe kesha ukiomba....
Solution hapo ndogo waite wote waambie huwapi kitovu cha mtoto.... Wewe ndo baba utakaa nacho......
Mwisho wa siku kitapotea tu.....
Sie wengine vitovu tuliambiwa tukavifukie tu.......
Hata hivyo kuwa makini vinatumika kwenye mambo ya nguvu za giza vilevile ndo maana nakwamnia usimpe hata mmoja kati yao..na vita vitakwaisha ukiwa firm.....
Halafu waafrica bwana badala ya kuhombea dhahabu tunagombea vitovu
Wakristo walio safi na wakweli hata kukumbuka habari za kitovu hatukumbukagi,kama wewe ni mkristo jichunguze una matatizo ktk ukristo wako.
Pole Kiranja Mkuu, iyo kitu ipo sana hasa kwa wazazi wetu. Kwanza nakushauri mkabidhi mwanao kwa Mwenyezi Mungu tu, yeye amekupa mtoto na yeye ndiye atakayemlinda mwanao. Wewe kama baba wa mtoto una final say, sio mama yake wala mama mkwe! Waambie ukweli kuwa hutowapa hicho kitovu na kwamba hizo imani zao za kishirikina wewe huzitaki kwenye familia yako. Baada ya hapo kama walikuja kumuuguza mkeo wape nauli warudi kijijini kuangalia nyumba zao na mashamba mana shughuli imekwisha, period!!
nimeambiwa nitarogwa kama nitaendelea kung'ang'ania kitovu cha mwanangu
Labda tu hawa wanaoshabikia vitovu wangetupa Elimu kwamba je ni kweli mtoto wa kiume akiangukiwa na kitovu anakuwa si riziki, yaani Dushelele linakuwa mlenda? mwenye uelewa juu ya tetesi hizi naomba anijuze sina sababu ya kuanzisha thread nyingine, naomba lift hapa hapa.