Tunatakiwa kusimama kwenye maandiko ya dini ili kutenda haki kwa kila mtu

Tunatakiwa kusimama kwenye maandiko ya dini ili kutenda haki kwa kila mtu

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
HATUWEZI KUHUBIRI
HAKI NA USAWA
HUKU TUKIWA WENYEWE
HATUFANYI
HAKI NA USAWA WENYEWE
TUKILAZIMISHA MUONEKANO TUSIO NAO TUTAKUWA WANAFIKI
Nilisikika katika Ulimwengu wa kiroho huko Ndotoni nikitoa somo ili kubadilisha mentality za Uchawa na upigaji.
Nikaanza
Mwenyezi Mungu ametupatia Akili ili tuzitumie kuzifanyia ibada
Tunapokubaliana na Wanajamii Kuhusu Uadilifu na Uaminifu unaozaa Haki na Usawa tunapoutekeleza kwa kufuata kikamilifu Ilani katiba kanuni Miongozo na Taratibu hapo ndipo tunakuwa tumefanya ibada ya kweli kwa Mwenyezi Mungu Ambaye anapenda tuishi tukimpinga Shetani kwa kujiepusha na kauli za hila , ujanja ujanja na utapeli.
Tunapomkiuka Mwenyezi Mungu kimwili ni Kama tunaonekana Bado wenye akili ila kiroho tunakuwa ni viumbe wampendao Shetani wenye Mapungufu Makubwa ya Akili wenye kuiendekeza Dunia ipitayo Kama upepo
Nakumbuka Tarehe 16/08/2024
Shekhe Othman Khamis Juma
Imam Masjid Mtoro
Alisema
Tatizo Mwenyezi Mungu amerejea Mara nyingi kwenye Qur aan
Anasema watu wengi hawana akili
Walio na akili wanataka Amani .
Sasa watu wengi hawana akili
Ina Maana wamebaki watu wachache wenye akili
Wenye akili wanataka Amani
Mungu atujaalie kuwa katika wao ( wenye akili)
Na wao wenye akili wanaitunza Amani.
Mwisho wa kunukuu
Watu wenye akili hawawatendei Mafukara fyongo fyongo
Wanatenda walivyoapa kwa Mwenyezi Mungu kwa hakillillah
Ukiona una cheo halafu umejwa viburi Ubaguzi na Upendeleo hutendi haki ujuwe Wewe huna akili na hutunzi Amani Bali unachochea machafuko kwa Ubinafsi wako wa kubeba watu waovu na kuamsha hisia za Mafukara wajihisi kugandamizwa
Siasa Sio Uongo
Alisha sema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Nyakati za nyuma
Hivyo hatupaswi kutumia Uongo kwenye siasa kwa sababu siasa ni Maisha ya watu walioumbwa na Mwenyezi Mungu wenye kututegemea watu wenye akili tuwasaidie tuwainue na Sio kutumia maneno ya kishetani ya Uongo Uongo kuwafanya Mafukara wazidi kuwa Duni .
Wakili Jasiri na Msomi
Boniface Mwabukusi
Rais wa TLS
Akizungumza na Wanahabari Tarehe 20/08/2024
Alisema
Nataka kusema
Mtu pekee asiyefanya siasa ni ( mtu) Maiti
NI maiti tu ndo hawezagi siasa kwa sababu sharti yake ni kuoza
Lakini mtu Yeyote Mwenye uhai na mwenye utashi anafanya siasa .
Siasa iko kwenye kila sekta .
Lakini Kuna siasa ya sheria
Kuna siasa ya Dini
Kuna siasa ya uchumi
TLS inafanya siasa ya sheria
Mwisho wa kunukuu
Siasa ni Ukweli unaohusisha ibada zetu kwa Mwenyezi Mungu.
Ibada Sio kwenda nyumba za ibada tu.
Ibada ni Pamoja na kuona tumekubaliana wote kutii na kutenda kwa Mujibu wa Ilani katiba kanuni Miongozo na Taratibu huku tukiwa tumeapa na kushika vitabu vitakatifu Vya Mwenyezi Mungu kwa imani zetu huku tukiiahidi mbele ya Jami kuwa watu wema
Tuanapaswa kuzizingatia ibada hizi tuzoziahidi kwa Wanajamii ambao wengi wao ni Mafukara .
Padre Dkt Charles Kitima
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC
Nakumbuka Tarehe 08/02/2024
Alisema
Sisi tulikuwa na Mkristo wetu anaitwa Benedikito
Yule aliyeanzisha Mashirika haya tunayoyaona Peramiho kule , kule Songea, Mtwara na Lindi
Yeye alikuwa anasema
Kazi unayoifanya kwa Nia njema yenyewe ni Sala .
Wee ifanye hiyo kazi kwa Nia njema inageuka kuwa Sala.
Mwisho wa kunukuu
Tujikague Viongozi wenzangu
Tumepewa Vyeo ili kuwatumikia watu kwa Haki na usawa
Huu ujasiri wa kusimama hadharani tukihubiri Amani na upendo Kisha Sisi tunakuwa Wabaguzi na Wapendeleaji
Kwa tabia hizi za kinafiki tunajiona tunamtumikia Nani !?!?!
Kwa Nini hatujipendekezi kwa Mwenyezi Mungu ili tuzidi kubarikiwa kwa Yale tunayotamani yatokee kwa Haki !?!
Kwa Nini tunapenda ushetani wa kuwalea watu waovu na kuwaonea Mafukara na Watumishi wa Umma hata kwa Makosa TU ambayo yanahitaji tuwaonye !?!?
Imani zetu za kidini ziko wapi kwa matendo haya tuyatendayo !?!?
Nakumbuka Tarehe 04/08/2024
Shekhe Kombo Ally Fundi
Akitoa Mawaidha
Alisema
Ukiona Allah amekufanya Wewe ni Mtumishi wa Dini yake kwa namna Yeyote ile juwa Allah anakupenda
Na Ukiona hautaki kuitumikia Dini ya Allah hata kidogo ( ujuwe Wewe ) haujapendwa ( na Allah)
Na ukiwa haujapendwa maanake haujajipendekeza
Jipendekeze kwa Allah (ili) upendwe.
Mwisho wa kunukuu
Tunaopindisha ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu ili kuwabeba Maswahiba zetu na kulinda safu ili tuzitumie siku za usoni tulisha jifikirisha maneno haya !?!?
Je tulisha fikiri Kuna kufa !?!?!?
Hapa tunagundua kwabisa Tena kwa mwandiko wa herufi kubwa kubwa ya kwamba
KUNA BAADHI YA VIONGOZI
WAMEMUASI
MWENYEZI MUNGU WAKIWA WANA MIONEKANO YA UCHA MUNGU.
WAMEJENGA USWAHIBA NA SHETANI
WANAKULA VIAPO HUKU DHAMIRA YAO YA NDANI IKIWA NI WIZI NA HUJUMA KWA MAFUKARA
HAWANA UTII KWA KAULI CHANYA ZA VIONGOZI WA KITAIFA
WANAJITAMKISHA KWA MANENO YA KIUONGO UONGO KUHUSU
HAKI
NA
USAWA
HUKU MATENDO YAO YAKIWAAIBISHA KWA KUTO KUENDANA NA KAULI WAZITAMKAZO
WANAHUBIRI
UADILIFU
NA
UAMINIFU
HUKU WAKITENDA NA KUAMUA KINYUME NA WANAVOTAMKA
HAWA NDIYO VIONGOZI MASHETANI WENYE MIONEKANO YA MIILI NA MAVAZI KAMA VILE NI BINAADAMU KUMBE SIVYO.
Nakumbuka Tarehe 02/06/2024
Shekhe Kombo Ally Fundi
Akitoa Mawaidha
Alisema
Allah Subhahanahu Wataalla anasema
Tumewafanya Mashetani.
Mashetani Majini wawe ni Marafiki Wapenzi wa ( watu) wale ambao hawaamini
Mtu Ambaye Hana imani ( ya Mwenyezi Mungu) ndiye ( mtu) Mwenye urafiki na ( Shetani) Jini.
Kwa hiyo Sheitwaan Mwenzie
Yule Sheitwaan amekwenda kumtafuta ( mtu) asiye na imani amekuwa Sheitwaan Mwenzake
Rafiki yake
( Allah anasema) tumewafanya Mashetani kuwa ni Marafiki kwa ( watu) wale wasiokuwa na imani .
Lakini Muumin ameambiwa ( na Allah ) Sheitwaan kwenu ni Adui .
Mfanyeni Adui.
Mwisho wa kunukuu
Mifumo ya nchi yetu inasisitiza Utawala Bora
Utawala wa sheria
Na Utawala wa sheria lazima uonekane ukitendeka kwa Vitendo huku tukijiepusha na Vitendo vya
Kiupendeleo
Na
Kiubaguzi
Haiwezekani watu wauze Ofisi ya chama Kinyume na utaratibu Kisha wapewe ulinzi na kuendelea kudumu Madarakani na Kisha Wahusika tuwe tunajitangaza kuwa Sisi ni watu wa kutenda Haki
Huu ni Unafiki ambao haulisadii Taifa.
Professor Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
Kwa Sasa Waziri wa Sheria
Nakumbuka Tarehe 07/05/2024
Alisema
Kwa hiyo tubadilike .
Mwisho wa kunukuu
Kweli kabisa tubadilike Sasa tuenende Kama watu wenye wingi wa hofu ya Mwenyezi Mungu
Nimeisha wapeni Mwangaza wa kuufuata utakao tutoa gizani
Wa kusimama kwenye maandiko ya Dini zetu kwa Imani zetu, Ilani katiba kanuni Miongozo na Taratibu pasipo Uongo Uongo na Ubinafsi , Huu ndiyo Mwanga pekee ambao umekuwa ukisisitizwa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuutumia kutenda haki kwa mafukara walio wengi
Tuwe watu tunaoendana na Yale tunayoyahubiri.
Tusiwe
Banu sakanu
Sakanu Banu
Nakumbuka Tarehe 10/08/2024
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Akiwa katika kikao Cha Maafisa Ugani na Wana Ushirika ikulu Chamwino
Alisema
Mwanga umeonekana
Kwa hiyo ni Sisi Viongozi Sasa tusimame tulisimamie na twende mbele
Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka Ndotoni katika Ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikiwa kimya





Kidumu chama Cha Mapinduzi


Mathias Mugerwa kahinga
 
Back
Top Bottom