Tunatakiwa tujikomboe na utumwa wa pesa

Tunatakiwa tujikomboe na utumwa wa pesa

Dede 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
1,182
Reaction score
2,248
Habari wakuu.
Kwenye Jamii yetu watu wengi ni watumwa wa pesa yaani unakuta mtu anafanya kazi kwa bidii sana hadi anakosa muda wa kukaa na familia yake yote sababu ya pesa.

Sisemi ya kwamba tusifanye kazi kwa bidii, la hasha. Ila tunatakiwa kuwa huru kufanya tutakacho maishani bila kuamriwa na mtu. Na njia pekee ya kupata uhuru huu ni kupata elimu ya kifedha(financial intelligence),hapa sizungumzii uhasibu ila nazungumzia elimu ambayo itakupa uwezo wa kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika eneo husika na kuzifanyia kazi ili kuongeza kipato.

Ni watu wachache sana wanaotambua kuwa wanatawaliwa na pesa na wachache wanaofanikiwa kujikomboa.

Njia pekee ya kupata financial intelligence ni kupitia kusoma vitabu vya masuala ya fedha na kwa bahati mbaya sana elimu hii haitolewi mashuleni.

Moja kati ya kitabu ninacho recommend mtu asome ni cha "RICH DAD,POOR DAD" kilichoandikwa na Robert Kiyosaki.

Mimi yangu ni hayo tu,kazi imebaki kwenu.
 
Attachments

Vitabu havikupi utajiri Wala undani wa ufasaha wa fedha.. kwa mtazamo wangu tu ila labda nikukumbushe kitu.

Ni wanadamu wote tunatafuta pesa/Mali lakini Ni wachache Sana wanaipata pesa kwa utoshelevu wote.

Hajiangaishae kutafuta Mali / pesa anahanagika bure. (Japo bidii inaleta matunda take)

Laiti ungelijua Yale yanayoleta utajiri na nguvu,,,❤️❤️ lakini yamefichika tusiyaone maana hatujayataka kuyafanya.
 
pesa lazima ucheze kwanza baada ya hapo fahamu ndio zinakurudia.hii kama unajitambua na kukaa na watu wa maana kipindi cha msoto baada ya kupungukiwa au kuipoteza kabisa pesa ulioichezea achana na mambo ya vitabu ingia kwenye mtanange mubashara ndugu

kama wewe ni mtu wa kujifunza kupitia makosa wala pesa haiwezi kukushinda nguvu
 
Tz watu wana mikwanja sema wanajificha sana

Wanasiasa

Wafanyabiasha

Watumishi

Haya makundi wapo wenye mipunga mirefu ila wanajificha kama ukimwi
 
Kuna tofauti kati ya kuwa na mkwanja na kuwa na uhuru wa kifedaha. Mtu mwenye uhuru wa kifedha hata akifukuzwa kazi leo anauhakika wa kusurvive ila watu wasio na uhuru huu wakifukuzwa kazi wataanza kusota.
 
Vitabu havikupi utajiri Wala undani wa ufasaha wa fedha.. kwa mtazamo wangu tu ila labda nikukumbushe kitu.

Ni wanadamu wote tunatafuta pesa/Mali lakini Ni wachache Sana wanaipata pesa kwa utoshelevu wote.

Hajiangaishae kutafuta Mali / pesa anahanagika bure. (Japo bidii inaleta matunda take)

Laiti ungelijua Yale yanayoleta utajiri na nguvu,,,❤️❤️ lakini yamefichika tusiyaone maana hatujayataka kuyafanya.
Kuwa huru kifedha si lazima uwe na majumba na magari ya kifahari au uwe na Mali nyingi lakini ni suala wewe kuingiza hela bila ya kuingilia muda wako binafsi na wa familia yako.Sio unafanya kazi kwa bidii kiasi cha kwamba unashindwa kutimiza wajibu wengine katika family na jamii.Na unakuta bado hela unayopata haitoshelezi.
 
Habari wakuu.
Kwenye Jamii yetu watu wengi ni watumwa wa pesa yaani unakuta mtu anafanya kazi kwa bidii sana hadi anakosa muda wa kukaa na familia yake yote sababu ya pesa.

Sisemi ya kwamba tusifanye kazi kwa bidii, la hasha. Ila tunatakiwa kuwa huru kufanya tutakacho maishani bila kuamriwa na mtu. Na njia pekee ya kupata uhuru huu ni kupata elimu ya kifedha(financial intelligence),hapa sizungumzii uhasibu ila nazungumzia elimu ambayo itakupa uwezo wa kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika eneo husika na kuzifanyia kazi ili kuongeza kipato.

Ni watu wachache sana wanaotambua kuwa wanatawaliwa na pesa na wachache wanaofanikiwa kujikomboa.

Njia pekee ya kupata financial intelligence ni kupitia kusoma vitabu vya masuala ya fedha na kwa bahati mbaya sana elimu hii haitolewi mashuleni.

Moja kati ya kitabu ninacho recommend mtu asome ni cha "RICH DAD,POOR DAD" kilichoandikwa na Robert Kiyosaki.

Mimi yangu ni hayo tu,kazi imebaki kwenu.
Je, wewe uko na hio financial freedom?na kama uko nayo naomba uthibitishe sasa hivi. Mambo ya nadharia sipendagi.
 
Usijali Tomaso mi ninayo. Na we unaweza kuwa nayo endapo uta utajiongezea hekima yako ya kifedha na ukaamua kutake risks.
 
Habari wakuu.
Kwenye Jamii yetu watu wengi ni watumwa wa pesa yaani unakuta mtu anafanya kazi kwa bidii sana hadi anakosa muda wa kukaa na familia yake yote sababu ya pesa.

Sisemi ya kwamba tusifanye kazi kwa bidii, la hasha. Ila tunatakiwa kuwa huru kufanya tutakacho maishani bila kuamriwa na mtu. Na njia pekee ya kupata uhuru huu ni kupata elimu ya kifedha(financial intelligence),hapa sizungumzii uhasibu ila nazungumzia elimu ambayo itakupa uwezo wa kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika eneo husika na kuzifanyia kazi ili kuongeza kipato.

Ni watu wachache sana wanaotambua kuwa wanatawaliwa na pesa na wachache wanaofanikiwa kujikomboa.

Njia pekee ya kupata financial intelligence ni kupitia kusoma vitabu vya masuala ya fedha na kwa bahati mbaya sana elimu hii haitolewi mashuleni.

Moja kati ya kitabu ninacho recommend mtu asome ni cha "RICH DAD,POOR DAD" kilichoandikwa na Robert Kiyosaki.

Mimi yangu ni hayo tu,kazi imebaki kwenu.
Baada ya kusoma hicho kitabu umekuwa Tajiri?
 
Kuna tofauti kati ya kuwa na mkwanja na kuwa na uhuru wa kifedaha. Mtu mwenye uhuru wa kifedha hata akifukuzwa kazi leo anauhakika wa kusurvive ila watu wasio na uhuru huu wakifukuzwa kazi wataanza kusota.
Uhuru wa kifedha bila pesa inakuwaje hebu dadavua kidogo mkuu
 
Dah naona watu wanamwandama jamaa kuhusu usomaji wa vitabu,Kusoma vitabu inakusaidia kuongeza maarifa ambayo moja kwa moja yanaweza kuchochea kwa namna moja ama nyingine mabadiliko ktk maisha yako kama utaapply maarifa hayo kwa vitendo. Kusoma vitabu kunamfungua mtu kwenye kifungo au changamoto kwa kupata experience ya watu waliopata changamoto kama zake ktk vitabu.
Sera yetu ya elimu ndo inatuua vitabu vingi vyenye maarifa konki ambayo yanaweza kua chachu ya ukombozi wa fikra,maendeleo binafsi na uchumi kwa ujumla viko ktk lugha ya KIINGEREZA,na hii ndo fimbo wanayoitumia watawala kutuchapia wanadhoofisha mfumo wa elimu yetu ili tuwe taifa la watu wenye fikra duni,tusiojua kuhoji,turidhike na hali yetu na tuone wao ndo wako sahihi huku wao wakiwaandaa watoto wao kua watawala kwa kuwapeleka shule nzuri na kuwahimiza kusoma vitabu waongeze maarifa wake kuwatawala mashibiki kindakindaki ambao kutwa story zao ni Simba na Yanga aisee 😔.
GOD HAVE MERCY ON US...
 
Uhuru wa kifedha bila pesa inakuwaje hebu dadavua kidogo mkuu
Uhuru wa kifedha ni uwezo wa mtu kuingiza hela bila kumtegemea mtu yeyote au kuendeshwa na mtu yeyote. Kuna watu wana pesa lakini unakuta wanamtegemea mtu fulani kupata hizo pesa endapo huyo mtu akiwatema basi pesa zao zitaisha. Mfano mafreemason na baadhi ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom