Tunatarajia baada ya korosho Serikali itanunua mahindi yote ya zaida yaliyorundikana Ruvuma, Iringa, Mbeya, Songwe na Rukwa

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Leo Rais John Pombe Joseph Magufuli (Sina hakika na mpangilio wa majina yake) amekagua magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yatakayotumika kusomba Korosho za wakulima zitakazonunuliwa na serikali endapo wanunuzi binafsi watashindwa kuthibitisha kununua korosho hizo ifikapo Jumatatu saa 10 jioni.
Ni jambo jema serikali kujali wananchi wake kwani ndio waliowaweka madarakani. Lakini kwa vile serikali hii siyo ya kibaguzi, tunataka nguvu hii inayotumika sasa kuokoa soko la Korosho, itumike pia kwa zao la Mahindi ambalo nalo limewadodea wakulima baada ya Sera mbovu ya serikali ya kuwazuia wakulima wa mikoa niliyotaja kuuza mahindi yao kwenye soko huria hususan nchi jirani za Zambia, Kongo DRC, Malawi na Msumbiji. Isipofanya hivyo utakuwa ni aina nyingine ya ubaguzi na itakuwa ni kutowatendea haki sawa wakulima wa mahindi kama wanavyofanyiwa sasa wakulima wa Korosho.
 
Tunaanza na mazao mkakati kwanza
Mahindi ni zao kuu la chakula ujue... Karibu kila kaya ugali unaliwa, wakati korosho kuna watu wengi hawajahi hata kuzioni, wanasikia tu kny habari!
 
Mahindi ni zao kuu la chakula ujue... Karibu kila kaya ugali unaliwa, wakati korosho kuna watu wengi hawajahi hata kuzioni, wanasikia tu kny habari!

Kuhusu kuziona korosho ni kosa la nani sasa..? La kwao au la serikali..!
 
Zao La chakula linalimwa kula ingawa Huwa tunauza pia ziada.
Korosho Huwa tunauza Kama zao La biashara
 
Nyanda za juu kusini nyie sio sehemu ya Tanzania hii ya awamu ya tano, pambaneni kivyenu.
 
Nyanda za juu kusini nyie sio sehemu ya Tanzania hii ya awamu ya tano, pambaneni kivyenu.
Hili likitokea ndo tutajua Nyanda za juu kusini siyo sehemu ya Tanzania, Lakini kwa sasa acha tuvumilie maana tunajua baada ya Kusini ni zamu yetu kuletewa Neema.

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…