Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Leo Rais John Pombe Joseph Magufuli (Sina hakika na mpangilio wa majina yake) amekagua magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yatakayotumika kusomba Korosho za wakulima zitakazonunuliwa na serikali endapo wanunuzi binafsi watashindwa kuthibitisha kununua korosho hizo ifikapo Jumatatu saa 10 jioni.
Ni jambo jema serikali kujali wananchi wake kwani ndio waliowaweka madarakani. Lakini kwa vile serikali hii siyo ya kibaguzi, tunataka nguvu hii inayotumika sasa kuokoa soko la Korosho, itumike pia kwa zao la Mahindi ambalo nalo limewadodea wakulima baada ya Sera mbovu ya serikali ya kuwazuia wakulima wa mikoa niliyotaja kuuza mahindi yao kwenye soko huria hususan nchi jirani za Zambia, Kongo DRC, Malawi na Msumbiji. Isipofanya hivyo utakuwa ni aina nyingine ya ubaguzi na itakuwa ni kutowatendea haki sawa wakulima wa mahindi kama wanavyofanyiwa sasa wakulima wa Korosho.