USHAURI JUU YA MAZDA RX 8
Hii sikushauri boss wangu, fikiria gari nyingine ya kispot, au la ujiandae na changamoto zake haswa za injini mwishowe uje kuweka injini za magari mengine huku ukifurahia bodi lake la kimichezo.
1. Inakuja na injini ndogo iliyoundwa kuzalisha nguvu kubwa kuliko uwezo wake hivyo kuifanya ifanye kazi za juu yake na matokeo yake ni kuwahi kuchoka
2. Licha ya Cc ndogo yaani Cc 1300 (Inakadiriwa kwenda km za juu kiasi cha km 12/L)
3. Kwenye nguvu, ni gari inayozalisha nguvu kubwa sawa na gari za Cc 3000 mpaka 3500
4. Pia inaelezewa na wengi walioitumia kuwa na changamoto kwenye uwakaji (stata) baada ya kutembea km kadhaa
5. Masega yake au Catalytic Converter inawahi kuchoka kutokana na muundo wake wa injini
6. Ili izalishe nguvu kubwa tunayoishuhudia, gari inalazimika kuchoka mafuta mengi na matokeo yake ni uchafuzi wa mazingira
Kwa ujumla gari hii haina rekodi nzuri boss na ilikusudiwa kuuzwa Amerika ya Kaskazini lakini haikufanya vizuri kupelekea Mazda watangaze kuasitisha uzalishaji wake 2012
Ukiihitaji hivyo hivyo, karibu tukuagizie kwa jumla ya gharama zote 17m