USAJILI WA KAMPUNI.
Kampuni ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye nia ya kufanya biashara halali na kuusajili mjumuiko huo chini ya Sheria ya kampuni.
Aina za Kampuni
1. Kampuni ya kigeni
2. Kampuni binafsi
3. Kampuni ya umma
Faida za Urasimishaji Kampuni ni zipi?
1. Kuipatia utu wa kisheria biashara yako
2. Kutambulika na taasisi za fedha mf. benki wakati wa kufungua akaunti.
3. Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
4. Kupanua wigo wa kufanya biashara kubwa, mf. biashara za kimataifa
5. Urahisi wa kuitangaza kampuni kwa urahisi na kupanua wigo wa wateja.
Vigezo vya kusajili Kampuni
1. Mwombaji anatakiwa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA
2. Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA ya kila mwanahisa
3. Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA au pasi ya kusafiria kwa raia wa kigeni na namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) ya kila mkurugenzi.
USAJILI WA MAJINA YA BIASHARA
Jina la biashara ni nini?
Jina la biashara ni utambulisho wa biashara fulani inayofanywa na mtu au kikundi cha watu. Hivyo mtu mmoja au kikundi cha watu wasiozidi 20 wanaweza kusajili jina la biashara. Mfano wa majina ya biashara ni Ali Entreprises, Rose Beauty Salon au John Urassa Investments, n.k
Faida za Urasimishaji wa Jina la Biashara ni zipi?
1. Kulipa jina la biashara utambulisho wa kisheria
2. Kulinda jina la biashara lisitumiwe na mtu mwingine.
3. Kutambulika na taasisi za fedha mf. benki (wakati wa kufungua akaunti).
4. Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
5. Kuifanya biashara yako kutambulika kisheria.
6. Kuitangaza biashara kwa urahisi na kupanua wigo wa wateja.
Vigezo vya kusajili Jina la biashara.
1. Jina la biashara linalokubalika kisheria.
2. Mwombaji awe Mtanzania.
3. Awe na umri kuanzia miaka 18.
4. Namba ya kitambulisho cha taifa (NIN)
5. Namba ya simu iliyosajiliwa ya kwake binafsi.
6. Anuani ya baruapepe hai (binafsi)
7. Anuani ya eneo la biashara.
8. Anuani ya makazi ya mmiliki au wamiliki wa biashara.