Mzee Mapenzi
Senior Member
- Jan 9, 2019
- 122
- 439
Mkoa mmoja ndani ya Kanda ya ziwa, wikendi kama hizi hukosi kusikia kelele za muziki wa kikopo(kipazasauti) na spika kubwa iliowekwa juu ya pipa na kuninginizwa kidogo juu ili mdundo upatikane. Kiingilio ilikuwa ni mia mbili tu na kunapopigwa huo muziki kumezungushiwa wigo wa masanzu ambayo ahsubuh huondolewa baada ya kila mtu kusambaa.
Sasa mida ya ahsubuh vijana tulikuwa tunashiriki shuguli za kilimo na kisha mchana kama huu tupo chini ya mti na kinyozi anatomia kitana na wembe.
Mitindo maarufu ni panki na Afro.
Disko sasa utakuta mwanamke ni mmoja na hawazidi watano,kila mtu anawangalia, mbabe ndo utacheza na demu au unaejua jua kuhonga jojo(big g,)
Disko haliwezi kuisha bila ngumi kuchapwa na chanzo kikubwa ni demu.
Na mwisho wa disko lazima demu mmoja abebwe kwa lazima na kundi lenye nguvu kupelekwa geto la mbabe wa kundi.
Wanyonge wanabaki kuangalia tu.
Kipindi hicho hamna simu ila taarifa za madisko vijiji vya mbali zilikuwa zinatufikia haraka na maandalizi huanza.
Wajasiliamali hawakosekani, wauza pipi na viboksi vya jojo(big g) waliuza japo kudhulumiwa ni jambo la kawaida....
Vipi na wewe umewahi kushiriki disko la aina hii na vipi kunyoa nywele kwa mkasi na wembe na kitana?
***
Nb; Mzee mapenzi nasema hivi; uzi huu hawauhusu vijana wa 2000.