Ukweli Babu yangu kwa Baba, alikuwa mtata sana yule mzee, na mimi ndiyo nilipewa jina lake, nakumbuka matukio machache sana ya yule mzee,
Kwanza alikuwa kila jioni akienda kulewa lazima apigane, na alikuwa anawatukana matusi yanguoni na maudhi mengi hajali na sasa walikuwa wanamsubiri njiani wamfundishe adabu. Yule mzee bwana alikuwa anakita fimbo yake chini. Anaisimika. Sasa jamaa watapigana na iyo fimbo mpana mzee anaingia nyumbani kaisha lala. Alfajiri wanakuja kushituka mtu hayupo na walikuwa wanapigana wenyewe.
Yule mzee alikuwa hapishani na nyoka. Kila nyoka lazima anamchukua anamleta nyumbani anamfuga, siku moja nimetoka shule mchana nikaenda kwa bibi, jikoni nipewe chakula. Bibi akaangalia nikae wapi kanielekeza nikalie mfuko ile ya mbolea , sasa kumbe mle kwenye mfuko kuna chatu, kina nikikaa natereza najitengeneza nakaa ten, hivyo hivyo, mwisho bibi akaona napata shida akaniuliza kulikoni , akasea alaaa kuna vitu vya babu yako humo. Basi akanipa kigoda alichokuwa amekalia yeye akakaa chini. Nilipomaliza kula nikataka kuona mle kwenye mfuko kuna nini, bibi kanikatalia, utoto bwana ! Alivyojipindua bibi nikacheki bwana ,duuuu. Nikatoka baruu.
Siku nyingine bwana wakaja watu kuiba ng'ombe, maana babu alikuwa na ng'ombe hawapungui elfu mbili , na aliwafahamu wote kwa rangi, na aliwapa majina, kulingana na mazingira ya kuzaliwa, basi kuamka asubuhi bwana ng'ombe wameibwa madume kadhaa, baba wadogo wakamwambia babu wawafuate, babu kasema waacheni watarudi wenyewe, kama muujiza vile bwana. Wale ng'ombe walirudi mbio za ajabu wamenyenyua mikia juu juu, haikwisha wiki wale wezi wakaja kujieleza wenyewe,
Nacho sikitika yule babu hakuniachia utaalamu, yaani acha tuu, wakati anakufa alikuja kuniaga. Akalia sana akaniambia maneno machache, ninayakumbuka hata leo, lakini nilikuwa mdogo sikuweza kuelewa anamaanisha nini wakati ananiaga. Nilikuwa form one.