Tunatokea familia za kichawi hapa mahala petu pa kukutana

Ahahahaha mkuu umetisha tutakupa cheo uwe mwenyekiti wetu na mshana atakuwa katibu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahahahaha mkuu umetisha tutakupa cheo uwe mwenyekiti wetu na mshana atakuwa katibu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapana, mshana jr

Huyu anaroho ya kichawi lakini anashindana mno na anahangaika namna ya kuikimbia japo huwa anatumiwa huku akiwa hajuwi, huyu yuko kwenye utumwa mkuu na yupo kwa sababu za msingi.

Anaifanya shughuri ya kichawi huku akiwa hajui na anaichukia mnoo.

Kwa sasa anapambana sana na nafsi yake mkuu

Mimi siwezi kuwa mwenye kiti kwani hua nina mdomo CHAFU mnoo kiyu ambacho mwenyekiti wa shughuri hizi hafai kamwe, labda niwasaidie kigooo kuna bint mmoja humu anastahili sana kwani yeye bado moto wa kichawi anao

Kwa mimi haiwezekani kwani niko kwenye harakati za kulikimbia hili pepo mkuu
 
Ukweli Babu yangu kwa Baba, alikuwa mtata sana yule mzee, na mimi ndiyo nilipewa jina lake, nakumbuka matukio machache sana ya yule mzee,
Kwanza alikuwa kila jioni akienda kulewa lazima apigane, na alikuwa anawatukana matusi yanguoni na maudhi mengi hajali na sasa walikuwa wanamsubiri njiani wamfundishe adabu. Yule mzee bwana alikuwa anakita fimbo yake chini. Anaisimika. Sasa jamaa watapigana na iyo fimbo mpana mzee anaingia nyumbani kaisha lala. Alfajiri wanakuja kushituka mtu hayupo na walikuwa wanapigana wenyewe.
Yule mzee alikuwa hapishani na nyoka. Kila nyoka lazima anamchukua anamleta nyumbani anamfuga, siku moja nimetoka shule mchana nikaenda kwa bibi, jikoni nipewe chakula. Bibi akaangalia nikae wapi kanielekeza nikalie mfuko ile ya mbolea , sasa kumbe mle kwenye mfuko kuna chatu, kina nikikaa natereza najitengeneza nakaa ten, hivyo hivyo, mwisho bibi akaona napata shida akaniuliza kulikoni , akasea alaaa kuna vitu vya babu yako humo. Basi akanipa kigoda alichokuwa amekalia yeye akakaa chini. Nilipomaliza kula nikataka kuona mle kwenye mfuko kuna nini, bibi kanikatalia, utoto bwana ! Alivyojipindua bibi nikacheki bwana ,duuuu. Nikatoka baruu.
Siku nyingine bwana wakaja watu kuiba ng'ombe, maana babu alikuwa na ng'ombe hawapungui elfu mbili , na aliwafahamu wote kwa rangi, na aliwapa majina, kulingana na mazingira ya kuzaliwa, basi kuamka asubuhi bwana ng'ombe wameibwa madume kadhaa, baba wadogo wakamwambia babu wawafuate, babu kasema waacheni watarudi wenyewe, kama muujiza vile bwana. Wale ng'ombe walirudi mbio za ajabu wamenyenyua mikia juu juu, haikwisha wiki wale wezi wakaja kujieleza wenyewe,
Nacho sikitika yule babu hakuniachia utaalamu, yaani acha tuu, wakati anakufa alikuja kuniaga. Akalia sana akaniambia maneno machache, ninayakumbuka hata leo, lakini nilikuwa mdogo sikuweza kuelewa anamaanisha nini wakati ananiaga. Nilikuwa form one.
 
Lakin mkuu kwa hayo maelezo yako hapo juu unatosha kabisa kuwa mwenyeketi wetu humu ndan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh mkuu huyo babu yako alikuwa kiboko nan kaachiwa mikoba kweenye ukoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikivuta bange zangu na uchawi wako unadunda
 
Nakumbuka niliwahi kupiga sana mtoto wa mganga/ mchawi mmoja, huyu mtoto alikuwa mkubwa kwangu Ila alikuwa mwizi balaa!! Nilipiga sana! Nikatishiwa sitaamka kesho yake.....
Ni mwaka wa 20 sasa! Mchawi alishakufa siku nyingi...huyo mwanae kawa mlevi tu kijijini!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…