SoC04 Tunatokomezaje viongozi machawa serikalini?

SoC04 Tunatokomezaje viongozi machawa serikalini?

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mrs Jucbreezy

New Member
Joined
May 3, 2024
Posts
2
Reaction score
2
TUNAWEZAJE KUTOKOMEZA VIONGOZI MACHAWA SERIKALINI
Tangu nchi yetu ya Tanganyika ipate uhuru mwaka 1961 tumekuwa na katiba tofauti tofauti zinazoongoza taifa hili, ambapo katiba hizi zimekuwa zikitoa miongozo na kanuni mbalimbali jinsi taifa hili litakavyo endeshwa. Na mpaka sasa nchi ya Tanzania inaendeshwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo mimi naiona katiba hii kuwa ndio chanzo cha viongozi machawa serikalini.

Katiba hii imempa mamlaka makubwa sana Rais ambapo Ibara ya 36 ya katiba hii inaeleza mamlaka ya Rais kuanzisha na kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka kama vile Majaji, mawaziri na naibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu wa wizara na viongozi wengine. Ibara hii inawabana wale viongozi wa kuteuliwa katika kutekeleza majukumu yao kwani wamekuwa wakifanya kazi ili kumridhisha yule aliyewateua (Rais) na sio kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi, hali imeendelea kuwa mbaya hasa katika awamu hii ya sita ya uongozi ambapo tumeshuhudia wimbi kubwa la viongozi likiimba nyimbo za kusifu na kuabudu ili tu kumridhisha yule wanaemtumikia. Iliibuka mijadala mingi bungeni ikiwemo suala la DP WORLD viongozi wetu wengi walifunga vinywa vyao pale walipotakiwa kuusema ukweli na kubakia kuunga mkono hata wasijue wanaunga mkono kitu gani?

Hali ikiendelea hivi nchi hii inaweza kuwa shirika la machawa lisilokuwa na viongozi wawajibikaji, rai yangu kwa serikali ili kuweza kuleta mabadiliko chanya napendekeza viongozi wote wanao wawakilisha wananchi/ wanaowatumikia wananchi wachaguliwe kwa kupigiwa kura na sio kuteuliwa na Rais kama ambavyo Ibara ya 67 ya katiba imeianisha sifa za mtu kuwa mbunge vivyo hivyo tupewe sifa za mtu kuwa mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa n.k ili nafasi hizi ziweze kugombewa viongozi hao wachaguliwe na wananchi na sio kuteuliwa. Lakini pia katika hili mtu aruhusiwe kugombea kama mgombea binafsi asitokee katika chama chochote cha siasa maana tumeona viongozi wengine wakifanya kazi kwa kuitumikia ilani ya chama na sio kuwatumikia wananchi. Tunatakiwa kufika mahali ambapo mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya atasimama jukwaani kuomba kura kwa wananchi huku akiwaeleza atafanya nini akipata nafasi hiyo na kama alikuwa amekwisha hudumu kwa awamu iliyopita atueleze amefanya nini serikalini hii itaweza kuleta mabadiliko chanya na uwajibikaji.

Kama wananchi watapata nafasi ya kuwachagua viongozi wengi wa serikali nchi hii itapata mabadiliko chanya ambapo viongozi watatekeleza majukumu yao wakiwa huru na sio kuwanyenyea wale walio wateua ili kuzilinda nafasi zao. Na hii ina mifano hai kwani tunaona jinsi wabunge wanavyowasikiliza wananchi kero zao na kuzifikisha bungeni pia tumeona hawa viongozi wa kuteuliwa wanavyowaona wananchi wa kawaida kama takataka.

Wananchi wa Tanzania wamekuwa waathirika/ wahanga wa viongozi hawa wa kuteuliwa kwani wamenyanyaswa, wamedharauliwa na wakati mwingine wamepoteza haki zao mikononi mwa viongozi hawa, tumeshuhudia kile kichofanywa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, pia hata aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya haya yote ni matokeo ya viongozi wa kuteuliwa kwani hufanya maamuzi ili kumlinda yule aliyewateua bila kujali ni jinsi gani wanawaumiza wananchi. Serikali ipitie upya katiba hii kuangalia ni viongozi gani wanatakiwa kuteuliwa na wapi wachaguliwe na wananchi. Kwa mfano mtu ni mbunge halafu anateuliwa tena kuwa waziri ina maana hapa anakuwa anafanya kazi katika mihimili miwili ya bunge na serikali, atawezaje kuwatumikia wananchi ilhali anaitumikia ile kofia ya teuzi kutoka kwa Rais, hii yote inapunguza uwajibikaji wa viongozi wa serikali. Wabunge wabakie kuwa wabunge tu na sio kuwateua tena kuwa mawaziri.

Rai yangu kwa serikali na wote wanaoshiriki katika tume ya katiba mpya, kama kuna mabadiliko wananchi wanayahitaji ni hii ya kuondoa viongozi wa kuteuliwa hii ndio utakuwa mwarobaini wa “TOKOMEZA VIONGOZI MACHAWA SERIKALINI”​
 
Upvote 2
Hali ikiendelea hivi nchi hii inaweza kuwa shirika la machawa lisilokuwa na viongozi wawajibikaji, rai yangu kwa serikali ili kuweza kuleta mabadiliko chanya napendekeza viongozi wote wanao wawakilisha wananchi/ wanaowatumikia wananchi wachaguliwe kwa kupigiwa kura na sio kuteuliwa na Rais kama ambavyo Ibara ya 67 ya katiba imeianisha sifa za mtu kuwa mbunge vivyo hivyo tupewe sifa za mtu kuwa mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa n.k ili nafasi hizi ziweze kugombewa viongozi hao wachaguliwe na wananchi na sio kuteuliwa
Tunaweza kuwa tunasisitiza njia za kumpata kiongozi fulani. Na pamoja na kuwa tunakubaliana kwamba katiba inaweza kuweka bayana mambo kama hayo. Ukifuatilia utagundua kuwa awe wa kuchaguliwa na Rais au kuchaguliwa na wananchi kitakachofanya tufanikiwe au la ni uwajibikaji na uwajibishwaji wa huyo kiongozi tu.

Nasema hivi maana lazima tuliangalie pia upande wa kumpa ugumu Rais wa kuongoza bila kuteua waandamizi wake upo ugumu sana

Lakini nakubali kwamba katiba ikibadilika kidooooogo sana, ikaondoa mianya ya mtu awaye yote kutowajibishwa baaaas tatizo litakuwa limekwisha maana toka juu mpaka chini watu ni kuwajibika tu. Hata kama ameteuliwa au amechaguliwa. We unaonaje mleta mada? Maoni tafadhali.
 
Kutowapa nafasi watu kwa kuangalia wanavyojua kusifia tutoe nafasi kulingana na utendaji na pia tuweze kuadhibu uzembe . Uchawa utakufa kawaida tu
 
Hiyo hoja ya kua na mgombea huru, imepiganiwa Sana miaka ya nyuma na Christopher mtikila (R I P), Na Kesi ilipigwa kisiasa .
 
Back
Top Bottom