kudamademede
Member
- Jan 1, 2020
- 62
- 241
Ukipita mtandaoni kwenye kurasa zinazoendeshwa na vyama vya upinzani katika kipindi hiki cha kampeni, utaona mambo makubwa mawili.
Jambo la kwanza utaona majigambo kwamba wanapendwa na kila mtu na kwamba Oktoba 28 watashinda!! Jambo pili utakaloliona ni matusi makubwa yakielekezwa kwa kila mtu atakayeonekana anaipenda CCM.
Hii inatuma message mbaya sana na ya hatari kwa kila anayeipenda Tanzania. Lakini basi mngetukana kila mtu mkawaacha watumishi wa Mungu. Kumtukana mtumishi wa Mungu kwasababu anaonekana anapenda na kuyasifia mambo aliyoyafanya Magufuli ni kitendo kibaya sana.
Huku kurasa zikiendelea kutukana, viongozi wa vyama vya upinzani wanaonekana mstari wa mbele kuweka maoni yao (comments) kubariki matusi hayo. Watanzania na wazalendo, hawa wanaotukanwa ndio wanaoliombea taifa letu, ndio wanaunda kamati ya amani, ndio watahudhuria uapisho wa rais wetu.
Hata kama mnajua hamtashinda, msitukane viongozi wetu wa dini na kulifanya taifa letu kuonekana halina Mungu. Nashauri hii tabia isitishwe mara moja na tunaomba viongozi wa dini kote nchini kutoyumbishwa kwasababu ya matusi na vitisho vinavyotolewa na wapinzani.
Kama kufurahia maendeleo ya nchi ndio mtutukane basi tutawaonesha kuwa fimbo ya kuwapigia tarehe 28 iko kwenye nyumba za ibada ambazo sisi ndio viongozi wake.
Askofu Jonathan Mwakatobe
TAG Temeke