Uchaguzi 2020 Tunatukanwa kwakuwa tumeona yaliyofanywa na Magufuli

Uchaguzi 2020 Tunatukanwa kwakuwa tumeona yaliyofanywa na Magufuli

Baba Askofu,

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Kristo.

Kwanza naomba radhi kwa matusi yaliyoelekezwa kwako na watu ambao naweza kusema wamepitiwa na ibilisi kwasababu matusi sio suluhisho na wala hayajawahi kuwa suluhisho.

Matusi hayapunguzi kura kwa mgombea wasiyemtaka wala hayaongezi kura kwa mgombea wanayemtaka.

Hivyo nakusihi baba Askofu uwasamehe tu.

Baada ya kusema hayo naomba uniruhusu nami nitoe maoni yangu kidogo kuhusu ninyi watumishi wa Mungu.

Kwa uelewa wangu ninyi watumishi mnaheshima kubwa sana katika jamii kwa maana ninyi ni wajumbe wa kristo kwa upande wa kikristo hivyo hivyo Mashekh ni wajumbe wa mtume kwa upande kiislamu.

Pamoja na heshima kubwa mliyonayo, hiyo haiondoi ukweli kwamba ninyi ni binadamu kama tulivyo binadamu wengine. Kwa maana kwamba mna hisia sawsawa na binadamu wengine. Kwangu mimi hainishangazi hata kidogo kwa watumishi kama nyie kuonyesha mapenzi yenu kwa mgombea fulani maana hapo mnadhihirisha ubinadamu wenu.

Hata hivyo kwa kuzingatia nafasi zenu katika jamii, na kwakuwa ninyi ni wajumbe wa Kristo/Mtume kwa waislamu mnapaswa kuenenda na kutenda kama Kristo/Mtume kwa waislam.

Katika makanisa na misikiti mnayoiongoza mna waumini wenye itikadi mbalimbali za kisiasa. Kwa kutambua hilo ni vema mgejiepusha na kujifungamanisha na upande wa mgombea fulani ili kuepuka kuwakwaza waumini wenu wasio na itikadi ya upande huo.

Najua katika hali ya ubindamu ni vigumu kuzuia kuionyesha itikadi yako na mapenzi yako kwa chama au mgombea fulani. Lakini inawapasa mjitahidi sana kujizuia kwani ninyi hamna tofauti na Mahakimu/Majaji na hata viongozi wa tume ya uchaguzi ili muweze kutenda haki kwa watanzania wote basi hampaswi kuonyesha mnafungamana na upande fulani.

Katika maelezo yako umesema watu wanawatukana kwa vile tu nyie mmeonyesha kukubaliana au kusifia kazi nzuri iliyofanywa na utawala wa sasa na umehitimisha kwa kusema sasa mtahamasisha waumini wenu ili wawakatae wagombea wengine tar/28. Samahani kama nimekunukuu vibaya.

Kama nimekunukuu sawasawa basi naomba baba Askofu niseme hao wanawatukana kwa sababu tu ya kusifia kazi nzuri zilizofanywa na utawala huu kwa kweli wanakosea muwasamehe.

Rai yangu kwako baba Askofu wakati mnasifia kazi nzuri za maendeleo msisite pia kukemea mambo mabaya yanayotokea nchini mwetu chini ya utawala huu.

Mkifanya hivyo mtakuwa mmesimama kwenye kweli na mmemuwakilisha vema Kristo Yesu/Mtume Mohamad.

Mwisho waache waumini wachague kiongozi wanayemtaka kwa utashi wao bila kuwashurutisha.

Amen
 
Tuna viongozi wa kiimani lakini pia tuna matapeli wanaotumia imani ya dini.

Kiongozi wa kweli wa dini ni yule ambaye kwanza kabisa anachukia uovu kama ule wa kuteka watu, kuua, kutesa na kupoteza binadamu, na maovu mengine yanayofanana na hayo.

Huwezi ukaua halafu dhambi ya kuua ikapotea kwa sababu umejenga daraja au barabara.
 
Askofu Bwana asifiwe,nimesikitika sana na mada yako hii,Ina maana katika hii miaka mitano ya utawala huu unakubaliana na matendo mabaya yaliyofanyika,unataka kutuaminisha kuwa matendo ya ukatili yaliyofanywa ilikuwa sawa,Lissu alipopigwa risasi ilikuwa sawa,Aliphonce mawazo aliuwawa kikatili,hakuna kesi.watu wamepotea kwenu ni sawa.kwa hiyo flyover Ndo muhimu kuliko damu za watu zilizopetea.OK ila biblia inasema nyakati za mwisho uovu utaongezeka.
Na pia watatokea nanabii wa uwongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Huyu tayari keshaonyesha kuwa viatu vya uchungaji ni vikubwa sana kwake. Aende Lumumba pale akanunue Shati ya CCM na kofia aanze kupiga siasa
 
Taifa hili halina dini,ni taifa la Wakristo,Waislamu,Wahindu,Wabudha,Waabudu mizimu,wapagani,wasio na dini n.k. Ni upuuzi kusema tusilifanye taifa hili halina Mungu.
 
Back
Top Bottom