Uchaguzi 2020 Tunautakia heri Mkutano Mkuu wa CHADEMA, nyie ndio tumaini la wanyonge halisi

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Mkutano wenu unaoanza leo umebeba matumaini kwa Watanzania wanyonge sio wanyonge wa CCM kina MO.

Umebeba matumaini kwa wafanyakazi wa umma ambao hawajaongezewa mishahara kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Umebeba matumaini kwa wakulima na wafugaji ambao wamekuwa wakikopwa mazao yao na serikali ya CCM.

Mkutano unaoanza leo umebeba matumaini kwa wanafunzi wanaonyimwa mikopo na kupunguziwa mikopo yao na bodi ya mikopo licha ya kuwepo kwa mkataba.

Ni Mkutano unaowapa matumaini wafanyabiashara wanaoongezewa na kubambikiziwa kodi kubwa na TRA.

Ni Mkutano wa matumaini kwa wajasiliamali wakiwepo wamachinga na mama ntilie wanaosumbuliwa na migambo wa jiji.

Umebeba matumaini kwa wananchi wanaonyanyaswa na polisi kwa kubambikiziwa kesi na kunyimwa dhamana za wazi.

Ni Mkutano uliobeba matumaini kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari vilivyonyimwa uhuru wa kuandika maoni huru.

Kifupi ni Mkutano wa matumaini kwa Watanzania wote.

Kila la heri Mkutano wa CHADEMA, ni mategemeo yetu kuwa mtatuletea chaguo la wananchi wanyonge.

IMG_20200802_084335.jpg
 
Eti mnataka kutuletea mtu ambae waTZ wengi washa mclassify Kama Gaidi?
 
Quinine,

Tunamuunga Mh. Lissu, yeye tu ndiyo tumaini LA wengi. Nadhani CDM hawawezi kufanya makosa ya kuwanyima Watanzania chaguo sahihi.

Pia,wapinzani wa kweli wataunganisha nguvu zao na kushirikiana ili kuwaondoa wakoloni weusi.

Kura zetu ziamue, tuchague viongozi na siyo watawala.
 
Wajumbe tupo makini sana. Hatutawaangusha. Tutawaletea mgombea bora kabisa, ni chuma cha uhakika.
 
Wajumbe wa mikutano yote mitatu, Kamati Kuu ya Chadema imekwisha toa dira ya kitu gani cha kufanya mkutanoni wakati wa kupiga kura.

Mkahakikishe Nyalandu anapita kwa kura nyingi. Hakuna maelezo mengine mapya. Kwenye ballot ni Mkulu na Nyalandu. Au mlitaka muambiwe kwa sauti wakati maelekezo ndio hayo. NYALANDU 2020.
 
Mkutano wenu unaoanza leo umebeba matumaini kwa Watanzania wanyonge sio wanyonge wa CCM kina MO.

Umebeba matumaini kwa wafanyakazi wa umma ambao hawajaongezewa mishahara kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Umebeba matumaini kwa wakulima na wafugaji ambao wamekuwa wakikopwa mazao yao na serikali ya CCM.

Mkutano unaoanza leo umebeba matumaini kwa wanafunzi wanaonyimwa mikopo na kupunguziwa mikopo yao na bodi ya mikopo licha ya kuwepo kwa mkataba.

Ni Mkutano unaowapa matumaini wafanyabiashara wanaoongezewa na kubambikiziwa kodi kubwa na TRA.

Ni Mkutano wa matumaini kwa wajasiliamali wakiwepo wamachinga na mama ntilie wanaosumbuliwa na migambo wa jiji.

Umebeba matumaini kwa wananchi wanaonyanyaswa na polisi kwa kubambikiziwa kesi na kunyimwa dhamana za wazi.

Ni Mkutano uliobeba matumaini kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari vilivyonyimwa uhuru wa kuandika maoni huru.

Kifupi ni Mkutano wa matumaini kwa Watanzania wote.

Kila la heri Mkutano wa CHADEMA, ni mategemeo yetu kuwa mtatuletea chaguo la wananchi wanyonge.
Nataman nione picha za wajumbe
 
Kiini macho, mpeperusha bendera anajulikana.. Nyalandu. Lisu ajiandae kisaikolojia kumwunga Nyalandu, mtu mnene, mwenye pesa, mwenye wafadhili, anyekubalika kwa Mbowe.
 
Back
Top Bottom