Kwanini sasa wakati tunazalisha wakutosha?
Shida kubwa umeme .....sio kama nyanya....kujenga miundo mbinu hadi unapotaka kuuza zaidi miaka 5.....je gharama zako na bei ina ushindani? Ethiopia wako Kenya long time umeme uko km 200 kutoka mpalani mwetu...easy kuleta na bei yao iko chini zaidi.....soma hapa
Ni kweli nchi ina umeme wa kutosha lakini haina maana kwasababu umeme upo wa kutosha basi unaweza kuupeleka popote pasipo kufanya tathmini!
Iko hivi umeme kutoka vyanzo vikuu vya umeme wa uhakika Rufiji na mikoa mingine ukitaka kuusafirisha kwenda mikoa ya kaskazini unakuwa unazungumzia mradi wa wastani wa 800km ~900Km
Gharama za kusafirisha umeme kwa umbali huo ni kubwa mno ukilinganisha na kuuchukulia hapo kenya .
Wanaposema umeme wa Ethiopia haina maana uko huko Ethiopia! Ni uko hapo jilani kenya wastani wa km 250km~300km tu
Hivyo ukichukulia gharama za kuusafirisha umeme kwa wastani 50mil kwa kila span moja ( nguzo moja hadi nyingine) hapa tutazungumzia wastani wa span elf 8000 hadi 9000 endapo utaamua kuutoa mikoa ya rufiji!
Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini
Mbali na gharama hizo mradi mkubwa kama huo unahitaji kulipa watu fidia na kuchepusha miundombinu itayoingiliana hapo katikati ya mradi!
Miradi ya mabomba ya mafuta yaliyopita ardhini yatalazimisha kubadilisha span badala ya kupitisha umeme juu ya bomba ushushwe chini (underground) ili kuepusha muingiliano wa frequency za umeme na zile za bomba la mafuta! Yote hayo yanapaisha gharama za mradi!
Muda wa kuujenga mradi mkubwa kama huo unaweza kuchukua miaka siyo chini ya mitano!
Upotevu wa umeme hapo katikati (power losses) kwa umbali huo ni Mkubwa ukilinganisha na faida utayovuna ukiuufikisha mikoa husika ya kaskazini!
Yote tisa hata kama umeme upo lakini kama jilani ana bei rahisi kuliko za nchi yetu kwanini kujichosha ilihali kwa jilani anao umeme karibu na ni bei nafuu zaidi?
Ambao hawajaelewa naomba kutoa mfano huu!