INAUZWA Tunauza, kufunga na kufanya marekebisho ya visimbuzi aina zote, pamoja na CCTV Camera na Uzio wa Umeme

INAUZWA Tunauza, kufunga na kufanya marekebisho ya visimbuzi aina zote, pamoja na CCTV Camera na Uzio wa Umeme

Ukiachilia local channels ambazo zipo nje ya uwezo wa kampuni ingawaje kampuni Kama kampuni haijakata tamaa bado inaendelea kuzipambania ili zirejee ni ki/vipindi gani ambavyo unahisi vinakosekana mpaka kushindwa kukonga nyoyo zenu!!??
Mkuu dstv ata mm nilikuwa natumia na nina kisimbuzi na dish lake bt kwa sasa dilishi la dstv nimeunganisha na kisimbuzi cha azam dstv nimewahama kwa reasons zifuatazo
1.vifurushi vyenu kiuhalisia ni ghali sana, kifurushi cha chini kabisa ni 19,000/=sina hakika kama imeshuka kdg bt kiuhalisia mpo juu sana. Azam ni 8000/= na local chanel zipo incase huna kifurushi.

2.hamuna local channels, so kama mteja hana hela ya kuunga kifurushi mara tu kiishapo, tv inabaki kama kabati tu sebuleni au aangalie chanel ya matangazo yenu. Azm zipo zaidi ya local chanel kumi incase ata kama huna hela ya kuunga kifurushi bado sebule inapendeza.

3.mvua ikinyesha kidg au kukiwa na wingu kdg tu dstv chaliiiiiii mpk hali ikitulia.

Ubora wenu ni mmoja tu, quality contents compare to other visimbuz.
 
Kwa Tsh 77,000 tu!!
Unapata: Dish, Decoder HD, Cable, ( vifaa vyote ), kifurushi Cha family cha Tsh 29,900 na unapata fundi wa kukufungia bila kulipa gharama ya ziada!!
Ili kupata offer hii piga 0789476655 WhatsApp +255784378129
Offer hii ni kwa Dar pekee!!
Mengineyo yote kuhusu DStv Kama:-
•Kulipia
•Vifurushi
•Mafundi
•Kununua

View attachment 1906653
Sawa,kwahiyo mimi huku kijijini hiyo hainihusu,poa tu endeleeni kupendeleana,ila mjue mtakuja tu huku na nyinyi siku moja...
 
Mkuu usitumie nguvu kubwa sana kuitetea dstv kwa sasa, in fact imepoteza sana mvuto tangu watoe local chanel + gharama za vifurushi ni kubwa sana.

Ukilipia 19900/= chanel za maana unazopewa hata tatu hazifiki, wakati upande wa star times mfano, ukilipia 21k ndio kifurushi chao cha juu na unapewa chanel karibia zote na local channels juu.

Nimekua dstv tangu 2014 ila saiz nimekiweka tu ndani maana nimetafuta wateja hata kwa 30k lakini sijapata hadi leo
Mimi mwenyewe nimekiweka pending tangu 2018, nimehamia azam kule maisha yako poa yaki sultan sultani na ki kulfi kulfi, ata kifurushi kikiisha still bado naweza nikaona chanel za local zaidi ya kumi mda wote, mpk nitakapoamua kuunga za kulipia.
 
Swala la kukata hapa tunaweza kukaa sana..
1.Inawezekana system ikafail channels zikakata ( sikatai Ila huwa Ni badra sana n ndo maana hata tukiomba kusikiliza malalamiko ya wateja wa DStv Kati ya wateja kumi inawezekana ukawa wewe tu kuhusu hiyo issue ya kukata channels kabla mwezi kuisha ) Ila unaweza ukazirejesha hata wewe mwenyewe bila hata kutupigia simu kwa kubofya *150*53#
2.Zinaweza zikakata kwasababu maalum pengine unatumia kwa matumizi ya biashara haliyakuwa a/c yako ni ya nyumbani!
3.Wakati mwengine signal kuwa weak Ni sababu pia
4.Kwa channels tukianzia quality ya picha hakuna kisimbuzi chenye quality Kama DStv na kuhusu urudiwaji wa movie inategemea na kifurushi na tunazingatia wapo ambao wanakosa kuona muda ambao inaonyeshwa kwa Mara ya kwanza ndio maana tuna channels zaidi ya 5 za movie..
Bado DStv inaendelea kuwa Bora ingawaje hatuwezi kumfurahisha kila mmoja ijapokuwa tunachukua Naomi katika kuboresha huduma zetu!
unajibu kwa weledi, vizuri

ila naunga hoja za wadau hapo juu, kutokuwa na local channels, vifurushi kupanda, channels useful chache mno, movies kutwa kucha kurudia izo izo tuuu

kiukweli dish lenu limeliweka benchi , nafikiria kujiunga na Azam
 
Duh basi nimeairisha. Nilitaka niuze azam ninunue dstv niwe naangalia EPL. Kumbe hata 20k hupati kifurushi cha kuangalia EPL?!
 
Kipindi cha Olympics wameniondolea baadhi ya stesheni kwenye kifurushi changu cha family Hadi Olympics zilivyokwisha ndo wakanirudishia! DSTV ni wa anabu Sana, kwa Sasa najiandaa kuhamia Azam au hata STAR TIMES ilibidi.
 
decoder pekee mnauza bei gani? yangu inaishia kuwaka njano haiendelei mbele.
 
Ukiachilia local channels ambazo zipo nje ya uwezo wa kampuni ingawaje kampuni Kama kampuni haijakata tamaa bado inaendelea kuzipambania ili zirejee ni ki/vipindi gani ambavyo unahisi vinakosekana mpaka kushindwa kukonga nyoyo zenu!!??
Ghalama zao kubwa sana
 
Binafsi najua vizuri uzuri na weakness za VISIMBUZI vyote Tanzania..!!
Labda ningesikia kilichokuhamisha DStv pengine tungeelimishana kitu hapa!
Mm usema ukweli hawa jamaa sio wasikivu kabisa.mfano mm napenda movie kifurushi changu cha 21000 movie zake za kizamani sana nimeshawaambia wala hawajali.hata kama wanaona hatuna pesa angalau kwa siku wawe wanatuwekea hata 1 Kali za kisasa.hzo laki 1 na kitu kwa mwezi tutazitoa wapi.nataka kuamia azam tuu
 
Na Azam akipata tu nafasi ya kuonyesha EPL basi DSTV watapumulia mashine zaidi..
 
Back
Top Bottom