Plot4Rent Tunauza Mashamba na Viwanja

Hivi mbona Wahindi hawaangaikagi na mambo ya viwanja/kujenga nyumba za kuishi ila wanamiliki biashara za maana (za thamani ya Mabiloni)? Tunakwama wapi?
Kwani wewe kujenga na ukamiliki biashara za thamani ya mabilioni kuna shida gani, ama lazima ukopi kwa Wahindi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila price kwangu ni kikwazo tu ila kweli tinatofautiana kifikili na kuona

mpuuzi mpuuzi tu
 
Mkuu Kwadilo,heshima yako kwanza.Bei 17.5 m au typing error?Ni sqm 610 tu?Kuna facilities zingine ndani ya uwanja au sifa ni title deed ipo on process/hunayo mkononi?Ina maana kiwanja mpaka sasa bado hukimiliki kisheria kwa sababu huenda/aidha Mipango Miji wakawa na matumizi ya eneo hilo,kuuzwa kwa zaidi ya mtu mmoja au kilinunuliwa lakini malipo hayajakamilishwa umeamua ku-resell tena.

Kuna kupigwa hapo wadau mkae chonjo/makini hata kama kwenye ramani kinaonekana kiwanja.

Ndio maana mimi huwa siku zote Anko Magu(Rais wa JMT) yupo sahihi kufunga mianya ya hela hovyo iliyosababisha viwanja kupanda bei.Pia kuhamisha shughuli za Ki-Serikali kuwa makao makuu Dodoma itafanya tupumue kwa bei zisizoendana na uhalisia kama hii,sqm 610 kwa 17.5 m?Ilikuwa enzi zile sasa hivi ni masikhara sheheee!!

Nunueni Viwanja Dodoma Jiji kwa ujenzi wa makazi na majengo ya biashara kwani baada ya miaka 6 ijayo Dodoma itakuwa inakimbiza kinoma.

Hahahahaha!!
 
Mtaviuza sana awamu hii na wanunuzi ndio hivyo tena.Watu wanakimbilia kununua Dodoma ndio maana ununuzi wa viwanja huko haupati Viwanja.Punguza bei Mtumishi wa Mungu naweza kukutafutia mteja fasta anahitaji kiwanja maeneo hayo huko.

Bei kubwa sana.Hakuna ujanja sasa hivi wa pesa kugaa zagaa ovyo kama enzi zetu zile.

Sala sala na Bunyokwa ni wewe tu unaviuza?We ni dalali au mmiliki?

Kama wewe ni dalali unaongeza bei mno ili upate cha juu.

Subiria wasio makini watakuja kununua.
 
Sawa kiongozi.Ila msiwe mnapandisha sana bei kwani nyie madalali hamshindwi kitu kwa kuvizia10%.Jiulize,watu/madalali msio na haya mnavamia na kuuza maeneo ya jeshi kwa utapeli(hujawahi kusikia raia wamevamia eneo la jeshi?) sembuse wewe dalali uliye nyuma ya keyboard na lugha nzuri/mororo kama demu wa Ki-ngazija ushindwe kweli kumshughulikia mnunuzi kiutapeli?

Sina hamu na nyie wadudu mnaojiita madalali,ovyo kabisa nyie.

Ni kiwanja kipi umepata mteja?Cha Bunyokwa au Salasala?

Njoo inbox tuyajenge ili nikuletee mteja aje achukue/anunue kiwanja uache kumbwela mbwela humu jamvini.

Mkuu,tupo pamoja au?
 

Mkuu kwema?
Plot bado ipo?
 
Hivi mbona Wahindi hawaangaikagi na mambo ya viwanja/kujenga nyumba za kuishi ila wanamiliki biashara za maana (za thamani ya Mabiloni)? Tunakwama wapi?
Kwasababu sio kwao hapa ndio maana wengi wanaogopa kufanya hivyo
 
Shamba linapatikana CHANIKA, nzasa.
Takribani km 4 kutoka CHANIKA mwisho.
Shamba lina jumla ya hekari 3
Eneo lote ni tambarare.
Lina documents za kutoka serikali ya mtaa.
Bei kwa kila hekari ni tsh 6m
Mawasiliano: 0756 832833




 
Kama unachukua milioni 15, nicheki PM tuje tufanye biashara
 
Viwanja viko vinne, vimegawanywa kwa ukubwa wa meter 20*20=sqm 400
Eneo ni tambarare na lina asili ya kichanga.
Umbali kutoka ferry/kivukoni ni km 20 (mwendo wa gari)
Eneo linaitwa mbutu mbele ya mwongozo.
Gari za moja kwa moja zinapatikana Kigamboni ferry (k/mboni via mbutu)
Bei ya kiwanja kimoja ni 3m tu.





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…