Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Tate Mkuu, yaani wajumbe...!. Wee acha tuu!.😁😁😁 Ngoja nimuulize huyu mentor wangu Pascal Mayalla anipe mbinu za kuwazidi maarifa hao WAJUMBE!! Maana nasikia ni noma kweli kweli!
Wanakupa matumaini na kukujaza upepo kweli kweli, halafu wakati wa kutangazwa matokeo unaambiwa umepata kura moja tu!!! 🙄
Jimbo la Kawe lina kata 10.
1. Unapaswa kujitambulisha kwa wajumbe kila kata. Kwenye utambulisho huo unagharimia 'maji ya kunywa', na baada ya utambulisho unawarejeshea wajumbe nauli wanaotumia kuja, nauli ya kurejea na nauli ya kuja kwenye kikao.
2. Wakati ukisubiri kura zao, unatumiwa sms, mwenzako kapita na kutoa nauli kubwa, hivyo kama hutaongeza kiwango cha nauli unaweza ukakosa kura. Hivyo unanyoosha mkono.
3. Tangu hapo ni kila siku kuna mjumbe kafiwa, anauguliwa, ana majanga, ada, kodi, mtaji, etc.
5. Siku ya kura, pale ukumbini kila mjumbe anakuhakikishia ni wewe tuu!, kura zote kwako, ila ongeza japo chochote kitu, maana wenzako wanamwaga mihela!.
Na baada ya matokeo, unapata kura moko!. Kila mjumbe ulio 'muona', anakujia na kukupa pole na kukuambia ile kura moja ni kura yake!.
Wajumbe..., waache tuu, Mungu anawaona!.
P