Tunauza vifaranga vya kuku wa Mayai (Layers)

KUKU_UFUGAJI

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2016
Posts
857
Reaction score
1,727
Habari wana jamvi, natumai mko salama kabisa. Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.

Vifaranga wanahitaji uangalizi mkubwa sana hasa katika hatua za mwanzo za ukuaji wao, na moja ya njia zinazoweza kuhakikisha usalama wa maisha yao kwanza wao kwa wao (yaani vifaranga) na usalama wa mayai hapo baadaye ni kwa kuwakata midomo.

Zoezi hili hufanyika pia kwa lengo la kusaidia kuzuia upotevu wa chakula kutokana namna vifaranga wanavyodonoa donoa chakula wakati wa kula. Mara nyingi huwa wanakitawanya chakula vibaya kutokana na urefu wa midomo yao. Hivyo wanapofikisha umri wa siku 7-10 zoezi hili la kuwapunguza midomo hufanyika kisha kurudiwa tena wanapokuwa na umri wa kati ya wiki 8 hadi 10.

Vifaa maalum hutumika kukamilisha zoezi hili, na kwa anayefuga kitaalam ni vema zoezi hili likafanywa na mtaalam kwa kuwa linahitaji umakini wa hali ya juu ili vifaranga wasidhurike macho wala ulimi.

Mtaalam atachunguza kwanza makali na joto la wembe wa kifaa cha kukatia midomo kabla ya kuanza zoezi. Kisha ataanza kukata mdomo mmoja baada ya mwingine yaani wa juu kisha wa chini ama vinginevyo.

Jukumu kwa mfugaji ni kuhakikisha kuwa joto la mazingira sio kali sana, vifaranga wana afya njema na wamepatiwa vitamini kabla ya kuanza zoezi la ukataji midomo na mara baada ya zoezi kukamilika hakikisha kuku wanapatiwa chakula cha kutosha na maji yenye vitamin wakati wote kwa muda wa wiki nzima.

Bovans Brown ni kuku bora kabisa wa mayai na wanaotaga kwa miezi 12 kabla ya kuacha ama kupunguza utagaji.

Karibu sana ujipatie kuku layers bora kabisa wa mayai. Vifaranga Vya Kuku Wa Mayai (Layers) Bovan Brown/Kuku Wa Mayai.

Kifaranga wa siku 1.

SIFA ZA HAWA KUKU (BOVANS BROWN)
✓Wanakuwa vizuri sana
✓Wanataga wakishafika miezi 5 toka akiwa kifaranga.
✓Wanastahimili magonjwa.
✓Utagaji wao asilimia 95
✓Wanataga mayai 250-300 kwa mwaka.
✓Wanakaa miaka 2 ukiwatunza vizuri.

BEI YAKE NI 1,500TZS TU UNAPATA KITU KILICHO BORA.

Call/WhatsApp: +255 679 003 511.

Mkuu video zako hazifunguki....

Hao kuku kwa nyama ni watamu au ndio wale makapi wakishamaliza kutaga hawana ladha.
Pia asili yao ni wapi? Wamechanganywa na nini?
 
View attachment 3029774
View attachment 3029775
Mkuu tunahitaji vifaranga kama 5000 ila tunachukua vya wiki nne ni shilling ngapi vya huo mda.
 
Hatuweki vya mwezi Mkuu. Ni, vifaranga vya siku moja mpaka siku 2 tuu.
Karibu sana
Mkuu tunahitaji vifaranga kama 5000 ila tunachukua vya wiki nne ni shilling ngapi vya huo mda.
 
Layers wanataga mno na wanarudisha gharama za matunzo na faida ya mayai na nyama ,nilisha wahi kufanya huu mradi unalipa mno.
 
Hapana, hakuna kitu kama hicho Mkuu.

Unatoa hela una pokea mzigo wako hapo hapo.

Bei ya Saba saba hii mkuu, karibu uchangamkie fursa.

Kwenye boksi wanakaa 100 ,haku a upigaji na tayari tumesha uzia wengine pia, siyo wageni kwenye hii kazi pia Mkuu.

Karibu sana urudishe mrejesho hapa hapa jukwaani.
Layers 1500 kuna harufu ya upigaji hapa
 
Layers wanataga mno na wanarudisha gharama za matunzo na faida ya mayai na nyama ,nilisha wahi kufanya huu mradi unalipa mno.
Wewe mtu wa nne leo nimekutana nae anaongelea habari za layers.Au ndio sauti ya Mungu?! Nashawishika.
 
Mbezi mwisho wapi ? Toa details mkuu hiyo biashara au farm haina jina? Haina ujirani au barabara mkuu au wewe ni dalali au sio mwenye biashara?
Nimeweka namba hapo Mkuu. Unaweza kutupigia.

Tupo mbezi mwisho karibu na Magufuli stand, ndipo ofisi ilipo.
 
Wewe mtu wa nne leo nimekutana nae anaongelea habari za layers.Au ndio sauti ya Mungu?! Nashawishika.
Fanya majaribio kwanza huanze na kuku 100 biashara ya kuku wa mayai, inategemea mkono wa mtu na bahati sio kingine.
 
Karibu sanaa Mkuu.
Ni biashara nzuri ndiyo maana ina ongelewa hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Hakuna bahati Mkuu, fanya tafiti ya namna ya ufugaji, na soko, pia anza kidogo kidogo, ukue pole pole, kupitia kufanya hivyo experience yako itakuwa kidogo kidogo ndani ya awamu mbili au tatu basi utakuwa vizuri kwenye ufugaji.
Fanya majaribio kwanza huanze na kuku 100 biashara ya kuku wa mayai, inategemea mkono wa mtu na bahati sio kingine.
 
Wewe mtu wa nne leo nimekutana nae anaongelea habari za layers.Au ndio sauti ya Mungu?! Nashawishika.
Mkuu hii ni biashara nzuri sana ukiwa mvumilivu , pesa yako inarudi haraka na faida juu, ndani ya miezi 6 wakianza kutaga muhimu apo ni chakula bora na madawa kulingna na vipindi vyao vya ukuaji.
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Nimeweka namba hapo Mkuu. Unaweza kutupigia.

Tupo mbezi mwisho karibu na Magufuli stand, ndipo ofisi ilipo.
Taja jina la ofisi weka vitu hadharani mambo ya kuweka number ya simu ni udalali mkuu watu watakulia mashaka.
 
Mkuu hii ni biashara nzuri sana ukiwa mvumilivu , pesa yako inarudi haraka na faida juu, ndani ya miezi 6 wakianza kutaga muhimu apo ni chakula bora na madawa kulingna na vipindi vyao vya ukuaji.
Vipi kwa kuanza na vifaranga 500 niandae shilingi ngapi kwa makadirio ,pamoja na gharama za msosi na dawa?
 
Back
Top Bottom