Habari wana jamvi, natumai mko salama kabisa. Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.
Vifaranga wanahitaji uangalizi mkubwa sana hasa katika hatua za mwanzo za ukuaji wao, na moja ya njia zinazoweza kuhakikisha usalama wa maisha yao kwanza wao kwa wao (yaani vifaranga) na usalama wa mayai hapo baadaye ni kwa kuwakata midomo.
Zoezi hili hufanyika pia kwa lengo la kusaidia kuzuia upotevu wa chakula kutokana namna vifaranga wanavyodonoa donoa chakula wakati wa kula. Mara nyingi huwa wanakitawanya chakula vibaya kutokana na urefu wa midomo yao. Hivyo wanapofikisha umri wa siku 7-10 zoezi hili la kuwapunguza midomo hufanyika kisha kurudiwa tena wanapokuwa na umri wa kati ya wiki 8 hadi 10.
Vifaa maalum hutumika kukamilisha zoezi hili, na kwa anayefuga kitaalam ni vema zoezi hili likafanywa na mtaalam kwa kuwa linahitaji umakini wa hali ya juu ili vifaranga wasidhurike macho wala ulimi.
Mtaalam atachunguza kwanza makali na joto la wembe wa kifaa cha kukatia midomo kabla ya kuanza zoezi. Kisha ataanza kukata mdomo mmoja baada ya mwingine yaani wa juu kisha wa chini ama vinginevyo.
Jukumu kwa mfugaji ni kuhakikisha kuwa joto la mazingira sio kali sana, vifaranga wana afya njema na wamepatiwa vitamini kabla ya kuanza zoezi la ukataji midomo na mara baada ya zoezi kukamilika hakikisha kuku wanapatiwa chakula cha kutosha na maji yenye vitamin wakati wote kwa muda wa wiki nzima.
Bovans Brown ni kuku bora kabisa wa mayai na wanaotaga kwa miezi 12 kabla ya kuacha ama kupunguza utagaji.
Karibu sana ujipatie kuku layers bora kabisa wa mayai. Vifaranga Vya Kuku Wa Mayai (Layers) Bovan Brown/Kuku Wa Mayai.
Kifaranga wa siku 1.
SIFA ZA HAWA KUKU (BOVANS BROWN)
✓Wanakuwa vizuri sana
✓Wanataga wakishafika miezi 5 toka akiwa kifaranga.
✓Wanastahimili magonjwa.
✓Utagaji wao asilimia 95
✓Wanataga mayai 250-300 kwa mwaka.
✓Wanakaa miaka 2 ukiwatunza vizuri.
BEI YAKE NI 1,500TZS TU UNAPATA KITU KILICHO BORA.
Call/WhatsApp: +255 679 003 511.
View attachment 3029774
View attachment 3029775