Tunawajibu wa kuboresha elimu yetu

Tunawajibu wa kuboresha elimu yetu

K2S7J3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
449
Reaction score
332
Wakati nikiwa katika shughuli zangu za kawaida nikaona ni vema tujadili mambo haya:

1. Shule za kata zilianzishwa kuimarisha elimu nchini lakin zimegeuka na kudidimiza elimu zaidi, kama serikali imeshindwa kuziboresha ni vema zifungwe?

2. Kufuatia maazimio ya EFA (Education for all) ya mwaka 1992, watu wote wanatakiwa kupata elimu sawa. Je, hii itawezekanaje kwa wale ambao wana uwezo mdogo darasani ambao PLATO aliwaita "Iron boys"

3. Kwa vile imeonekana kuwa shule zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalum kuondoa O'levels mnamo mwaka 2008, elimu ya ngazi hiyo ya elimu inazid kudolola mwaka hadi mwaka. Je, inabidi turudishe O'levels katika shule hizi?

Nimeona tujadili mambo haya kwa mustakabali wa taifa letu kwa kuzingatia kwamba waboreshaji wakuu wa elimu yetu ni sisi wemyewe na sio kuitegemea serikali tutabakia kulalamika. Tafakari, chukua hatua.

Naomba kuwasilisha mada ndugu zangu wana JF
 
Acha mawazo finyu,zifungwe?halafu wadogo zetu wasome wapi?wana hayo mamilion ya kulipia st.mary's?issue is to modernize them NOTHING ELSE
 
kwani hzo shule za kata hazifungwi.?si huwa znafungwa kila mwezi wa 3.6.9,na 12.?
au wew3e ulikuwa unamaanisha zifutiwe usajili.?kama ni hvo utakuwa umeteleza mkuu,halafu hao watu wanaosoma huko waende wapi?
 
Wakati nikiwa katika shughuli zangu za kawaida nikaona ni vema tujadili mambo haya:

1. Shule za kata zilianzishwa kuimarisha elimu nchini lakin zimegeuka na kudidimiza elimu zaidi, kama serikali imeshindwa kuziboresha ni vema zifungwe?

2. Kufuatia maazimio ya EFA (Education for all) ya mwaka 1992, watu wote wanatakiwa kupata elimu sawa. Je, hii itawezekanaje kwa wale ambao wana uwezo mdogo darasani ambao PLATO aliwaita "Iron boys"

3. Kwa vile imeonekana kuwa shule zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalum kuondoa O'levels mnamo mwaka 2008, elimu ya ngazi hiyo ya elimu inazid kudolola mwaka hadi mwaka. Je, inabidi turudishe O'levels katika shule hizi?

Nimeona tujadili mambo haya kwa mustakabali wa taifa letu kwa kuzingatia kwamba waboreshaji wakuu wa elimu yetu ni sisi wemyewe na sio kuitegemea serikali tutabakia kulalamika. Tafakari, chukua hatua.

Naomba kuwasilisha mada ndugu zangu wana JF

Kama kweli una maanisha unalo lisema basi ishauri kwanza serikali iboreshe maslahi ya walimu. Kuporomoka kwa ubora wa elimu tanzania ni matokea ya kauli ya Mwantumu Mahiza aliyo itoa chuo cha ualimu mtwara kuwa anaye ona mshara wa walimu ni mdogo atafute ajira nyingine. Na baadaye mkuu wa inchi aliposema kama walimu wanaona mshahara hautoshi waache kazi kauli hizi za viongozi zinawavunja moyo walimu. Enzi za mwalimu Nyerere na Waziri Makweta japo mishahara ilikua midogo walimu waliheshimiwa na serikali na walipewa maneno ya kuwapa ujasiri wa kupambana na mazingira magumu ndio maana Elimu ya Tanzania wakati huo ilikuwa ya kiwango cha kimataifa lakini sasa kauli chafu zilizo jaa kejeri zinazo tolewa na viongozi zimewafanya walimu wadharauliwe na jamii matokeo yake ni wanafunzi kumaliza Elimu ya msngi wakiwa hawajui kusoma na kuandika hata majina yao na bado wanafaulu na kujiunga na elimu ya sekondari. Raisi wetu, Mawaziri, na wabunge wanaliona hili ila haliwaumi sababu watoto wao wanasoma nje ya nchi wanao athirika ni watoto wa sisi wapigakura na walala hoi NCHI YANGU TANZANIA IAANGAMIA HUKU NIKIIONA KWA MACHO LAKINI NINASHINDWA KUISALIMISHA hiki ni sawa na kilio cha samaki machozi hayaonekani
 
Mmenena vijana......ila tukumbuke usipo ona umuhimu wa golikipa uwanjani basi subiri kufungwa na hichi ndicho kulicho tokea tz. Na kuieka kwenye genius book of record....kwa tukio la kufuta matokeo kisa wanafunz yapata lakitana asilimia 20 tuu ndo wamefaulu!
 
Unatakiwa ufikirie ni kwa nini nimeuliza zifungwe nikimanisha zifutwe kabisa halafu ndo utoe maoni yako sio kukurupuka ili uonekane umechallange, Ahsanteni
 
Back
Top Bottom