Tunawakaribisha wanasheria, wahasibu, wahandisi, watawala, wawekezaji...


watanzania "we are very poor in business"

yaani unachokifanya ni kama kuuza hisa but unatafuta wanunuzi wa hisa kwa njia ya kitapeli. naita njia ya kitapeli kwa maana matapeli ndio wanaoficha kile wanachokiuza na kutafuta kuwaingiza watu mkenge kwanza ndio mtu anakuja kujua kama kaliwa au kala.

lakini serious businessmen wanashawishi mitaji kwa kuweka wazi mipango ya kibiashara waliyo nayo. wanaokubaliana na wewe wanajiunga na wasiokubaliana na wewe wanakataa.

only an ignorant person ndiye anayeweza kuleta fedha kuingiza kwenye kitu kwa jina tu kutengeneza kampuni kubwa.

kama hutaki kuweka wazi basi anzisha watu waone pace ya kampuni uliyounda ndio uwashawishi walete mitaji muongeze soko na faida.

ile tu kugangania kusaini mikataba ya "non disclosure agreement" ni weakness kwa mtu ambaye anajua ujasiriamali maana wewe unaonyesha woga wa kibiashara na mtu kama huyo hawezi kutoka kibiashara maana biashara zinahitaji wateja washawishiwe kwa taarifa sasa kama fikra zenyewe ndio hizi za kuwaambia watu nunua kwanza ndio utajua faida za bidhaa au huduma zetu hakuna biashara hapo.
 

We are not only poor in business we are even poorer in the way of our thinking. You are the best example.

Katika tangazo la juu hapo sijaona mahala kakwambia uweke pesa zako, inaonesha how ignorant you are. Simply anasema kama uko interested nenda kasaini non disclosure agreements akueleze ni biashara ipi. Ukiridhika unawekeza, though sidhani kama wewe unaweza kuwekeza.

Unaongea afunguwe kampuni, unajuwa maana ya kampuni? Kampuni hufunguliwa na mtu mmoja? Au ulitaka afunguwe zile kampuni za mradi majina yawepo la babu, bibi, mjomba, mwana, na kumbe ni one man show?

Ni ujinga kufikiria kuwa non disclosure agreement ni weakness, zisingekuwepo.

Ni wewe tu utaanza ku dis kuwa huu ni utapeli, tapeli ana saini mikataba ya kisheria kabla hamjaanza hata mazungumzo?

Wenye uelewa wa haya mambo tumeshaingia na tumesha saini mikataba ya non disclosure na tumeridhika na idea, ni nzuri sana, tunasubiri watu watimie tutumbukize pesa zetu tuanze kazi.

Wewe kaa na ujuwaji wako, utaendelea sana.
 
Utapeli mtupu....siamin kama na wewe bibi yetu waweza kuwa tapeli ,eti niinvest 10m bila kujua ni project gani hiyo halafu unanilazimisha nisain kwanza kama mwekezaji..........
YESU tusaidie waja wako.
 


ego,

Natumai umzima wa afya.

Hatuuzi hisa, tunatafuta wabia wa biashara. Hilo neno "kitapeli" tafadhali liondoe mpaka utapokutana na sisi na au kuuliza tukupe majibu ya kina au uulize tuliokwisha fanya nao kazi, wapo wengi humu JF,hatujaanza leo kujitangaza humu. Na uzuri ni kuwa wengi walituona hapa JF na wakafika mpaka kwetu na kujiridhisha.

Kuhusu "kuleta fedha", labda hujatusoma vizuri, ngoja nikufahamishe kwa kituo...

Kwenye heading hapo juu tuesema tunahitaji wasomi wa fani mbali mbali. Hao wasommi tunawahitaji ili wawe wabia kwenye huu mradi mmkubwa ambao tutauanzisha. Mradi huu hatutauanzisha mpaka team itimie, na kwa ucha team yenyewe inahitaji hao wasomi tuliowata hapo juu.

Hatuhitaji mtu yeyote kuwekeza pesa zake kabla hiyo team haijatimia na shirika kuanzishwa. Na hao wasomi niliowataja awali ndio watakuwa "board members" wa kampuni na kila mmoja atakuwa na majukumu kutokana na fani yake.

Leo hii hata ukija na millioni 100 au zaidi hatutazipokea kwa kuwa team haijakamilika. Kuna mambo ya kisheria, ya kihasibu, ya kiengineer, na fani tofauti tofauti ambazo tunahitaji waliobobea wakamilike ndio to form company.

"Non disclosure agreement" ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya wazo hilo na nyaraka ama dokezo zozote zitakazokuwa zinajadiliwa na kutolewa wakati wa mazungumzo ya awali. Ni muhimu sana kwa kuwa wengi wataohusika na mradi huu hatujuani na ni lazima tutabadilishana kila aina ya mawazo na tuyaheshimu na kuyalinda na isiwe holela tu.

Hatutaweka wazi mpaka tumesaini mikataba ya kisheria ya "non disclosure agreement". Hilo hatutabadilisha.

Kama unaiona hiyo ni "weakness" basi hauna budi kutuwachia "weakness" yetu nawe yanini unapoteza muda na energy yako kwa watu ambao wapo "weak"?

Hakuna mahala tumesema "nunua kwanza halafu ndiyo utaijuwa faida", hayo unayafikiria tu kichwani mwako kwa kuwa mwenzetu upo na extremely higher strength kuliko sisi wenye weakness ambao hata hatujayafikiria hayo.

Tunakukaribisha kwetu ili ujionee miradi mingineyo tuliyokwisha ianzisha inayofanyika wakati huu, lakini huu hatutakuelezea unahusu nini na utafanyikaje mpaka usani "non disclosure agreement".

Asante.

Abdul
 
Utapeli mtupu....siamin kama na wewe bibi yetu waweza kuwa tapeli ,eti niinvest 10m bila kujua ni project gani hiyo halafu unanilazimisha nisain kwanza kama mwekezaji..........
YESU tusaidie waja wako.


Bibi yako yupi unaemzungumzia?

Hakuna mahala tumesema "invest kwanza 10m", tumesema kabla hatujakuelezea ni mradi upi basi itatulazimu tusaini sisi na wewe "non disclosure agreement" ili kulinda wazo letu na maslahi yetu na yako. Baada ya hapo tunakuelezea na hatutachukua pesa zako mpaka team ya watu tuliowataja kwenye post namba moja ikamilike na company iwe formed.

Si tuhuma nzuri hizo.

Tunakukaribisha uje kujionea kazi zetu kwa macho yako na ufanye utafiti japo kidogo ili ujiridhishe kabla hujatuchafua na huku hautujui.

Njoo ujionee na unaweza kuwa mgeni wetu kujiridhisha na shughuli zetu ili uje kutusafisha hiyo tuhuma nzito ya "utapeli" ulioturushia ambayo nafikiri uliitoa bila ya kufikiri.
 
Bado tunakaribishwa? naomba nikaribie Bi Zainab, muongazo tafaadhal.


Mnakaribishwa, bado kabisa team haijakamilika. Unaweza kutu pm kwa details au ukiona ni sawa hapa hapa basi hakuna neno.

Karibu sana.
 
Din zote au waislamu tu!!?


Karibu sana, hatutaki wala hatuna muda wa kusikia kuhusu masuala ya dini kwenye kazi zetu. Tunafanya kazi na watu wa dini zote na wale wasio na dini pia na wengi sana hatujui hata dini zao.

Nyote mwakaribishwa.

Sisi tunamkaribisha yeyote mwenye kuhisi anaweza kufanya kazi na sisi, tunamkunjulia moyo wetu na mikono yetu.

Tafadhali sana tuwe makini, Tanzania hii inajengwa na wote wenye dini na wasio na dini. Tunaishi, tunafanya kazi, tunakula, tunatembea hatuulizani dini zetu. Vipi tuanze kuulizana hapa?

Asante.

Abdul
 
Aisee hivi kumbe kweli JF watu wnajisajiri majina yakike kumbe vidume.... zainabu tamim.... halafu mleta uzi Abdul
 
Et anaficha aina ya Huduma, anauza mbuzi kwenye gunia,
Kwenye competitive market huu ni ushamba,
Anaogopa kuigwa!
 
Aisee hivi kumbe kweli JF watu wnajisajiri majina yakike kumbe vidume.... zainabu tamim.... halafu mleta uzi Abdul

Mzee Abdul mume wangu, kuna vitu anavyojibu yeye anaandika jina lake chini ili uelewe kuwa si mimi.
 
Et anaficha aina ya Huduma, anauza mbuzi kwenye gunia,
Kwenye competitive market huu ni ushamba,
Anaogopa kuigwa!

Kama ni ushamba tuwache na ushamba wetu, wewe unakuumiza nini ushamba wetu?

Asante.
 
Nikipata wasaa nitawatembelea kujua hiyo Idea na kama fani yangu itahitajika.
 
Nimeona wengi humu neno "non disclosure agreement" wamelitafsiri vibaya.

Ninapenda kuwajulisha kuwa hatakiwi mtu kulipa malipo yoyote kabla ya maridhiano na sisi, kama tulivyosema tutakuwa na mkataba wa kutunziana siri za mawazo/ kazi tunazotarajia kufanya na hiyo haina maana kuwa ukisaini mkataba huo ndiyo umeingia kwenye mkataba wa kuwekeza. Sivyo hivyo.

Mikataba ya"non disclosure"ipo ya aina nyingi sana.

Hii ni sample ya "non disclosure agreement" niliyoitoa kwenye mtandao, naomba uisome ili uelewe umuhimu wake:



Mkataba wetu unaweza kufanana na huo isipokuwa tutaurekebisha kutokana na yale yetu ambayo tusingependa yatumike nje ya makubaliano yetu.

Abdul
 
Wizi kama huu uliwahi fanyika Arusha

Mtatapeliwa nyie

Nasubiri mtu anibishie ni funguke zaidi
 

Mimi nadhani wewe hujiweki katika viatu vya wengine.

kuingiza gharama katika kitu sio in terms of cash peke yake bali ile mtu kutenga mda tu akaja kuwatafuta na kupewa hiyo mikataba na kusaini na then kupewa maelezo ya kile mnachotaka kufanya ndio nitazame kama kinanifaa au la hizo ni gharama.

Katika kitu chochote ambacho ni cha kibiashara ili mtu avutike kuingia katika jambo kwa kununua au kuwekeza kuna taarifa za awali ambazo muuzaji au mvutia mitaji anawajibika kuzitoa "free of charge" kupitia mitandao nakadhalika kwa watu.

labda nikuulize wewe binafsi umewahi kwenda sehemu ngapi ambazo mtu anatangaza tunauza bidhaa nzuri njoo mnunue hujui ni bidhaa gani eti ukafunga safari kwenda kutazama?

au ni wangapi humu wanaweza kuandika kama wewe kuwa tunataka kuanzisha kampuni kubwa au biashara nzuri ukavutika wewe uliyeandika uzi huu kwenda kusikiliza?

unachotaka kuhitaji taaluma tofauti sio tija ya wawekezaji fedha kuwa taaluma hizo na kama unataka anayeweka fedha ndiye anatafuta mda wa kufanya hizo shughuli zenu weka wazi pia.

ki msingi utata ni mwingi kuliko majibu.
 
Wizi kama huu uliwahi fanyika Arusha

Mtatapeliwa nyier

Nasubiri mtu anibishie ni funguke zaidi

Tunaomba sana uje ututembelee uone shughuli zetu kisha utuponde upendavyo lakini si kabla. Hututendei haki.

Hayo ya Arusha unaweza kuyafungulia uzi wake.
 

Sisi hatutoi hizo information za awali kwa mradi huu bila kusaini "non disclosure agreement" na yeyote yule ataependa kufahamu zaidi. Tuna miradi yetu tuliyoiweka wazi kabisa hapa JF unaweza kuitembelea ukaiona ukauliza, ipo wazi kabisa. Huu NO WAY.

Nimefurahi sana kuwa umebadilika kutoka kututuhumu utapeli wa million kumi mpaka kufikia kuwa sasa unahesabu gharama.

Karibu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…