Tunawamiss sana watangazaji hawa

Tunawamiss sana watangazaji hawa

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,203
Radio Tanzania RTD mama wa tbc ndio redio kongwe nchini. Imechangia sana maendeleo ya nchi yetu tangu Uhuru.
Huwezi kuzungumzia historia ya Tanzania bila kutaja mchango wa RTD.
Radio hii imesaidia sana kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Imesaidia kuwaelimisha Watanzania katika mambo ya siasa, uchumi, historia, afya na michezo.

RTD imesaidia kuliunganisha taifa hili linaloundwa na watu toka makabila mengi. Redio hii imekuwa mwalimu kwa wananchi wote toka siku nyingi. Elimu hii ilipitishwa kupitia watangazaji wake mahiri ambao hakika tutawaenzi daima.

Tunawamiss sana Julius Nyaisanga RIP, Halima Mchuka, Bati Kombwa, Sara Dumba, Paul Sozigwa, Abdallah Mlawa, Khalid Ponera, Thecla Gumbo, Mshindo Mkeyenge na wengine.
Tunauenzi pia mchango wa Halima Kihemba, Betty Mkwassa, Abdallah Majura, Charles Hillary, TIDO MUHANDO, Pascal Mayalla, Eda Sanga, Nswima Ernest, Jacob Tesha, Mikidadi Mahmoud, DAVID WAKATI, BEN KIKO na nk.
Pia wapo Yusuf Omar Chunda, Ahmed na Sango Kipozi, Abisai Stephen, Ahmed Jongo, Salim Mbonde, Suleiman Hega, Hamza Kasongo, Idrissa Sadalla na Suzanne Mongi.
Tunawamiss pia Vick Ntetema, Deborah Mwenda , Alecia Maneno, Sekion Kitojo, Ana Kidela, Suleiman Kumchaya, Mohamed Kisengo, Sued Mwinyi, Juma Nkamia na wengine wengi kama Shaban Kissu ambaye pia ni mtangazaji makini.
Sifa kwao pia ambao labda nimewasahau.
Watangazaji hawa nawaita kama ni "unsung heroes". Wametoa mchango mkubwa sana kwa nchi hii ingawa walikuwa wakilipwa mishahara midogo sana.
Wamekuwa wazalendo kwa nchi yetu kwa kiwango cha juu kabisa. Nchi iwaenzi watangazaji hawa ambao ndio walikuwa chachu ya kukuza umoja, uzalendo na mshikamanoTanzania.
 
Daaah!! Nimekumbuka mbali sana, kitambo hicho RTD, nikiwa bado dogo sana, ikifika saa 2 usiku tunasikiliza taarifa ya habari kwenye redio(zilikuwa zinaitwa redio mkulima), basi tunashindana kumtambua msomaji wa habari kwa sauti yake kabla hajajitambulisha. Kina Shaban Kisu, Swedi Mwinyi, Abdallah Mlawa, Sarah Dumba, Halima Mchuka, n.k.

Mungu awabariki sana walio hai na awapumzishe kwa amani waliotangulia.

Shukrani mkuu kwa kumbukizi hii. Nimekumbuka mengi sana.
 
Radio Tanzania RTD mama wa tbc ndio redio kongwe nchini. Imechangia sana maendeleo ya nchi yetu tangu Uhuru.
Huwezi kuzungumzia historia ya Tanzania bila kutaja mchango wa RTD.
Radio hii imesaidia sana kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Imesaidia kuwaelimisha Watanzania katika mambo ya siasa, uchumi, historia, afya na michezo.

RTD imesaidia kuliunganisha taifa hili linaloundwa na watu toka makabila mengi. Redio hii imekuwa mwalimu kwa wananchi wote toka siku nyingi. Elimu hii ilipitishwa kupitia watangazaji wake mahiri ambao hakika tutawaenzi daima.

Tunawamiss sana Julius Nyaisanga RIP, Halima Mchuka, Bati Kombwa, Sara Dumba, Paul Sozigwa, Abdallah Mlawa, Khalid Ponera, Thecla Gumbo, Mshindo Mkeyenge na wengine.
Tunauenzi pia mchango wa Halima Kihemba, Betty Mkwassa, Abdallah Majura, Charles Hillary, TIDO MUHANDO, Pascal Mayalla, Eda Sanga, Nswima Ernest, Jacob Tesha, Mikidadi Mahmoud, DAVID WAKATI, BEN KIKO na nk.
Pia wapo Yusuf Omar Chunda, Ahmed na Sango Kipozi, Abisai Stephen, Ahmed Jongo, Salim Mbonde, Suleiman Hega, Hamza Kasongo, Idrissa Sadalla na Suzanne Mongi.
Tunawamiss pia Vick Ntetema, Deborah Mwenda , Alecia Maneno, Sekion Kitojo, Ana Kidela, Suleiman Kumchaya, Mohamed Kisengo, Sued Mwinyi, Juma Nkamia na wengine wengi kama Shaban Kissu ambaye pia ni mtangazaji makini.
Sifa kwao pia ambao labda nimewasahau.
Watangazaji hawa nawaita kama ni "unsung heroes". Wametoa mchango mkubwa sana kwa nchi hii ingawa walikuwa wakilipwa mishahara midogo sana.
Wamekuwa wazalendo kwa nchi yetu kwa kiwango cha juu kabisa. Nchi iwaenzi watangazaji hawa ambao ndio walikuwa chachu ya kukuza umoja, uzalendo na mshikamanoTanzania.
Sijamuona Michael katembo ,Dominic Chilambo , huyo jamaa katangaza mechi leo kesho yake akavuta.
 
Back
Top Bottom