Tunawataka DP World, Wabongo wa bandarini tumewachoka wamejaa rushwa na urasimu. Kuwe na kipengere cha Mkataba kuisha kila baada ya Miaka mitano!

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Dp world waje ila kwa mkataba wa miaka mitano mitano, kila baada ya miaka mitano kuwe na option ya kuwaruhusu waendelee kukiwa na ufanisi ama waondoke wakizingua.

Kama Dp World hataki kuwa na mkataba wa miaka mitano, ije hata hio kampuni ya kigeni ambayo imepewa tenda kuendesha bandari ya Zanzibar kwa miaka mitano. ( mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadam mchungu, walitaka sisi tutoe bandari yetu milele wao ya kwao isimamiwe kwa miaka 5)

Bandarini kumejaa urasimu wa kujuana na rushwa kibao.

Watu wananenepeana kama nguruwe kwa kuendekeza rushwa, msione watu wanasomesha watoto wao familia nzima na michepuko huko feza boys / girls, majumba ya kifahari, magari ya kifahari, n.k. RUSHWA, RUSHWA L, RUSHWA!!
 
Ubinafsishwajj ni jambo la muhimu katika maendeleo ya nchi, hawa wazawa TPA wamejaarushwa hujumu, na ufisadi hii bandari inawanufaisha wachache. Tunamtaka DP WORLD kwa maslahi ya taifa
 
Kama Dp World hataki kuwa na mkataba wa miaka mitano, ije hio kampuni ya kigeni ambayo imepewa tenda kuendesha bandari ya Zanzibar kwa miaka mitano. (

Bandarini kumejaa urasimu wa kujuana na rushwa kibao.

Watu wananenepeana kama nguruwe kwa kuendekeza rushwa, msione watu wanasomesha watoto wao familia nzima na michepuko huko feza boys / girls, majumba ya kifahari, magari ya kifahari, n.k. RUSHWA, RUSHWA L, RUSHWA!!
Wewe unaweza kuwekeza sehemu mabilion kwa mkataba wa miaka mitano?
 
Kwenye biashara huwa tunaangalia faida ikiwepo ndio panaweza kuwa na uwekezaji.

Kwa akili yako umeona inashindikana kupata faida ya kusimamia bandari zote za Tanganyika kwa miaka mitano?
 
Ubinafsishwajj ni jambo la muhimu katika maendeleo ya nchi, hawa wazawa TPA wamejaarushwa hujumu, na ufisadi hii bandari inawanufaisha wachache. Tunamtaka DP WORLD kwa maslahi ya taifa
Ni kweli tunamuhitaji sana ila sasa asitake kuugeuza uhitaji wetu kwake iwe fimbo ya kutuchapia aamue anachotaka ambacho kitatubana mbeleni.

Dp world aje hapa awekeze tupo tayari kumpa babdari zote lakini iwe ni kwa muda wa kurenew mkataba kila baada ya miaka mitano,

Hapo Zanzibar wameipa kampuni kubwa tu mkataba wa miaka mitano kwanini isiwe kwetu?
 
Ubinafsishwajj ni jambo la muhimu katika maendeleo ya nchi, hawa wazawa TPA wamejaarushwa hujumu, na ufisadi hii bandari inawanufaisha wachache. Tunamtaka DP WORLD kwa maslahi ya taifa
Tafasiri ya hii ni kwamba mamlaka zetu/serikali haina uwezo kabisa wa kusimamia taasisi zake zikazaa matunda, unamaanisha miafrika hatuwezi kujiongoza kbs na kujiletea maendeleo yetu sisi wenyewe...bali, maendeleo yetu yataletwa na wageni....Watu weusi huenda tuna laana!
 
Hii ngozi nyeusi inalaana waafrika tumejaa ubinafsi na wala hatupo kwaajili ya maslahi ya taifa, watu wana waza matumbo yao. Image ni mara ngapi tumesikia ubadhilifu na ukatishaji wa fedha bandalini??? Na wahalifu hawachukuliwi hatua mashirika mengi ya serikali yamejaa rushwa na ufisadi. Ubinafsishwaji ni jambo la muhimu kwa maslahi ya taifa
 
Ubinafsishwajj ni jambo la muhimu katika maendeleo ya nchi, hawa wazawa TPA wamejaarushwa hujumu, na ufisadi hii bandari inawanufaisha wachache. Tunamtaka DP WORLD kwa maslahi ya taifa
Huu ni upumbavu wa hali ya juu. Huyo DP world alitengenezwa kutoka mbinguni? Kwa nini tushindwe kufanya kila kitu? Tulipata uhuru wa nini? Si tungewaacha wakoloni waendelee kututawala na ungekuta sasa hivi tuna maendeleo makubwa kabisa?
 
Kama TPA wenyewe wamekiri kushindwa kuiendesha bandari unafikiri kuna kingine cha ziada zaidi ya kumpa mwekezaji mwenye nia ya kuleta ushindani wa bandarini kikanda au wewe unafurahia jinsi tunavyopoteza mabilioni ya pesa na wapigaji wakiwa hao hao TPA unaowatetea
 
TPA kushindwa ndiyo watanzania wote wameshindwa? Hii bandari imefeli kwa sababu ya uongozi mbaya kutoka chama kinachotawala. Wanaingiza siasa na kuchagua mafisadi kuongoza TPA. Kama ni kuondoa chanzo cha matatizo basi inatakiwa tuanze na uongozi wa nchi. Ni bora hata tuajiri rais, mawaziri na watendaji wakuu wa wizara kutoka nchi za nje.
 
hata uingereza na india kuna bandari zake zinaendeshwa na wageni ili kupata maximum returns.

kubinafsisha ni suala la kuwapa wenye utaalam zaidi walete return zaidi sio mambo ya utaifa.

cha muhimu mkataba uwe feasible, sio kwa mikataba hii ya milele.
 
Ubinafsishwajj ni jambo la muhimu katika maendeleo ya nchi, hawa wazawa TPA wamejaarushwa hujumu, na ufisadi hii bandari inawanufaisha wachache. Tunamtaka DP WORLD kwa maslahi ya taifa
Yes lakini tusiweke mkataba ambao tutakuwa on the losing side, hauna mwisho na ni ngumu kuuvunja hadi muarabu akubali, hakuna mkataba kama huo duniani huu ni wizi na rushwa kwa watu wachache ,baadae inapotakiwa kuvunja wote tutalipishwa kwa namna moja au nyingine
 
Kuwaajiri Raisi , mawaziri na watendaji wakuu kutoka nje ya nchi hilo haliingii akilini huko tutakuwa tuna jinyan'ganya uhuru wetu.

Ni bora ubinafsishwaji ili kuwepo na makubaliano baina ya mwekezaji na serikali njia hii itapunguza mianya ya rushwa huko bandarini.
 
Ubinafsishwajj ni jambo la muhimu katika maendeleo ya nchi, hawa wazawa TPA wamejaarushwa hujumu, na ufisadi hii bandari inawanufaisha wachache. Tunamtaka DP WORLD kwa maslahi ya taifa
Umelipwa sh ngapi?
 
hata uingereza na india kuna bandari zake zinaendeshwa na wageni ili kupata maximum returns.

kubinafsisha ni suala la kuwapa wenye utaalam zaidi walete return zaidi sio mambo ya utaifa.

cha muhimu mkataba uwe feasible, sio kwa mikataba hii ya milele.
Uingereza na India siyo Tanzania. Badnari walizowapa hawajawakadhi kila kitu kama tulivyo sisi. Pia wameweza kufanya mengine mengi. Sisi tunashindwa kila kitu.
 
Dp world waje ila kwa mkataba wa miaka mitano mitano, kila baada ya miaka mitano kuwe na option ya kuwaruhusu waendelee kukiwa na ufanisi ama waondoke wakizingua.

Kama Dp World hataki kuwa na mkataba wa miaka mitano, ije hata hio kampuni ya kigeni ambayo imepewa tenda kuendesha bandari ya Zanzibar kwa miaka mitano. ( mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadam mchungu, walitaka sisi tutoe bandari yetu milele wao ya kwao isimamiwe kwa miaka 5)

Bandarini kumejaa urasimu wa kujuana na rushwa kibao.

Watu wananenepeana kama nguruwe kwa kuendekeza rushwa, msione watu wanasomesha watoto wao familia nzima na michepuko huko feza boys / girls, majumba ya kifahari, magari ya kifahari, n.k. RUSHWA, RUSHWA L, RUSHWA!!
Umelipwa sh ngapi?
 
Kuwaajiri Raisi , mawaziri na watendaji wakuu kutoka nje ya nchi hilo haliingii akili huko tutakuwa tuna jinyan'ganya uhuru wetu.

Ni bora ubinafsishwaji ili kuwepo na makubaliano baina ya mwekezaji na serikali njia hii itapunguza mianya ya rushwa huko bandarini.
Tatizo la rushwa haliko bandarini tu. Kwanza huko bandarini ni sehemu ndogo sana. Rushwa iko kwenye serikali nzima. Hata hizo zitakazopatika huko bandarini zitapigwa juu kwa juu na kina Samia na Rostam.
 
Yes lakini tusiweke mkataba ambao tutakuwa on the losing side, hauna mwisho na ni ngumu kuuvunja hadi muarabu akubali, hakuna mkataba kama huo duniani huu ni wizi na rushwa kwa watu wachache ,baadae inapotakiwa kuvunja wote tutalipishwa kwa namna moja au nyingine
Ukomo kwa mwekezaji ndio jambo tunalolitaka sisi.
 
Back
Top Bottom