talentbrain
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 1,187
- 760
Mi nadhani hatuna malengo mazuri kwa taifa hili, walianza na kuwabeba wanawake, wakawekewa vigezo vya chini, mara wakawekewa viti maalum, mwisho wakasema wapewe uspika na wakapewa. Hawakuishia hapo wakaja kwenye elimu ya juu, ikawa si kufaulu tu mitihani bali combination ambapo bila kutafakari wakazishusha hadhi baadhi ya combination. Hawakuishia hapo wakaleta ujinsia, mara kwenye mikopo wakaja waliosomea private na government, hawakuridhika sasa wa NACTE wametengwa na kwakuwa tumezoea kubaguana sasa habari ya mjini ni kufiwa na wazazi wote ili upewe mkopo. Je, sisi wenye wazazi masikini tuwauwe wazazi wetu?
Hakuna sababu ya kubashiri kwani hali ya uchumi wa mtu anaijua mwenyewe. Mpaka anaomba mkopo anautaka. Kwanini wasingetoa 50% kwa wote?
Hii ni bodi ya mikopo na sio NGO, ndio maana watu wanakopeshwa na wanakuja lipa na riba.
Hebi jiulize,je ni haki kumpa mtoto wa pedeshee 50% na mtoto wa mvuvi nae apewe kiasi hicho hicho....??
Lazima baadhi ya vigezo japo havina accuracy to 100% vitumike ili kuwatenganisha mapedeshee na wavuvi.....
Hata kama wangekuwa NGO haimaanishi kuwa wanaendeshwa kulingana na wateja wao...
Pia kumbuka kua kila asasi ina sheria,masharti na vigezo...
Kwanza ikumbukwe kuwa,heslb wana kifungu kinachoainosha kuwa kupata mkopo si lazima,maanake nini??
Hivi unajisikiliza? Unahakika gani kuwa wafaidika wa mkopo kwa 100% ya mkopo ni watoto masikini?
Bodi ipo kwa ajili yetu ndo maana inatumia pesa za kodi zetu kufanya kazi zake. Kila mwaka wanaongezewa pesa ili watuhudumie na utambue uwepo wa bodi ni kuhakikisha watu wanasoma na sio kuwazua watu wasisome. Sasa kusema kuwa wanakipengele kuwa ukikosa ni sahihi hakina mantiki.
Chukulia mfano;wewe ndio upo pale last say wa heslb;
je ungempa nani mkopo na kumnyima nani,wakati haujui family background ya applicant hata mmoja....
Hapa ndipo utakuta kuna vigezo fulani vinajitokeza kubashiri kua mtu fulani ni muhitaji mkubwa..
*yatima
*aliyesoma shule za serikali nk nk
Nakuona kama unatetea pasipokuwa na hoja! Wewe ndo mkurugenzi wa mikopo? Basi kama kweli wewe ni mfanyakazi wa hiyo Bodi nachelea kusema akili yenu ndogo! Unapotuuliza tungekuwa wasemaji wa mwisho pale HESLB tungefanyaje, nakuona kama mburula fulani hivi! Hivi unaona kabisa vigezo walivyoweka vinatoa taswira halisi ya wahitaji wakubwa? Basi mimi ningekuwa bodi ningeigawanya fedha iliyopo kidogo kidogo angalau kila mmoja apate japo 70%. Hapa kigezo kingekuwa kupata chuo tu!!
Mi nakupinga vilevile na kaulli zako hasa 2,,,ya kusema si busara kusema kuwa wanawake wanapendelewa,,hilo lipo wazi,,,wengi wao hawana vigezo na ndio maana grade zao zinashuswa,,,,,,kama kweli wanaweza wafight na vidume na washindane ili watoke siyo kuwashushia alama za ufaulu,,,,,kingine unasema coz za sayansi zimepewa vipaumbele,,,vipaumbele vipi hivyo na wakati 2po wengi 2 na 2na vigezo vya kupata hiyo mikopo 2nasoma engineering,,ha2pati hata sh 0,,,,na wanaopata ni wa2 ambao wanapga mabiashara na social sciences coz,,,,,ni hayo 2Napingana na wewe katika baadhu ya maeneo;
1.kuhusu kupendelea wanawake (si busara kusema hivo),jamii zetu za kiafrika zilikua na desturi za kuundergrade wanawake,kitu ambacho ni tofauti na haki za binadamu.Kwahiyo affirmative actions kama kuwapa nafasi kwenye sekta za uongozi,elimu,kazini,siasa nk nk ili kupunguza gender discrimination...
2.kuhusu elimu ya juu si vyema kusema kuwa baadhi ya michepuo imeshushwa hadhi, ni kwamba baada ya kuona kuwa kuna uhitaji mkubwa wa wanasayansi,michepuo ya sayansi ilipewa vipaumbele ili kuwapa motisha wanafunzi wasome hayo masomo....
3.kuhusu nikopo,nahisi nchi yetu haina uwezo wa kuwapatia wanafunzi wote hiyi mkopo,so inabidi ichaguo baadhi ya wanafunzi watakaonufaika na hiyo mikopo,,hapa ni hekima zaidi kuwapa wale wenye uhitaji,swali la kujiuliza ni;
Ni vipi utawatambua hao wenye uhitaji mkubwa wa mkopo...??
Mi nakupinga vilevile na kaulli zako hasa 2,,,ya kusema si busara kusema kuwa wanawake wanapendelewa,,hilo lipo wazi,,,wengi wao hawana vigezo na ndio maana grade zao zinashuswa,,,,,,kama kweli wanaweza wafight na vidume na washindane ili watoke siyo kuwashushia alama za ufaulu,,,,,kingine unasema coz za sayansi zimepewa vipaumbele,,,vipaumbele vipi hivyo na wakati 2po wengi 2 na 2na vigezo vya kupata hiyo mikopo 2nasoma engineering,,ha2pati hata sh 0,,,,na wanaopata ni wa2 ambao wanapga mabiashara na social sciences coz,,,,,ni hayo 2
Kuomba kuna mawili,kupata au kukosa,bodi haikusema kuwa wanafunzi wote walioomba watanufaika na mkopo,na kama mnakumbuka mwisho wa kujaza chaguzi za kozi na vyuo kuna sehemu ilitakiwa ukubali kuwa mkopo si guaranteed,na hata hizo priority course waliandika kiasi unachoweza kusaidiwa endapo utafanikiwa kupata mkopo,kwahyo kama hujapata mkopo ujue kuna mwingine kapata,c lazima wewe upate hata kama una vigezo kwa maana wapo wenye vigezo zaidi yako ndio maana wamepata na tatizo inginre msijiamini sana,inaonyesha mnajipaga mkopo kabla bodi hawajatoa majina,siku waki release majina mkiwa hampo ndio mnaanza kulalamika,hapo mlishapanga bajeti kbs,
Poleni sana