talentbrain
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 1,187
- 760
Mi nadhani hatuna malengo mazuri kwa taifa hili, walianza na kuwabeba wanawake, wakawekewa vigezo vya chini, mara wakawekewa viti maalum, mwisho wakasema wapewe uspika na wakapewa. Hawakuishia hapo wakaja kwenye elimu ya juu, ikawa si kufaulu tu mitihani bali combination ambapo bila kutafakari wakazishusha hadhi baadhi ya combination. Hawakuishia hapo wakaleta ujinsia, mara kwenye mikopo wakaja waliosomea private na government, hawakuridhika sasa wa NACTE wametengwa na kwakuwa tumezoea kubaguana sasa habari ya mjini ni kufiwa na wazazi wote ili upewe mkopo. Je, sisi wenye wazazi masikini tuwauwe wazazi wetu?