SoC04 Tunaweza kumaliza uhaba wa chakula

SoC04 Tunaweza kumaliza uhaba wa chakula

Tanzania Tuitakayo competition threads

hauleibrahim

Senior Member
Joined
May 17, 2024
Posts
183
Reaction score
125
Tanzania kama tukiamua kumaliza tatizo la uhaba wa chakula inawezekana ila Kwa kila mikoa yenye vilimo tunapaswa kuzingatia mambo machache yenye kuleta tija na kumaliza tatizo la uhaba wa chakula.

Kuna njia zinaweza kutumika kumaliza kama SI kushawishi Kwa vitendo watu Waka wajibika kulima sana na kuvuna chakula kingi.

Ili mkulima alime sana ni muhimu serikali iamue Kwa dhati kushirikiana na mkulima kule shambani kutambua changamoto za kiujumla za mkulima ili kujua kama serikali na wadau wa kilimo wanapata kuanzia wapi kufanya marekebisho ya kufanya watu kuwa na kilimo chenye tija na uhakika wa chakula Cha kutosha kila mkoa mpaka taifa kiujumla

Yako mambo machache ambayo wanapaswa kuyafuatilia Kwa vitendo huko mashambani Kwa wakulima na kuwasikiliza na wao kufanya Kwa vitendo ila kuacha mambo ya vilimo vya maneno visivyo kidhi kutatua changamoto ya uhaba wa chakula.

1.tuuze mbegu ZeNye sifa sahihi kuendana na hali ya hewa ya mkoa husika:tunaweza kuwa na wakala maalum wa mbegu maalum za kuendana na mkoa husika maalum kama ilivyo Tari.

2.tufanye majaribio ya mbegu mashambani Kwa kuwaonesha wakulima matokeo chanya ya mbegu husika:ni vizuri tunapo kuwa na wakala wa mbegu anaye endana na mkoa husika anapo pewa dhamana ni vizuri kuchukua wakulima wanao weza kwenda shambani kwao wakajifunza kwenye mashamba darasa ya mawakala wa mbegu hatua zote toka kupanda mpka kuvuna ili kujiridhisha na mchakato na matokeo ya mbegu hiyo.

3.majaribio yafanyike huku wakulima wakishiriki: Kun wakati ili mkulima ashawishike na kilimo Cha kisasa chenye tija vizuri wao wakawa wanaona kila hatua za majaribio za mbegu shambani ili kuwashawishi wakulima kuona matokeo ili wapate morali ya kilimo cha tija.

Njia ya kuona itasaidia kuwa elimisha Kwa vitendo wakulima kujua kiundani hatua zote ni vizuri hili zoezi liwe endelevu na kubadilisha wakulima kila wakati wa majaribio ya mbegu ili kuwapa WiGo Mpana wakulima wengi kujifunza na kuelewa kila aina ya mbegu ziingiapo mkoani kwao.

Wakulima wengi ni matomatho ndo mana sayansi ya kilimo Hawai amini sana wanaona n upigaji tu wa fedha zao matokeo yake wamebakia wakilima kizamani zamani na kutumia mbegu za kienyeji Kwa kuogopa gharama zisizo na matokeo chanya.

Kuna mkulima alipiga dawa mti wake wa matunda ya maembe ya kulinda maua kupukutika ila hakupata matokeo chanya ya matunda mpka Sasa haamini ktika sayansi ya kilimo. Kwa hiyo ni jukumu la wataalam kutoa elimu na dawa Bora ili kumshawishi mkulima kuamini sayansi ya kilimo itoe matokeo chanya ili aweze kuwekeza kwenye kilimo chenye sayansi na matokeo makubwa.

Kilimo kinaweza kuleta mazao mengi kikiwekezwa Kwa ushirikiano mkubwa wa wataalam na wakulima Kwa pamoja Kwa miaka mingi sana kama umoja utakuwepo katika nchi.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom