SoC03 Tunaweza kupita njia yetu

SoC03 Tunaweza kupita njia yetu

Stories of Change - 2023 Competition

Padrone

New Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
1
Reaction score
2
Tanzania taifa lililozaliwa miaka 59 iliyopita baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar lenye watu takribani milioni 60

Taifa ambalo mchezo wa Mpira wa miguu unapendwa zaidi kuliko mchezo wowote taifa ambalo kuanzia asubuhi mpaka usiku wake watu wanazungumzia Mpira wa miguu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye redio ,television ,mitandao ya kijamii na mitaani

Mpira wa miguu ndiyo mchezo pekee anaochezwa kila Kona ya hii Nchi

Sambamba na hayo piaMpira wa miguu ndiyo mchezo unaowatoa machozi ,Kuwaliza na kuwapa maumivu na majonzi makubwa watanzania wengi Kutokana na kuwapa matokeo wasiyo yataka na kuwanyima matokeo wanayo yataka

Washabiki wanahitaji mafanikio makubwa kwenye Mpira wa miguu kinyume na ilivyosasa

Mafanikio makubwa kwenye Mpira wa miguu ni ushiriki Bora kwenye mashindano makubwa na ushindi wa mataji kwenye hayo mashindano

Mashindano Kwa timu za Mpira wa miguu yapo ya ngazi za timu za taifa na ngazi ya vilabu

Tuanze na ngazi za timu za taifa mashindano makubwa Kwa ngazi ya timu za taifa ni Kombe la Afrika (Afcon) na kombe la Dunia

Timu za taifa Kwa jinsia zote mbili wanaume na wanawake zimegawanyika kwenye Makundi mawili

Kundi la timu za taifa za wakubwa na timu za taifa za vijana

Tuanze na timu ya taifa ya wakubwa wanaume taifa stars imeshiriki mara mbili kombe la Afrika (Afcon) na mara mbili pia kwenye kombe la Afrika Kwa wachezaji wa ndani (Chan) Kwa miaka yote 59 na mara zote ilizoshiriki haikufanya vizuri na wala haikuchukua kombe Kwa upande wa kombe la Dunia Taifa stars haijafanikiwa kupata nafasi ya kushiriki

Kwa timu ya taifa ya wanawake Twiga stars haijawahi kushiriki Kombe la Afrika (Afcon ) wala kombe la Dunia
Kwa upande wa timu ya taifa ya wavulana Serengeti boys imeshiriki mara moja Kombe la Afrika (Afcon) na haijawahi kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya wasichana Serengeti girls imeshiriki kombe la Dunia mara moja na haikushinda hilo taji na haijawahi kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Afrika (Afcon) kwahyo ushiriki na ushindani wa timu zetu za taifa kwenye mashindano makubwa ni wakusuasua

Kwa upande wa vilabu mashindano makubwa Kwa vilabu barani Afrika ni Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la shirikisho

Vilabu vyetu vya Tanzania vimekuwa na ushindani wa wastani kwenye mashindano yote haya mawili na hakuna timu kutoka Tanzania iliyowahi kushinda taji lolote Kati ya haya mawili

Twende kwa wachezaji wa Tanzania

Ukiangalia ushindani na ubora wa wachezaji wetu dhidi ya wachezaji wa mataifa mengine

Ubora wa ushindani wa wachezaji wetu kulinganisha na wachezaji wa mataifa mengine ni mdogo Hususani ukiangalia wachezaji wa kitanzania wanaocheza kwenye timu kubwa na ligi kubwa barani Afrika na ulaya hautawapata mathalani hakuna Mchezaji mtanzania anayecheza kwenye timu kubwa za ligi kubwa Afrika iwe Afrika kusini ,Misri ,Tunisia na Moroco na waliyopo kwenye hizi ligi ni wachache mnoo na wapo kwenye timu ndogo ndogo Hakuna mtanzania anayecheza kwenye timu yoyote ya ligi tano kubwa barani ulaya yaani ligi ya England ligi ya ujerani ,Ligi ya Uhispania ,Ligi ya Italia na ligi ya ufaransa

Ukirudi kwenye ligi Tanzania inapotokea timu yoyote ya Tanzania ina wachezaji wengi wa kigeni wachezaji wa kitanzania wachache ndiyo wanaopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Kwanza cha hiyo timu
Makocha

Upande huu wa makocha una sehemu mbili makocha wa timu za vijana na makocha wa timu za wakubwa
Kwa upande wa Makocha wa timu za vijana kama kuna sehemu Nchi yetu ipo nyuma zaidi basi ni kwenye hii idara ya makocha wa timu za vijana tunaomakocha kidogo sana waliyosomea ukocha wa timu za vijana


Kwa upande wa makocha wa timu za wakubwa wapo wengi japo Bado kunao walakini juu yao haswa linapokuja suala la kukosekana makocha wa Tanzania wanaofundisha nje ya Nchi wakati kuna makocha wengi wa kigeni wanaofundisha ndani ya Nchi yetu. Tunapoona timu kubwa na shindani ndani Nchi yetu zinatumia makocha wa kigeni na Hata timu yetu ya taifa kuamua kutumia makocha wa kigeni kuna Jambo halipo Sawa kwenye ubora wa makocha wetu

Ukifatilia mlolongo huu wa maelezo utakuonyesha kuwa Tanzania hatujafanikiwa na bado tupo nyuma Sana kwenye Maendeleo ya Mpira wa miguu Hii inatokana na kutowekeza na kutilia mkazo kwenye misingi sahihi ya Mpira wa miguu Hususani kwenye Soka la vijana ambao ndiyo msingi wa Maendeleo ya Mpira wa miguu wa Nchi yeyote ile

Na ndio maana inapelekea kuzalisha wachezaji wenye ubora mdogo wa ushindani mbele ya wachezaji wa mataifa mengine

Hatujawekeza kwenye Soka la vijana Kwa sababu kuu tatu ya Kwanza ni kukosa viongozi wenye uono sahihi pili kukosa sera sahihi (Dira) na uchumi mdogo

Suala la Viongozi sahihi na Dira linaweza kurekebishika Kwa kubadili namna ya kufikiri na kutenda na suala la uchumi tunaweza kukabiliana nalo Kwa kubuni mbinu mbadala kutokana na mazingira na uwezo wetu wa kiuchumi

Namna yakufanya
Hapa ndipo tunapokuja kwenye kauli yangu ninayosema .(Tunaweza kupita njia yetu na kufika walipo wao )
Ili tufike walipo wao tunapaswa kuwaweka kwenye Soka la vijana kama wanavyofanya wao ila ni Kwa kutumia njia yetu Kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi na mazingira ya kijiografia ya Nchi yetu

Tunapaswa kuja na muono na Sera rafiki na rahisi kutekelezeka

Kwa maoni yangu Sera hii hapa inaweza kutufikisha tunapotaka na kuyafuta machozi yetu na kuirejesha furaha ilipojificha

Open football academy (OFA) yaani Shule huria za Mpira wa miguu

Maana ya OFA
OFa ni Shule huria za Mpira wa miguu Tanzania zenye Malengo ya kuzalisha ,kulea na kukuza Vipaji vya Watoto wa Tanzania Kwa ngazi za Shule msingi ,sekondary na Mtaani

Malengo ya Ofa

Kuifanya elimu ya Mpira wa miguu iwafikie wachezaji wakiwa na umri sahihi na katika eneo waliyopo

Kubadili mfumo mzima wa Mpira wa miguu wa Nchi kutoka kwenye muono wa Mpira utamaduni kwenda kwenye Mpira taaluma na biashara

Kuzibadili timu za Mtaani za kawaida kuwa taasisi na kuendeshwa Kwa ueledi ili kulete matokeo chanya kwenye Soka letu

Kuzifanya Shule za msingi na Sekondary kufundisha Mpira wa miguu darasani na maeneo ya kuchezea (viwanjani)

Utekelezaji wake
Kwa kuzingatia Soka la vijana linachezwa kwenye maeneo matatu yaani shuleni ,Mtaani (kwenye jamii) na kwenye timu rasmi za Mpira miguu

Shuleni

Kwakuwa shuleni ndipo sehemu ambapo Watoto wanashinda Kwa muda mrefu na kukaa darasani basi ndiyo sehemu sahihi Kwa kupata masomo ya darasani yahusuyo Mpira wa miguu

Mtaani (kwenye jamii)
Mtaani ndipo sehemu ambapo Watoto wanacheza mara nyingi basi huku ndipo sehemu sahihi ya kupata elimu ya vitendo ya Mpira wa miguu

Ili OFA iweze kutekelezeka kikamilifu yafuayao yanapaswa kufanyika

Serikali

Kupitia wizara ya elimu ,Sanaa utamaduni na michezo na wizara ya Afya Kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (Tff) na wadau wa Mpira wa miguu waandae mtaala utakaotumika kufundishia shuleni yaani Shule za msingi na Sekondary

Wizara ya elimu itoe muongozo wa kila Shule ya msingi na sekondary kuwepo na mwalimu atakayefundisha somo la michezo na kuwepo na ratiba ya somo hilo

Wizara ya Sanaa utamaduni na michezo iwe inapanga fungu maalumu la kifedha zikuelekeza kwenye Vituo vitakazokuwepo Nchi mzima

Shiriko la Mpira wa miguu Tanzania (TFF)

Tff Kwa kushirikiana na wadau wa Mpira miguu waandae falsafa ya Mpira wa miguu Kwa Soka la vijana itakayotumika kufundishia kwenye Vituo vyoye nchini

Tff iandae mfumo maalumu wa kuvisajili hivi vituo ili viweze kutambulika rasmini nchini kote pia iandae wakufunzi Kwa kuanzia walau wanne kila mkoa watakao tumika kufundisha makocha watakao kuwa makocha kwenye hivivituo

Vyama vya Soka vya wilaya viandae kozi za makocha Kwa ajili ya upatikanaji wa walimu watakaofundisha kwenye hivi vituo Vyama vya Soka vya wilaya viandae semina elekezi Kwa ajili Viongozi wa vituo na wadau mbali mbali ili kurahisisha utekelezaji wake Uendeshwaji wa OFA

Uongozi
Vituo vitakuwa na mfumo wa uongozi na uongozi rasmi
Vituo vitakuwa na katiba
Mfumo wa kuwaweka Watoto Kwa kuzingatia umri

Uendeshwaji wa OFA kiuchumi
Kwa kuwa ofa itakuwa inahudumia Watoto wanaoishi nyumbani kwao na kuendeshwaji wake ni nafuu
Mahitaji yatakayokuwa yanahitaji Kwa kituo ni
Vifaa vya kuchezea ikiwemo mipira ,jezi ,bipsi na Koni pamoja viatu vya kuchezea
Upatikaji wa fedha za kuendesha kituo

Kupitia wanachama wa vituo
Wafadhiri na wadhamini wa vituo
Viongozi watakuwa wanajukumu la kutafuta wanachama .wafadhiri na wadhamini
Ruzuku kutoka wizara ya Sanaa utamaduni na michezo

Serikali kupitia wizara yake inayohusiana na michezo inapaswa kuvihudumia hivi vituo Kwa sababu vitakuwa ndiyo msingi mkubwa wa Maendeleo ya Soka la Nchi yetu

Ruzuku kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania Kwa kuwa Tff inapata fungu maalumu la fedha kutoka FIFA Kwa ajili ya maendeleo ya Soka la vijana inapaswa ilo fungu kuelekezwa kwenye hivi vituo

Ruzuku kutoka Halmashauri
Kila Halmashauri inapaswa kuandaa fungu maalumu Kwa ajili ya hivi vituo
Kwani ni moja ya jukumu la Halmashauri kuwawezesha vijana na Hawa waliyopo kwenye hivi vituo ni vijana wao

Matarajio ya OFA
Hivi vituo vikianza kufanya kazi yafuatayo tunayategemea
Itaibua chachu na ari mpya ya Mpira wa miguu hasa kwenye Soka la vijana
Wachezaji watazalishwa wengi na wenye ubora
Mafanikio mengine yatapatikana kwenye Nyanja zifuatazo

Kiuchumi
Mpira wa miguu ni Biashara Kwa makampuni wa watu binafsi wanaowekeza kwenye Mpira na ni kazi na ajira Kwa wachezaji ,makocha na watu wengine. Kwahyo Kutakuwa na ongezeko la ajira na ongezeko la biashara

Kijamii
Mpira ni burudani na starehe Kwa Wale washabikia na wapenzi wa Mpira pia unaondoa ubaguzi ,unaunganisha watu unaleta Hali ya kuheshimiana na kuoneana huruma Kwa ile kauli maarufu ya Uungwana michezoni (Fair play)

Mpira wa miguu unakemea vitendo vya uzalilishaji ,unyanyasaji na matumizi ya madawa ya kulevya
Kimataifa

Kulitangaza taifa ulimwenguni kote Kwa kuwepo Kwa wachezaji Duniani kote na kuongeza vivutio vya utalii

Note .. Tunaweza kufika walipo wao Kwa kupita njia yetu .
#OFA
 
Upvote 2
Back
Top Bottom