Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
Zab 108:13 SUV
[13] Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
Mtu akikuangalia ulivyo, ulipozaliwa, kazi yako, biashara yako, elimu yako, maisha yako, anaweza asiamini juu yako unaweza kufanya mambo makubwa katika maisha yako.
Jamii zetu zinatuona hivyo, familia zetu vile vile zinatuchukulia kawaida wakati mwingine, wafanyakazi wenzetu, na wafanyabiashara wenzetu, mpaka pale wanapoona kitu kikubwa kimetokea ndipo hushtuka na kuona utofauti wetu.
Ipo nguvu ya ushindi kwa mtu anayemtegemea Mungu, mtu anayeamini MUNGU anaweza kumsaidia kutenda mambo makubwa katika maisha yake, uwe na uhakika mtu huyu lazima afike mahali ambapo haikutegemewa afike kwa akili za kawaida.
Watu wanaweza kutuweka katika vipimo vyao kutokana na wanavyotufahamu kimwili, lakini hawajui tunaweza kutenda mambo makubwa kwa msaada wa Mungu na kushinda vizuizi vyote vinavyojitokeza mbele yetu.
Kwa Kumtegemea Mungu tunaweza kufanya mambo mbalimbali makubwa yaliyo nje ya uwezo wetu wa kawaida, nikimaanisha ule uwezo uliozoeleka na ndugu zetu, marafiki zetu, na wazazi wetu, uwezo unaopimwa kwa macho ya nyama.
Mungu anaweza kutupa ushindi mkubwa dhidi ya maadui zetu, adui yetu au mtesi wetu mkubwa anaweza akawa njaa, watu, hali zetu, ama changamoto zetu tunazizopitia wakati huo, lakini kwa uwezo wa Mungu tutayashinda hayo yote na kufikia ushindi wetu.
Ondoka na hii, ushindi wetu unatoka kwa Mungu, hatushindi kwa akili zetu au kwa ujanja wetu au kwa uwezo wetu wa kifedha, tunaweza kutegemea hayo tukashindwa vibaya sana, vizuizi vingine ni vya kiroho, haviangalii pesa zako nyingi, wala haviogopi elimu yako kubwa, bali vinamwogopa Mungu wako.
Mtumaini Mungu siku zote za maisha yako, na mtegemee Yeye nyakati zote, ukijua msaada wa uhakika na wa pekee unatoka kwake, pale unaposhindwa kwa akili zako za kibinadamu Yeye yupo kukusaidia ufikie hatima yako njema.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia
Mungu akubariki sana