Kenya ni taifa katika mazingira halisi tuliyomo sisi. Hata hivyo taifa hili limepiga hatua kubwa sana kidemokrasia zenye kustahili kupigiwa mfano.
Hizi tantarira za eti kuwa IEBC ni sawa tu na NEC yetu, kwamba ya Kenya tuwaachie wakenya wenyewe, nk nk, zote ni kelele za vyura tu. Nia na madhumuni kutupoteza maboya tuache kuzichambua mbivu za wenzetu dhidi ya mbichi zao.
Haipo shaka kuwa ukaribu usiokuwa na afya baina ya Raila na shujaa wetu, ulimweka Raila kwenye upande dhoofu wa historia ya wapigania haki. Hata hivyo weka mahusiano hayo binafsi na jiwe pembeni, huyu bwana ni jembe haswa na demokrasia ya Kenya inayo mengi ya kumkumbuka nayo.
Kwa hakika wandugu kama ni kwa dhati tunataka haki, demokrasia au katiba mpya? Baba anayo majibu na anayo njia inayoweza kutufaa:
Raila anaongelea watu milioni moja kuifanyaia mageuzi mahakama kwa anachoamini moyoni kuwa hakipo sawa.
Kwani kwetu, kuna hata aliyewahi kutamka anahitaji watu wangapi Ili kufanya nini? Kwani agenda yetu ni nini basi?
Au kwetu sisi ni uwoga (playing it safe) na kutegeana (opportunism)?
"Woga kuchelea kulipa gharama zozote au kutegeana yaani kuwa mkao wa kifursa zaidi Ili kujilia matunda yakipatikana kwa gharama za wengine, kiulaini?"
Tunataka katiba mpya. Iko wapi roadmap ya kufanikisha tunayafikia malengo yetu?
Tupende au tusipende, Baba anaweza kuwa wa msaada kwetu pia.
Source: Raila, Rigathi in surprise meeting