Tunayopenda Tusahau

Tunayopenda Tusahau

Mzee wetu, Mohamed Said, kuna platform yeyote ilipo historia uliyoandika (documents, audio or visual) inayohusu Palestine na mzozo wake Middle East?

Mimi natamani kujifunza, kama naweza kupata darasa lako nitashukuru,

NB: Mimi ni mwanafunzi wako kwenye jukwaa hili,Asante!
Yurri,
Sote ni wanafunzi hapa tunasoma:
  1. BAADA YA KUONDOKA BABA WA TAIFA TANZANIA BADO INAUNGA MKONO PALESTINA? SIKU YA QUDS - STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR
  2. BALOZI WA TANZANIA ISRAEL
  3. SHEIKH ALI SALEH ALIIUNGA MKONO PALESTINA AKITUMIA MEMBARI YA MSIKITI WA KITUMBINI MIAKA YA 1940
Soma na hii:
 
Prof. Ibrahim Lipumba ni msomi wa kutajika katika kundi kubwa lolote la wasomi popote pale duniani.

Prof. Lipumba aliingia katika siasa mwaka wa 1995 si kwa mapenzi yake bali kwa kuchagizwa na marafiki zake kufuatia kifo cha ghafla cha Prof. Kighoma Malima.

Mwaka wa 1995 aligombea urais kwa tiketi ya CUF na kuanzia hapo aliweza kuijenga CUF kufikia kuwa chama chenye nguvu.

Lakini kubwa katika historia ya vyama vya siasa Tanzania ni kule CUF Bara kwa wakati ule kutia nguvu kubwa katika siasa za visiwani na kuifanya CUF chama pekee katika vyama vya upinzani ukiondoa CCM, chenye wafuasi wengi Tanzania Visiwani na Tanzania Bara.

Hakuna chama chochote Bara ambacho kimeweza kutimiza hili.

Katika haya yote mchango wa Prof. Lipumba ulikuwa mkubwa sana usio na kifani.

(Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania August 22, 2016 0)

View attachment 2891363
Prof. Lipumba wa kwanza kushoto, Shekue Pashua na wanachama wa CUF nyumbani kwa Mama Ummi bint Anzuani (aliyevaa nguo nyekundu) Tanga 1995​
Shekue alirudi kugombea ubunge tanga mjini kupitia CCM mwaka 2020 kura hazikutosha amestaafu akiwa katibu wa CCM wilaya huko manyara.
 
Kama Sykes ameandika kwa msingi ya utaifa naweza shawishika kusoma, lakini kama ameandika kwa malalamiko ya Waislam kubaguliwa na utawala wa Nyerere kwasababu ya ukristo wake, utaniwia radhi.

Kuna andiko mzee Said ulilokuwa ukilalamikia serikali ya Nyerere kuwanyima ruhusa mashirika ya Kiislam ikiwemo OIC kujenga vyuo vikuu, kama kweli ilikuwa hivyo. Ninaelewa sasa ni kwanini Nyerere aliona mbali na kufanya hivyo. Na ndiyo maana hata Shule na Hospital zizokuwa zikimilikiwa na kuendeshwa na madhehebu ya kikristo alizitaifisha.
A. Sykes hakua mdini, bali purely nationalistic. Ukisoma hiki kitabu kina taswira mbili;kwanza ni maisha ya kihistoria yake [account ya Historia ya Tanzania]-na ndio ubora wa hiki kitabu ulipo, na pili ni tafsiri ya Mwandishi Juu ya Historia hiyo ya A. Sykes[his thesis ya Uislam na Uhuru wa Tanganyika]-ambayo to me, ni flawed view. So, kama unapenda kuijua historia yetu, its a must-read, but with open mind.
 
A. Sykes hakua mdini, bali purely nationalistic. Ukisoma hiki kitabu kina taswira mbili;kwanza ni maisha ya kihistoria yake [account ya Historia ya Tanzania]-na ndio ubora wa hiki kitabu ulipo, na pili ni tafsiri ya Mwandishi Juu ya Historia hiyo ya A. Sykes[his thesis ya Uislam na Uhuru wa Tanganyika]-ambayo to me, ni flawed view. So, kama unapenda kuijua historia yetu, its a must-read, but with open mind.
that...
Ahsante sana.
 
Cover photo ya hicho kitabu inapalilia chuki na kama sikosehi kinachoongelewa hapa ni mauaji yaliyotokana na fujo za Mwembechai - Magomeni. Ni bahati nzuri niseme huu ulikuwa ni utawala wa Mwinyi.
Yaani hapa tayari umeshawakilisha jina lako yaani Mbuzi
Tena ni mbuzi fulani ya maporini inakurupukia vitu hata havielewi, utafakamia majani ya kisamvu utavimba tumbo mbuzi wewe
Na kufuatilia utumbo wote ulioandika humu unaonyesha kabisa ni mporipori na mlugaluga wa vijijini
Kama hujui kitu kaa kimya kenge wewe sio unashobokashoboka kama mdada mwenye mimba changa mbuzi wewe
 
Mohamed, unajisikiaje kupost vitu vyenye uelekeo wa kupalilia chuki kwa misingi ya imani za kidini? Hayo mauaji unayoyafanyia reference, unatuletea hizo picha mulizogawiana na Lipumba gesti ili iweje? Nijuwavyo Lipumba ni kiongozi wa chama cha siasa kumbe uchochoroni ni gaidi anaejaribu kueneza chuki za kidini, siyo? Too low for a Prof. to behave such way.

Kwenye post yako moja ya Rais kupewa mwaliko Vatican unahusisha mwaliko huo na maswala ya bandari na mikataba ya DPW, na umejaribu kujitungia na kueleza vitu vya hovyo kabisa. Hivi wewe ukoje? Unadhani huko Vatican wana shida na hizi bandari zenu? TEC ni Baraza la maaskofu hapa Tanzania, si Baraza la Vatican na Chadema ni chama cha siasa hakina uhusiano ama na Ukatoliki au dini yoyote, iweje uwafungamanishe hata kama hoja zao zilikuwa za aina moja kwenye kupinga mkataba wa hovyo ambao serikali ilitaka kuingia na hiyo kampuni.
Huyu ni moja kati ya wazee wa hovyo kabisa kuwahi kutokea, n8 mdini,mchochezi na mbaguzi mkubwa.
 
Mbussi,
Sina msimamo wowote dhidi ya dini yeyote.

Wala hakuna ushahidi popote kuwa Uislam ulipata kupanga njama dhidi ya dini nyingine.

Soma kitabu cha Abdul Sykes uone historia ya Waislam katika kujenga umoja.

Tazama picha hizo hapo chini:
Wewe huna lingine unaloweza kuandika,au wewe ni mwandishi wa waislamu?
 
Wewe huna lingine unaloweza kuandika,au wewe ni mwandishi wa waislamu?
Yve...
Nimeandika mengi kuhusu Uislam na Waislam Tanzania.

Sababu ya kufanya hivi ni pale nilipogundua kuwa wanahistoria wa Tanzania walikuwa wanaikwepa historia hii.

Huwa napokea msg mfano wa hiyo hapo chini kutoka kwa watu wengi sana:

1707501517612.jpeg
''Mtu anaweza kuviona kama ni vitabu vya kawaida lakini kwangu ni moja ya vitabu vilivyonifanya nitetee hoja kwa kujiamini na ujasiri kwani vimenitoa katika ombwe kubwa ...

Allah akuzidishie kheri ndugu yangu...''
 
Huyu ni moja kati ya wazee wa hovyo kabisa kuwahi kutokea, n8 mdini,mchochezi na mbaguzi mkubwa.
Yve...
Husemi kweli.
Wabaguzi, wachochezi, wadini nk ni wale waliovunja EAMWS kwa kuwa ilikuwa inajenga Chuo Kikuu.

Wabaguzi, wadini, wachochezi ni wale waliokataa kutoa kibali OIC kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Wabaguzi, wadini nk ni wale waliofuta historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa hofu ya Uislam.

Mbaguzi na mchochezi siwezi kuwa mimi kwa kutahadharisha haya nchini petu.

Kiswahili kizuri ni "ovyo," si "hovyo."

Sifa hizo za udini nk.
Si zangu.

Wenye sifa hizi wanajijua.
 
Back
Top Bottom