mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Ni giza nene sana limetanda mbele ya macho ya wataalamu tulio nao katika nchi yetu. Wataalamu hawa wamebaki na taaluma zao bila ya kujua mahali gani wazipeleke taaluma hizo ili ziweze kuwanufaisha wao wenyewe na Jamii kwa ujumla.
Nchi yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha vijana wake wasome kwa bidii taaluma mbalimbali ikiamini kuwa kufanya hivyo ni kutengeneza taifa hai, taifa lisilo na wajinga, taifa lenye nguvu na lenye upeo wa kufanya mambo kisomi zaidi.
Matokeo ya jitihada hizo za kuhamasisha vijana kusoma ni kupata wataalamu wengi wenye ujuzi mkubwa kwenye nyanja mbalimbali za elimu.
Kwa hatua iliyofikiwa na nchi yetu kwa sasa haina upungufu mkubwa sana wa wataalamu katika nyanja mbalimbali kama vile walimu, madaktari, wahandisi na taaluma nyinginezo.
Hakika vijana wametimiza wajibu wao.
Lakini je, tunanufaika vipi kama taifa na taaluma za vijana hawa?
Baada ya mwanafunzi kuhitimu masomo yake ya taaluma yoyote anatarajia kupata Sehemu ya kwenda kuwasilisha ile taaluma yake aliyosomea. Lakini kwa Tanzania imekuwa tofauti vijana wanasoma huku wakijua kabisa kuwa baada ya hapa hamna Sehemu ya kukipeleka hiki ninachosomea.
Lakini hilo ni moja suala lingine linalotia doa wataalamu wetu ni kuwa hata kama wamekosa Sehemu ya kunufaisha jamii bado serikali na jamii kwa pamoja havionekani kuthamini mchango wa wataalamu hawa hata kidogo kutokana na kutotumika katika Jamii na kila mtu kufanya chochote anachohitaji hata kama hana ujuzi na iko kitu matokeo yake ni kuharibu.
Zipo baadhi ya dalili za wazi kabisa za miaka ya hivi karibuni zilizoonyesha kutotambua mchango wa wataalamu katika nyanja zao hali hiyo inapelekea hata serikali kuingia hasara katika baadhi ya miradi kutokana na baadhi ya sekta kutotumia wataalamu kabla ya kuweka pesa katika miradi husika.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio yalioonyesha kutothaminiwa kwa wataalamu tuliowasomesha kwa pesa zetu wenyewe:
Kujengwa kwa masoko mengi yasiyotumika
Katika kipindi kama cha miaka minne iliyopita serikali iliamua kuwekeza katika miundombinu ya masoko. Hilo lilikuwa ni jambo zuri ukizingatia masoko yaliyojengwa yalikuwa ya kisasa zaidi. Richa ya masoko hayo kuwa ya kisasa lakini hata baada ya masoko hayo kukamilika bado wafanyabiashara waliendelea kufanya biashara zao Sehemu za mwanzo ambazo hazikuwa na miundombinu mizuri.
Hapo tatizo lilikuwa kutoshirikishwa kwa wataalamu pamoja na wananchi kabla ya ujenzi wa masoko hayo mapya. Kama wataalamu wangeshirikishwa kabla ya ujenzi wa masoko hayo naamini wangefanya utafiti Kabla na wangepata Sehemu sahihi za kujenga masoko hayo. Majengo yakabaki hayana matumizi tena.
Picha kutoka mtandaoni Nilitegemea baada ya hilo kosa la kwanza wangerudi kwa wataalamu hao kuwauliza tufanye nini ili masoko haya wafanyabishara na wateja wavutiwe nayo? Lakini hawakufanya hivyo bali nilisikia tu kauli ikisema masoko hayo yatafutiwe shughuli nyingine ya kufanyia.
Hii pia haikuwa kauli ya kitaalamu kwa sababu wapo wataalamu wa masoko wangeweza mikakati mizuri ambayo ingewavutia wafanyabishara kupeleka biashara zao pale na wateja wangepatikana.
Janga la UVIKO-19
Nchi yetu imebarikiwa wataalamu wengi sana wa afya wa nje na ndani ya nchi. Ugonjwa wa UVIKO-19 ulipoingia tulienda nao kwa pamoja na wakitupatia maelekezo ya mbinu mbalimbali za kufanya ili tuweze kuepuka maambukizi ya ugonjwa huo hatari. Lakini katikati ya safari ya vita hiyo tuliwasaliti wataalamu wa afya na tukawaona waongo na wanatuchelewesha kufanya mambo yetu.
Tukawaita waongo na wafuasi wa mabepari hatukujua kama kufanya hivyo ni kosa kubwa tulilikabili janga hili kwa matumizi ya akili zetu ambazo hazikuwa na utaalamu wowote wa kiafya Tukachukua kauli ya “ukale washinda usasa” Mungu nae akataka kutuonesha kuwa tunapaswa kuwaheshimu wale aliyewapa tunu ya elimu.
Picha kutoka mtandaoni
Tukapoteza ndugu zetu wakaisha, wakateketea kama wadudu. Tulipokuja kuzinduka tena tumeshachelewa. Tunarudi tena kwa wataalamu wale wale tuliowaita waongo wakatupokea tena na kutupa njia sahihi za kujikinga lakini wahenga wanasema “maji yakimwagika hayazoleki” ndugu zetu wa muhimu tulishawapoteza tayari kwa kutowaheshimu wataalamu wa afya. Sasa kama hatuwaamini tulizalisha wengi ili wafanye kazi gani?
Ujenzi wa bwawa la umeme Rufiji
Mradi wa bwawa la umeme Rufiji ni miradi mkubwa sana na utaleta tija kwa taifa pale utakapokamilika.
Lakini katika hili nimesikia baadhi ya wataalamu wakileta hoja kadhaa ambazo kwa upeo wangu wa kufikiri nimeona kama zina chembe ya mashiko.
Kwa sasa Tanzania inazalisha megawati 1500 kupitia vyanzo tofauti tofauti vya umeme wakati huo mradi wa bwawa la umeme la Nyerere endapo mradi utakamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2115. Ni megawati nyingi sana lakini swali la msingi hapa ni kwanini hayo mabilioni ya pesa yaliyotumika na yanaendelea kutumika kwenye mradi huo yasingetumika kuboresha vyanzo hivi vingine vilivyopo nchini.
Mfano tuna gesi asilia nyingi sana nchini lakini haijatunufaisha kwa kiasi kikubwa kutokana na kukosa teknolojia itakayotuwezesha kuichakata gesi hiyo ili iweze kutunufaisha. Nadhani ingekuwa vizuri zaidi kama pesa hiyo tungeiwekeza uku kwenye gesi ili tuvune umeme mwingi zaidi kupitia gesi asilia ukizingatia umeme wa maji hauna uhakika sana kwa sababu maji wakati wowote yanaweza kupungua. Hata hapa pia nina imani wataalamu waliwekwa pembeni au walishirikishwa ila maoni yao hayakuzingatiwa.
Wataalamu wa Kiswahili
Kila mwaka katika nchi yetu wanahitimu wataalamu wengi sana wa lugha ya kiswahili ambayo ndio lugha mama ya taifa hili. Lakini uwingi wao haufanani na mchango wao katika kukikuza kiswahili kitaifa na kimataifa. Lakini ukifanya utafiti rahisi utagundua kuwa kwa sasa dunia ina uhitaji mkubwa wa wataalamu wa kiswahili na sio kama wataalamu hilo hawalijui , Lahasha! wanalijua ila wamekosa njia na mwongozo wa kufuata ili wanufaike na soko hilo la ajira.
Kwa sasa nchi yetu haina uwezo wa kuwaajiri wataalamu wote wa lugha ya kiswahili hivyo basi kama nchi ilitakiwa itafute namna ya kuwasambaza au kuwawekea njia rahisi ya kulifikia soko la kiswahili ili lugha izidi kukua na hawa wataalamu nao wanufaike na taaluma yao. Lakini ikiwa tutaendelea kuwaacha hivi hivi basi hata wale vijana waliokuwa na ndoto ya kuwa wataalamu wa kiswahili kule chini tutawapoteza.
Mapendekezo
Hitimisho
Serikali inapaswa kutambua kuwa inatumia pesa nyingi sana za wananchi kuwasomesha vijana hawa lakini pia hao hao wananchi nao wanatumia pesa kuwahudumia vijana wao ili waondokane na ujinga na matarajio makubwa ya serikali pamoja na wananchi wake ni kuona mwisho wa vijana hawa ni kuja kulinufaisha taifa hili tukufu na kama watashindwa kunufaisha taifa basi iwepo njia rahisi ya wao kwenda kusaidia jamii nyingine nje ya Tanzania hiyo itasaidia kutangaza taifa letu ikiwa watatuwakilisha vizuri.
Tunapowaacha mtaani wanadhalilika, hatuwatumii lazima wataenda kufanya kazi tofauti na zile walizosomea jambo ambalo litafanya nchi yetu kutokuwa na ufanisi katika kila tunachokifanya kutokana na kutokuwa na watu sahihi katika mahali sahihi.
Ahsanteni

- Hatupaswi kutekeleza mradi wowote bila kuwashirikisha wataalamu wenye ujuzi na huo mradi
- Tunatakiwa Kuthamini na kuheshimu mchango wa wasomi wetu katika Taifa hili

Upvote
7