Tunda aina ya Parachichi tunavyolichukulia hapa kwetu ni tofauti na wenzetu

Tunda aina ya Parachichi tunavyolichukulia hapa kwetu ni tofauti na wenzetu

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Jambo lilonishangaza baada ya mzungu mmoja kutoka ufaransa kufakamia maparachichi.

Nikamuuliza mbona unakula sana haya maparachichi ndipo kunifungulia ukweli kuwa ni bei sana kwao .

Kumbe tuna vyakula ambavyo tunachukulia ni vya kawaida ila kwa wenzetu vikawa vya kitajiri sana.

IMG_5936.jpg
 
South Africa tunanunua rand 20 mpaka 30 moja, r 1 ni shilingi150 ya bongo
 
Parachichi ni hela kule Njombe ukiiba kuku unaweza samehewa Ila sio uibe parachichi watu wanatajirika kwa parachichi hasa zile za vipele ndo dili
 
Jambo lilonishangaza baada ya mzungu mmoja kutoka ufaransa kufakamia maparachichi.

Nikamuuliza mbona unakula sana haya maparachichi ndipo kunifungulia ukweli kuwa ni bei sana kwao .

Kumbe tuna vyakula ambavyo tunachukulia ni vya kawaida ila kwa wenzetu vikawa vya kitajiri sana.

View attachment 2174091
Hakuna tofauti kubwa hizo bei. Parachichi kubwa Tanzania linauzwa mpaka sh 1500/- , huko kwao ni dollar 1(sh 2300/)
 
Bei zetu zinatokana na GDP yetu na mzunguko wa pesa mtaani. Unataka tuuze parachichi $4 ni wangapi watamudu kununua?
 
Tatizo ya bongo species kama zinazopatikana BUKOBA zimejaa maji ni testless, labda zile za kilimanjaro na mbeya
 
Tatizo ya bongo species kama zinazopatikana BUKOBA zimejaa maji ni testless, labda zile za kilimanjaro na mbeya
Yale ya hivyo yanaitwaga makubwa jinga. dude kubwa kama kichwa ila lina ladha ya maji.upuuzi mtupu. Mbeya na kilimanjaro ndiyo product yenye radha.sema zile mbegu zinatafutwa ili ziuwawe zipotelee mbali.tuendelee kuagiza za wenzetu kama walivyofanikiwa kwenye matikiti,mpunga na mahindi.
 
Back
Top Bottom