Tunda gani ulikuwa unalitamani kutokana na kusifiwa ila baada ya kulionja hulitaki tena?

Tunda gani ulikuwa unalitamani kutokana na kusifiwa ila baada ya kulionja hulitaki tena?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Nilikuwa nikisikia sifa zinazopewa kwenye tunda linaitwa embe ng'ong'o nilikuwa natamani sana kulionja kwa kuwa huku kwetu kanda ya magharibi halipo na kama lipo mie sijwahi kukutana nalo.

Nikawa natamani sana kulionja, ila siku niliyolionja nikasema chaaa nini hiki, sitaki hata kulisikia tena na nalipa alama 1 kati ya 10

Wewe tunda gani unaona haliendani na sifa za uzuri au utamu linazopewa?
 
Parachichi sijawahi kulielewa kwa kweli
Waliolijulia ukubwani wengi hawapendezwi nalo, ila ndo tunda langu pendwa.

Kwangu ni Fenesi, kuanzia harufu yake mbaya mpaka ladha yake kwangu ni kizungumkuti.
Naishia kushangaa watu wakilishambulia kwa wamachinga, wengine hudiriki kubeba kabisa akajinafi nyumbani.
 
hakuna tunda nisilokula katika yote ambayo mpka sasa nishawahi tia mdomoni..
Labda nikutane na tunda jipya ambalo sijawahi kula
 
Tango, nikiweka mdomoni badala ya kutafuna najikuta mate yamejaa.
 
Back
Top Bottom