Nilikuwa nikisikia sifa zinazopewa kwenye tunda linaitwa embe ng'ong'o nilikuwa natamani sana kulionja kwa kuwa huku kwetu kanda ya magharibi halipo na kama lipo mie sijwahi kukutana nalo.
Nikawa natamani sana kulionja, ila siku niliyolionja nikasema chaaa nini hiki, sitaki hata kulisikia tena na nalipa alama 1 kati ya 10
Wewe tunda gani unaona haliendani na sifa za uzuri au utamu linazopewa?
Waliolijulia ukubwani wengi hawapendezwi nalo, ila ndo tunda langu pendwa.
Kwangu ni Fenesi, kuanzia harufu yake mbaya mpaka ladha yake kwangu ni kizungumkuti.
Naishia kushangaa watu wakilishambulia kwa wamachinga, wengine hudiriki kubeba kabisa akajinafi nyumbani.