Uchaguzi 2020 Tundu Lissu achambua mifuko ya Jamii na fao la kujitoa, CCM jibuni hoja hizi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu achambua mifuko ya Jamii na fao la kujitoa, CCM jibuni hoja hizi

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Na: Mh Tundu Lissu

Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu. Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara. Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake.

Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja. Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja.

Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja. Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja. Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao.

Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa. Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.
 
Sasa shughuri ndokwaanza imeanza tunasubiri tuambiwe ripoti za CAG za miaka yote Mitano,tunataka tuambiwe matumizi ya Serikali yasasa yamepungua ama la ! Maana tulikuwa gizani kipindi chote Cha miaka5,tunataka kujua kwanini Deni linekuwa kwa Kasi nahuku tukiwa namakusanyo Bora kuliko awamu zote,pia tunataka tufahamu utekelezaji wa ilani yao ni kwakiasi gani wametekeleza? ili tupate kuona Kama tunaweza waamini tena TL tunaamini utatueleza yote huwenda wenye wajibu wakusema wasiseme,,
 
Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.
Tatizo la wafanykazi wa Tanzania ni midabwada, watu hopeless and stupid ! Kuna wale ambao wana ka upenyo ka kupata bakishishi/marupurupu kazini, haya ya mifuko hayawahusu, "wanafidia" huku wanakochota. Kundi la walimu (siyo wote tafadhali, ila wengi wao wako hivyo) ni kundi la academic failures ambao walipata Div 4 na hivyo kujiona "afadhali" wanapata hata hicho kidogo! WAMEGAWANYIKA katika makundi ya imani/itifaki mbali mbali. Mapolisi/wanajeshi ni academic failures, wao wanaona kama wamekuwa favoured na hiyo wanashukuru hata kidogo hicho wanachokipata, wanapata virushwa rushwa, wanaona ahueni. Kuwaunganisha siyo kazi rahisi! Wanahitaji mental liberation!
 
Wafanyakazi weni ni waoga wako kama digidigi polini,

Mwezi wa tatu huu nahangaika na haya mamifuko kazi yenyewe mkataba uliisha 2018.
Tukajiongeza na kujiajiri ila mambo yamebadilika na mifuko pesa ndio hizo kila siku sheria inasema sheria ..halafu hawafatilii michango kwa waajiri sijui wanakula mlungula.

Kiukweli huu utofauti wa wenzetu miaka mitano tu wanapata chao 240ml halafu sisi walala hoi milioni 2/3/4/5/10 unaambiwa usubiri au utafute kazi nyingine sijui hawaelewi kwamba wanatupandikizia chuki na uwekaji huu wa matabaka.

Kwenye hili mnyapaaa ameongea msumari haswaaa.
 
Back
Top Bottom