Tundu Lissu aelekeza mambo sita yanayopaswa kufanywa tunapoanza mwaka wa 61 wa Uhuru wa Tanganyika

Tundu Lissu aelekeza mambo sita yanayopaswa kufanywa tunapoanza mwaka wa 61 wa Uhuru wa Tanganyika

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Akitoa hotuba katika Miaka 60 ya Uhuru, Mhe Tundu lLisu amependekeza mambo yafuatayo kufikia au kuelekea kupata Uhuru wa kweli baada ya kupata Uhuru wa bendera.

1. Ni lazima tuakikishe kwamba, bila masharti yoyote wafungwa wote wa kisiasa wanakuwa huru kutoka mikononi mwa Mahakama na dola.

2. Lazima tuakikishe kwamba, bila masharti yoyote Uhuru wa vyama vyote kufanya siasa kwa mujibu wa Sheria unarejea katika Taifa letu.

3. Lazima tuakikishe kwamba, bila masharti yoyote tunafufua mchakato wa Kupata Katiba mpya itakayotoa haki Kwa wote.

4. Lazima tuakikishe kwamba tunakuwa na tume huru ya UCHAGUZI

5. Tunapigania Uhuru wa vyombo vya habari viweze kutenda haki Kwa wananchi

6. Lazima tuakikishe tunajenga Taifa lililoshikamana na lisiyoyumba Kwa mpishano wa hoja za kisiasa. Tuzingatie kwamba hakuna binadamu mwenye haki yakuondoa haki ya kuishi na kutoa maoni.
 
Kupitia TUME HURU YA UCHAGUZI ndipo tunaweza pata wawakilishi wa kweli wa wananchi, wawakilishi ambao watakuwepo kwaajili ya wananchi na hatimae kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Ujingaujinga tunaoufanya waafrika ni ndio mtaji mkubwa wa mataifa ya ulaya na marekani kuendelea kuzinyonya nchi zetu.

Tukitawala vibaya tunasababisha migogolo ambayo kwayo watu wa ulaya+ USA hutumia kutunyonya.

Kimsingi Afrika hatuna wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa ubinafisi wetu uliokithiri.
 
Katika muda uliosalia kati ya sasa hadi 2025, ni bora CHADEMA na vyama vingine vya upinzani waelekeze nguvu zao zote kwenye uchaguzi kuliko kufikiria mambo mengine kama Katiba, ambayo kwa vyovyote CCM hawako tayari kushughulikia katiba.

Wafanye juhudi kila iwezekanavyo, tume huru ya uchaguzi ipatikane kusimamia uchaguzi huo wa 2025.
 
Back
Top Bottom