Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Kila siku najisema wazi mimi ni MwanaCCM na sidanganyi lakini. Pia nakubali JPM anafanya vizuri ndiyoooooo (lakini ni kwenye jambo moja tu may be macro economics) lakini kuna mambo ameharibu sana (kuminya demokrasia, nepotism, rushwa kwa wapendwa wake imekithiri, wafanyakazi ndiyo nyang'anyng'a usiseme kabisa, kulinda uovu fulani, ubabe, kutozuia au hata kukemea tu mauaji yanayofanywa na wasiojulikana, kutotia neno TL alipopigwa risasi, kufunga gerezani wapinzani, kuharibu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, n.k). Kwa hakika ameharibu sana sana hapo.
Sasa jana Mnyika kanikosha, tena kanikosha sana. Iwapo Tundu Lisu atatia nia mara moja atabadilisha upepo wa kisiasa nchini ingawa najua fika atakapofika tu watamkamata. Wakimkamata hapo sasa ndiyo mzimu George Floyd utaanza Tanzania. Ni MCCM lkn sitaogopa kitu, nitaomba Mungu TL awe ndani mpaka siku ya kura. Tutampigia Kampeni akiwa ndani. Hatutaogopa Mapolisi - hatutaogopa virungu vyao na wala risasi zao.
Moja ya slogan ya Kampeni itakuwa ni kumwachia Rais wetu awe huru. Najua uongozi wa sasa hautakuwa tayari kumwachia Lisu kwa namana yeyote ile na hapo itakuwa ni kama Mungu katusikia maombi yetu kwa sababu hilo watakalofanya ndilo litakalowapotezea kura.
Serikali hii sio tu kuwa ni ya kibabe lakini pia haina hata upendo na watu wake kwa sababu sikio lao linataka nyimbo tamu tu na hawataki kukosolewa. Juzi nimeacha kubeaba kadi yangu ya CCM lkn sasa kama Tundu Lisu akija na akawekewa vikwazo ndipo nitaichoma kabisa kadi hiyo.
Agosti sio mbali - imebaki miezi miwili tu. CHADEMA nawaomba pls pls watia nia waruhusiwe wajiseme hadharani na mfuate utaratibu kama mlivyoweka. Jitahidi msitoe Mgombea nje ya Chama this time. Tunamtaka Tundu Lissu. Hata huku huku CCM baadhi tunanyanyasika. Tena tunanyanyasika sana. Tumewachoka hawa wagawana Tausi wa Ikulu.
Tunataka mabadiliko ili wananchi na wafanyakazi wa kawaida mafurahie uhuru wa nchi yao. Midege na mitreni ya mwendo kasi sio ugali. Mi fly ova ya Ubungo sio pembejeo za kilimo za Idukilo. Mivyeo inayotolewa kwa wanajeshi sio nyongeza ya mishahara kwa wafanyazi wengine.
Tunamtaka Tundu Lissu nchi hii ibadilike. Tumechoka kunyimwa hewa ya kukosa demokrasia. We can't breath!