Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini, anatarajiwa kuhitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wa utetezi wake, yaani ushahidi mkuu, ikiwa ni siku ya tatu katika mfululizo wa utetezi wake.

TUNDU LISSU .jpg

Leo Jumatano, Agosti 26, 2026, Lissu anatarajiwa kuhitimisha kwa kuangazia ushahidi wa upande wa mashtaka, kwa kuuchambua anachokiita udhaifu wake kuishawishi mahakama kuwa haukuweza kuthibitisha shtaka linalomkabili kwa kiwango kinachotakiwa kisheria, yaani bila kuacha mashaka yoyote.

Hatua hiyo itahitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wake, yaani ushahidi mkuu, na kuingia sehemu ya pili ya ushahidi wake, yaani ushahidi wa nyongeza (cross examination).

Katika hatua hii, atahojiwa na waendesha mashtaka maswali mbalimbali ya dodoso kuhusiana na ushahidi wake wa msingi.

Lissu anakabiliwa na kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, Dunstan Ndunguru akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

1787727679755.png

Updates za Mahakamani

Dada wa Tundu Lissu akiongoza maombi muda huu mahakamani kabla ya Kesi kuanza.


Tundu Lissu ameingia ndani ya chumba cha Mahakama na kama kawaida Watu wanaimba Lissu siyo Muhaini baada ya muda mfupi akaongea na John Heche kwa kumwagiza ongeza Moto wameanza kutoana maini.

UPDATES KUTOKA MAHAKAMANI, KESI YA UHAINI - SEHEMU YA 277

Anasimama karani Criminal session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Lissu.

Anasimama Ajuaye Zengeli wakili wa serikali yupo na Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri na Lissu yupo anajiwakilisha mwenyewe.

Waheshimiwa majaji na mimi niko tayari anajibu Lissu. Na mashahidi wangu wako humu naomba watoke ila wasikae mbali.

Majaji wanateta na kucheka kidogo. Makamu Heche, Mnyika, Golugwa na Brenda wanatoka zao nje.

Watu wanajiset kwenye viti vyao hapo wanakaaa.

Majaji wanateta kidogo kisha wanasema tuendeleee.

Mhe. Lissu anasema haitakuwa vibaya mkinikumbusha nilipoishia.

Jaji Ndunguru pale ulipomtaja Askofu Pissa.

Mhe. Lissu sasa leo nataka nijikite kwenye kesi kama ilivyowasilishwa kwenu na Upande wa Mashitaka. Ushahidi wao walivyouleta, Waheshimiwa Majaji naomba niseme utangulizi ufuatao:

1. Mashahidi walioletwa mbele yenu ni mashahidi wa aina gani na ushahidi wao unapaswa upewe uzito wa aina gani?

2. La pili nitazungumzia ushahidi wenyewe. Ushahidi uliotolewa na mashahidi hawa. Na nitaonesha hakuna kosa la Uhaini na hakuna kosa lolote la jinai kwahiyo hayo ndo mawili ya utangulizi.

Sasa nianze na la kwanza kuhusu hao mashahidi.

Wakati wa Preliminary hearing upande wa mashitaka ulileta orodha ya mashahidi 30. Ambao walisema hao ndio wataleta ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za uhaini dhidi yangu.

Upande wa mashitaka haukuleta mashahidi wote hao 30 badala yake walileta mashahidi 17 peke yake.

Hao 13 ambao hawakuletwa, hawakuletwa kwasababu muhimu fulani na nitazisema.

Hiyo ommission ya hao mashahidi 13 is neither insignificant nore without importance.

Sio kwasababu hawana maana na sio kwasababu hawana umuhimu.

Nianze na ambao waliletwa.

Katika mashahidi 17 walioletwa. Mashahidi 8 ni askari Polisi.

Mashahidi 9 waliobaki ni mashahidi wa kificho.

Mahakama haiwafahamu majina yao. Haiwafahamu kabisa, haifahamu wanaishi wapi? Haifahamu wanafanya kazi gani na haifahamu chochote zaidi ya majina ya P, P1, P2 P nini huko.

Inaweza kuwa tumekuwa nao throughout hapa kesi ikiwa inaendelea kwasababu Mahakama haiwajui na upande wa utetezi hauwajui hata kidogo.

Kwahiyo ushahidi wa hao mashahidi 9 ni ushahidi wa watu wasiojulikana na Mahakama wala utetezi, Watu pekeee wanaowajua ni waendesha mashitaka waliowaleta.

SEHEMU YA 278

Inawezekana mashahidi hao wa siri ni Mapolisi au mtu yeyote, hao ndio mashahidi wa kesi ya Uhaini.

Mashahidi 8 ambao ni Mapolisi hao ni mashahidi wa Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Camilius Wambura na DCI Ramadhani Kingai ambao nimeonesha kuwa nina ugomvi nao wa zaidi ya miongo miwili.

Person vendetta dhidi yangu, Hii vendetta ni neno la kiitaliano lenye maana ya Chuki.
Hawa watu wamekuwa na chuki dhidi yangu ndio wameleta hao mashahidi waje kunitolea ushahidi wa uhaini.

Waheshimiwa Majaji ushahidi wa Shahidi Na. 1 na Na. 16 PW1 na PW 16, ni ushahidi muhimu sana.

Sio kwamba una uzito lakini ni muhimu unaonesha aina ya ushahidi ulioletwa.

PW 1 George Bagyemu (ukisikia PW jua ni Prosecution Witness) alisema kwenye ushahidi wake kwamba, Yeye ndie aliyeongoza timu ya wapelelezi wa kesi hii kati ya Tarehe 04 April na Tarehe 08 April, 2025.

PW1 kwa maneno mengine alikuwa anaongoza upelelezi siku moja kabla sijakamatwa.

PW1 alisema kwenye ushahidi wake in chief na kwenye cross examination kwamba wakati anaongoza timu ya upelelezi kuanzia hiyo Tarehe and 04 alikuwa anawasiliana moja kwa moja na DCI Kingai kwa kupitia Ramadhani Ng'azi Deputy Commissioner of Police.

Kwenye Cross Examination nilimuuliza kama aliwahi kuwasiliana hata mara moja na ZCO ambae ni Boss wake akasema hapana.

Akasema pia hajawahi kuwasiliana na office ya DPP kwasababu huyu ndie anaratibu upelelezi wa jinai akasema HAPANA.

Nilimuuliza kama amewasiliana Regional security officer amewahi kuwasiliana nae? Akasema Hapana. Kwamba mkuu wa usalama wa mkoa alisena hajafanya hivyo.

Mtu aliyekubali aliwasiliana nae ni DCI Ramadhani Kingai kupitia kwa DCP Ramadhani Ng'anzi.

PW1 alisema aliunda timu tatu za Upelelezi. Ambazo ni 1. Operesheni, 2 inteligentsia na 3. ushauri.

Kwenye hizo timu 3 timu ninayotaka kuitolea ushahidi ni timu Oparesheni ambayo alisema ilihusika na ukamataji. Nilimuuliza ni wewe ndio uliyeamuru nikamatwe akasema Hapana yani Kiongozi mkuu wa upelelezi hafahamu nani aliyeamuru nikamatwe.

Ilikuwaje nikakamatwa? Akajibu kuwa alipigiwa simu na DCP Ng'anzi kuwa mtuhumiwa amekamatwa Mbinga na analetwa Dar es salaaam.

Kumbuka yeye anasema ndie mpelelezi mkuu wakati huo, sasa Waheshimiwa Majaji huyo aliyetoa taarifa kuwa nimekamatwa ni yule ambae alikuwa ni kiunganishi kati yake na DCI Kingai na presumably na IGP Wambura.

Sasa ni ushahidi wangu kuwa nilikamatwa kwa amri ya KINGAI DCI na Presumably na IGP Wambura ndio walioamuru nikamatwe na ndio walitengeneza kesi sio hawa hapa anamuonesha Katuga.

Na hawa akina Kingai miaka 24 iliyopita wamekuwa kwenye Mkakati wa Kunifunga. Wameshindwa siku zote. Waheshimiwa Majaji hayo aliyoysema PW 1 yalithibitishwa substantially 16 aliyathibitisha ACP Amin Mahamba.

Mashahidi wengine ni PW2, PW 3, PW 6, PW 9, PW 12 na PW 15. Ushahidi wao kwa ujumla wao ni ushahidi wa watu wa Ramadhani Kingai na Camilius Wambura.

Maafisa wa Polisi ambao wakubwa wao wamekuwa na mkakati wa kunifunga kwa miaka 24. Mtakapofanya majumuisho ya ushahidi huu na wa namna hii hauna thamani yoyote.

Ni ushahidi wa mashahidi wenye maslahi unahitaji kuwa corroborated na ushahidi huru.

Nataka kusema ndio ushahidi tulionao na nitaileta baadae.

Sasa nizungumzie ushahidi wa mashahidi wasiokuwa Polisi. PW4, PW 5, PW7, PW 8, PW 10, PW 11, PW13 na PW 14. Hawa ndio mashahidi ambao hakuna anayewajua isipokuwa prosecutor.

Mashahidi wote hawa tuna maelezo yao ya maandishi na maelezo yao ya midomo wakiwa hapa Mahakamani. Isipokuwa PW 1 ndio hatuna ushahidi wake wa maandishi ila wengine wote tunao.

Sasa nirudi kwa mashahidi wa kificho ukimwachia PW 4 wengine wote 7 walisema hivi kwa maandishi na wakiwa kizimbani hapa.

SEHEMU YA 279

Mhe. Lissu anaendelea kutoa utetezi wake.

1. Walipanga njama za kufanya uhalifu wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka jana. Wote walisema hivyo kwa maandishi hawa mashahidi wa siri na maelezo hayo yaliandikwa Polisi. (Kupiga watu, kuchoma vitu) ni wao walisema hayo. Na ushahidi huo uko hapo mko nao.

2. Wote hao isipokuwa PW4 walikamatwa na Polisi kwa kufanya njama hizo kwa kufanya fujo na wote walikamatwa kwa hizo siku nne yaani Tarehe 04 na Tarehe 08 April. Polisi waliwajua na kuwakamata wote within four days.

3. Mashahidi wote hao baada ya kukamatwa na Polisi wali confess. Walikiri kuwa tunapanga kufanya vurugu kwenye Uchaguzi, wakiwa kizimbani walisema kwamba walipanga kufanya uhalifu tena walikiri hivyo kwa maandishi

4. Mashahidi ambao walikamatwa kama watuhumiwa wote waliachiwa ili waendeleee kupanga njama yani unamkamata mtu kwa uhalifu na unamuachia.

5. Wote waliitwa na Polisi PW 16 Amin Mahamba na kuwambia kubalini kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu na mkikubali tutawafutia mashitaka.

Wahalifu wamekiri mbele ya Polisi, Wakaachiwa na kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu.

6. Wahalifu hao self confessed walitoka Dar es salaam na Dar es salaam Oktoba walikufa watu 182 kwa mujibu wa Jaji Chande.

PW 10 and PW 11 Walitoka Arusha na Arusha walikufa watu 53 kwa mujibu wa Jaji Chande. PW13 na PW 14 walitokea Mbeya na huko waliuawa watu 80 kwa mujibu wa Jaji CHANDE. (Polisi walikamata watu waliosema wamepanga kufanya uhalifu Oktoba na wakawaachia na hiyo Oktoba ukatokea huo uhalifu watu hao wakiwa uraiani.) Pw 5 na Pw 7 walitokea Songea na Jaji Chande anasema huko nako walikufa watu ila hawakutaja idadi ya waliokufa Songea.

PW 16 Amin Mahamba alisema alikuwa kwenye timu ya wapelelezi walioyachunguza mauaji ya Oktoba 29 na nikamuuliza hao waliosema walipanga kufanya fujo Je mliwachukulia hatua yoyote kwasababu machafuko yalitokea? Akajibu kuwa HAPANA, hakuna hatua walichukua.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa wahalifu wa aina hii una uzito gani KISHERIA?
Huu ndio ushahidi wa Serikali dhidi yangu.

Ushahidi wa wahalifu waliokiri tutafanya uhalifu wakaja Mahakamani wakakiri. Wakarudi walikokuwa wanapanga na baadae watu wakauwawa wengi huko mitaani. Ushahidi wa aina hii una uzito gani kwenye kesi ya uhaini?

Mashahidi wa aina hii ni totally unreliable. Nitaleta kwa maandishi hoja hizo za kisheria.

Waheshimiwa Majaji shitaka linasema nilitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nikathibitisha nia hiyo kwa kutamka yale maneno maarufu.

Sasa Waheshimiwa Majaji kuhusiana na shitaka hili na kwa mujibu wa maamuzi ya kisheria tuliyozungumza sana kitu cha muhimu ni uwepo wa nia ya kutenda kosa la uhaini.

Ushahidi wa Jamhuri unasemaje kuhusu hiyo nia ya kutenda kosa la uhaini? Mashahidi waliotoa ushahidi kuthibitisha hoja hii ni hawa wafuatao.

PW1, PW2, PW16 na PW17 ambae ni P yule mwandishi kwa ridhaa yenu naomba nipatiwe exhibit D1, D15 na D16.

Kimya kidogo kinapita.

Majaji wanaandika na hizo exhibit zinatafutwa.

Ushahidi wa PW 1 George Bagyemu Msaidizi wa Mafwele kuhusiana na nia ya kutenda kosa la uhaini inayodaiwa katika hati ya mashitaka kwenye ushahidi wake alisema kwamba mimi nilitengeneza nia ya kuitishia serikali.

Aliona nia ya kutenda kosa la uhaini katika kauli niliyotoa. Nia aliiona kwenye maneno yeye.

Waheshimiwa Majaji shahidi mwingine aliyeona nia hiyo ni PW 16 Amin Mahamba. Waheshimiwa Majaji Exhibit D15 maelezo yake Polisi alisema huyu Mahamba akasema hivi

"Mimi pamoja na timu nzima ya upelelezi tuliitizama na kuiskiliza video hiyo tukabaini kuna kosa la uhaini na kuchapisha taarifa za uongo."

SEHEMU YA 280

Anasimama Wakili wa Serikali Katuga anasema huu ni utetezi na kielelezo hivyo kilipokelewa kama kielelezo D.

Kinapokelewa kuonesha contradiction na kuanza kukirejea kama kielelezo cha kawaida. Kitakuwa na kinyume cha kifungu cha 163 kipo for specific purpose na mkiruhusu tutakitumia dhidi yake. Kitakula pande zote mbili, tunaiomba Mahakama irudi kwenye hiyo purpose ya kukipokea hicho kielelezo.

Lissu anasema sasa mimi niseme kuwa kwao kama ni furaha mimi kukitumia nataka iwe furaha.

Mimi sina shida na wao wayatumie tu, Kielelezo kinahusu kesi hii na Mahakama lazima ikisome ikiangalie.
Hamna kielelezo kinachukuliwa kwa ajili ya cross tu peke yake, Waheshimiwa nakitumia kwa sababu kinahusu kesi.

Sasa kwa vile wamesema ni furaha yao nashangaa kwanini wanalalamika. Mimi nilikiingiza makusudi ili na wao wakitumie, nashangaa tena hawataki.

Jaji Ndunguru anasema kwa vile kielelezo kimeingia hatuwezi kusema tunazuia matumizi ya hicho kilelezo. Kwahiyo wewe endelea tu, kilelezo tayari kipo Mahakamani we kitumie.

Lissu anasema sawa naendelea.

Amin Mahamba amesema kuwa mimi pamoja na timu tulitazama video na kuona makosa ya uhaini na kusambaza taarifa za uongo.

Kwahiyo PW 16 aliona nia ya kutenda kosa akiwa na PW 1 hawa waliona nia.

PW2 na PW 17 Je waliona nia?

Waheshimiwa Majaji kwa mujibu wa kielelezo D1 John Kaaya anasema katika picha mjongeo niliona Tundu Lissu akitamka matamshi yenye viashiria vya jinai.

Hakuna mahali kokote alipozungumzia uhaini, kosa la uhaini na nia ya uhaini.

Aliona viashiria vya jinai.

PW 17 anasema kwenye maelezo yake anasema hivi. Katika mkutano huo masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni masuala kuhusu Uchaguzi Mkuu na agenda yao ya No reforms, No election na matatizo yao wanayokumbana nayo kwenye Uchaguzi. Huyu yeye hakuna uhaini aliouona hata mmoja.

Anasema alituona tunazungumzia No Reforms No Election na Matatizo tunayokumbana nayo, hakuna uhaini aliousema kabisa.

PW 17 ndie shahidi pekee aliyekuwepo kwenye mkutano na hakuona kosa lolote wala uhaini.

Hoja ya pili inayogombaniwa kwenye kesi hii ni manifestation ya hiyo nia. Maneno ni haya wanasema kitu kimoja hapa, msimamo huu unaashiria uasi ........ anayasoma yote.

Yanayodaiwa kusemwa ndio maneno hayo.

Sasa ushahidi unasemaje kuhusu haya maneno?

Kuhusiana na hayo maneno, ushahidi wa PW1, PW2 na PW 16 unafanana na mashahidi wote hao wanasema kuwa waliona hiyo video yenye maneno hayo.

Na ushahidi wao wamesema mimi ndie niliyechapisha na kuyapeleka Jambo TV. Ushahidi wa PW 17 the eye witness unasemaje?

Shahidi Na. 17 wa upande wa mashitaka kwenye maelezo yake D16 anasema hivi katika mkutano huo masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni kuhusu uchaguzi mkuu na mambo ya No Reforms No Election.

Hakuna kokote kwenye D15, hakuyaona hayo maneno hakuyasikia, hajayaandika wala hajayasema hapa. Aliyekuwepo hajayaona, hajayasikia kwasababu hajayaandika na hajayasema.

Angeyasikia angesema, angeyaona angeyaandika.

PW17 alisema hapa Mahakamani na iko kwenye D16 kwamba yeye ndio alipiga picha na kurusha akiwa na wenzake wanne wakitumia camera za SON. Wote ni wafanyakazi wa JAMBO TV. Walirusha mkutano huo ukiwa Live.

PW17 alisema kwa maandishi na hapa Mahakamani pia kuwa yeye ndie aliyehifadhi hizo video kwenye mtandao wa Jambo kule Youtube, X na instagram. Alisema yeye sio mimi.

Sehemu ya 281

Lissu anaendelea na kutoa utetezi wake.

Kwahiyo wenye element ya publication ushahidi ulioletwa na upande wa mashitaka ndo huo.

Mashahidi ambao hawakuwepo walisema maneno yalisemwa na ambae alikuwepo hakuna anaposema maneno yalisemwa.

Aliyekuwepo anakiri publication alifanya yeye. Usambazaji ni wakwake na sio mtu mwingine.

PW 17 aliulizwa wewe ulisikia kauli yoyote ya Kijinai? Akasema HAPANA.

Nilimuuliza ulisikia kauli yoyote ya kihaini? jibu lake ni HAPANA.

Ushahidi wangu juu ya hiyo publication na intention ni ushahidi wangu mashahidi waliokuja na kusema nimetenda kosa wanajichanganya wanasema mambo tofauti wao wenyewe.

Sasa Waheshimiwa Majaji huu Mkanganyiko kati ya maneno yalisemwa au hayakusemwa. Kulikuwa na nia au hakukuwa na nia? Kitu gani kilizungumzwa au hakikuzungumzwa, kungekuwa na video yenyewe tungeweza kutatua huo mgogoro.

Wajibu wa kuleta hiyo video ulikuwa ni wajibu wa upande wa mashitaka hawakuleta hiyo video.

Mahakama haitakaaa ijue yote yanayosemwa yapo kwenye video ni ya kweli au ni uongo tu.

Proof ni video sio maneno na hiyo video haipo. Wao wamechomoa vimaneno viwili vitatu wanataka kusema ni uhaini halafu wameacha maneno yote.

Walisema wataleta vielelezo 11, walisema wataleta vingine 9 na visivyokuwa vya maandishi wataleta viwili. Hawajaleta hata kimoja. Sio vya maandishi wale hivyo physical ni maneno matupu, na maneno matupu hayavunji mfupa.

Na kwenye uhaini mere words do not constitute overt act. Maneno maneno hayatengenezi uhaini. Khatibu Gandi someni nyie hiyo kesi. Mnafanya nini kwenye ofisi za serikali halafu mnajiita mawakili?

Waheshimiwa Majaji kuna vitendo vya ukiukwaji wa taratibu wakati wananikamata na upelelezi wa hili shauri.

1. Ni sheria kwamba National Prosecution Act kwamba Mkurugenzi wa mashitaka wao ndo wanacoordinate criminal investigation.

Katuga anasema kwa hatua ya sasa asiingie kwenye sheria huko.

Lissu anasema mimi nilikuwa nafanya foundation ya ushahidi wangu tu ninaotaka kutoa.

Jaji Ndunguru haya endelea sasa,
Tumeelewana nenda direct sasa.

Mhe. Lissu Ushahidi Na. 1 na 16 niliwauliza hivi, DPP ndie aliyeratibu huu upelelezi majibu ni hapana.

Wakaulizwa tena mwakilishi wa DPP alikuwepo kwenye timu ya upelelezi wakasema hapana lakini PW 16 Akasema alikuwepo mwenye jina la kibantu mmoja.

Kwahiyo upelelezi haukumshirikisha DPP.

Waheshimiwa Majaji Shahidi Na. 01, 02 na 16 Yaani George, Kaaya na Mahamba waliulizwa kwamba mnatambua kwenye PGO mmeamuliwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kutoa maoni na kufanya mikusanyiko wakaulizwa waoneshe kama walizingatia haki za mtuhumiwa?

Niliwaambiwa waoneshe haki zangu kwenye maelezo yao na ushahidi wao hawakuwa na lakusema kuhusu namna walivyolinda haki zangu.

Sehemu ya 282

Anasema hawa PW1, 2 na 16 niliwaonesha vifungu vya kanuni ya adhabu na sheria ya vyombo vya habari kuhusu sio uchochezi wala sio kosa kuonesha mapungufu ya serikali na kuipinga serikali na wao walikiri na kusema ndio sio makosa. Nilifanya kazi hiyo na wao walikiri kuwa sio makosa.

Nikwaambia ni wapi walizingatia vifungu hivyo wakati wa upelelezi wao wakasema hawana na lakusema kuhusu mambo hayo.

PGO 1 (24) nguzo kuu ni presumption of inocence niliwauliza walinitreat wapi kwamba sina hatia wakati wote waliokaa na mimi? Hakuna walipozingatia hilo kabisa. Walikuwa wanajiendea tu. Walishaniona nina tuhuma tayari na muhaini.

Tar. 04/04 ndio waliona video yaani PW1 na PW 2 yaani PW 1 alimpelekea PW 2 akamuonesha vipande vipande. Na siku hiyo hiyo akaamuru kuonesha jalada lifunguliwe. Akaaamuru jalada lifunguliwe.

Kwahiyo hakukuwa na presumption of innocence kwamba Lissu ametenda uhaini siku hiyo hiyo waliamua hivyo.

PW 16 Amin Mahamba anasema na yeye alipotizama akaona uhaini hakukuwa na presumption of innocence ndio maana hawakutaka kupata ushauri wa DPP wala washauri wa kisheria wa Serikali.

Na kwa vile walikuwa na Majibu tayari ndio maana waliulizwa mliwatafuta Viongozi wa Chadema muwaulize? Wakajibu HAPANA.

Je mlinitafuta Mimi Lissu mwenyewe mniulize nilikuwa na maana gani? Wakasema HAPANA.

Kwahiyo nasema kwamba hawakunitafuta kwasababu walishaona tayari wana mkosaji.

Ndio maana hata walipoletewa na ushahidi wa PW 17 yule wa JAMBO. Yeye anasema ndie aliyechapisha na kusambaza na hakuona uhaini. Maelezo ya P hayakuwa na maana tena kwao.

Wao majibu yao walikuwa nayo kabisa.

Nilimuuliza Amin Mahamba kuwa Insp. Andrew Churu ulisoma maelezo yake aliyosema kuwa ni P ndio alichapisha na kusambaza? Huyu Amin Mahamba hakuna na lakusema kwasababu walifanya kazi hii wakiamini mimi ni muhaini kabla ya lolote.

Pia, niliwauliza juu ya matakwa ya PGO No. 1 (25) inayowaambia kuwa makosa ni yale yaliyopo kwenye sheria na sio vinginevyo.

Wakajibu ni kweli. Nikawauliza someni kifungu nilichoshitakiwa nacho kuhusu kosa nikiloshtakiwa nalo kama kwenye hicho kifungu kuna habari ya kuzuia uchaguzi, kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi nayo? Ibara ya 151(1) kuhusu serikali kwamba niliitishia serikali kweli?

Yote hayo wakasema hawajui na hakuna kosa nimelifanya kwenye hayo. Wakasema hakuna nilichofanya kuitishia serikali.

Yuko speed majaji wanasema unaenda kasi sana tunashindwa kuandika.

Ni ushahidi wangu kwamba hiyo Executive wanayosema niliitishia yaani serikali maana yake nilimtishia Rais, Vice President, Ministers na Deputy Ministers, Inaweza kuwa RC na Ma DC hao wote ni Executive. Wakurugenzi wa Wilaya na manispaa wanaitwa District Executive Directors (DED) hata majina yao wanaitwa Executive.

Exevutive of the United Republic wanaweza kuwa ma VEO au WEO yaani Village Executive officer na Ward Executive Officer wote hao ni Executive.

Na Executive wanaweza kuwa watu wowote waajiriwa wa serikali isipokuwa Mahakama na Bunge. Kwahiyo kifungu cha 39(2) cha Penal Code hakitekelezeki hakuna atakayepona na hawawezi kuithibitisha.

Kwamba hawajasema kati ya hao kuanzia Rais hadi mtendaji wa kijiji na mtaaa ambao wote ni Serikali nilimtisha nani kati yao? Kifungu hicho kilichotungwa wakati wa Grey Likungu Mataka wakati wa utawala wa Chama kimoja hakifai tena kuwa sehemu ya sheria zetu.

Waheshimiwa majaji hakuna shahidi hata mmoja amesema nia yangu ya kuitishia serikali ilitekelezeka hata mmoja.

Hakuna aliyesema kuwa serikali iliogopa sana siku hiyo. Hakuna aliyesema IKULU HAKUKUKALIKA siku hiyo.

Sehemu ya 283

Wote wameongeza mambo kwa mdomo ambayo kwenye maandishi hayapo kabisa. Wameongeza yasiyokuwemo kwenye maelezo yao.

Ni ushahidi wangu kwamba ushahidi wa maneno unaotofautiana na ushahidi wa maandishi kwenye jambo hilo hilo ni ushahidi usioaminika.

Ndio kusema ushahidi wote wa mashahidi wote wa upande wa mashitaka hauaminiki.

PW1,2,3,6,9,12 and 16 hawa wote ni mapolisi na waliandika maelezo polisi wenyewe na wakajikanya wenyewe na kujishuhudia wenyewe. Niliwauliza ni sheria gani iliwaruhusu wafanye hivi wakadai ndivyo huwa wanafanya mapolisi.

Sasa ni ushahidi wangu kuwa Mapolisi wanafanya mambo kienyeji na vielelezo D1,2,5,8,12 wote walijaindika ni polisi mmoja tu ndio aliandikwa na polisi mwenzake kwa mashahidi wote walioletwa na Jamhuri.

Waheshimiwa Majaji wale Mapolisi wa Ruvuma waliandikwa na mapolisi wengine lakini hawakuletwa. Wangewaleta njngewathibitishia kuwa maelezo yao yaliandikwa kwa usahihi.

Kwahiyo ushahidi wangu ni huo. Nimemaliza ingawa nimevuta vuta kidogo. Majaji wanaandika.

Jaji Ndunguru: Sasa hawa ambao hawajaletwa mahakamani unasemaje sasa?

Mhe. Lissu : Wangeletwa tungethibitisha taratibu za kuandika maelezo huwa ukoje. Kwahiyo ni ushahidi unreliable huu unatakiwa kwa kesi kubwa kama hii.

Ajuaye Wakili wa Serikali anasema tunaomba health break kabla ya kuanza cross exanination.

Tundu Lissu amemaliza utetezi wake, kesi imeahirishwa kwa saa moja na nusu ikitarajiwa kurejea tena saa 8 na nusu mchana ambapo Lissu atakabiliana na maswali ya dodoso na kama muda utatosha basi mashahidi wengine upande wa utetezi watatoa ushahidi wao.

KESI YA LISSU YAREJEA, WANACHADEMA WAJAZA MAHAKAMA

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu imerejea saa 8:30 mchana katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo upande wa Jamhuri utamfanyia dodoso shahidi wa kwanza, Tundu Lissu ambaye amesimama kujitetea.

Sehemu ya 284

Mwenyekiti Lissu alipata wasaa wa kuongea na Mawakili na mashahidi wake kwa muda wa nusu saa aliongea na Katibu Mkuu wa Chama John Mnyika, Amani Golugwa Naibu na Brenda Rupia.

Anasimama Ajuaye Zengeli amesema wako tayari kumuuliza maswali shahidi ambae ni Tundu Lissu. Wako tayari kuendelea.

Majaji wanaaandika andika hapa.

Mhe. Lissu amekaa zake pale kizimbani. Anaulizwa uko tayari kuulizwa tuanze maana bado uko chini ya kiapo pia.

Tutauliza maswali wote na ataanza Nasoro na baadae wengine:

Anasimama Katuga. Anasema Shahidi Pole na ushahidi mrefu.

Katuga: ulisema kuwa sisi ni ndugu zako?

Mhe. Lissu: Nilisema ndio.

Katuga: ni kitu cha kisheria na hakuna tofauti yoyote ya mimi na wewe?

Mhe. Lissu: Sawa.

Katuga: Wewe ni mwanasheria

Mhe. Lissu: Kweli

Katuga: Una ujuzi wa kisheria

Mhe. Lissu: Ni kweli

Katuga: Kama una kumbukumbu Tanzania ilipata uhuru mwaka gani?

Mhe. Lissu: Tar. 09 December 1961

Katuga: Ni nchi huru?

Mhe. Lissu: Ni nchi huru.

Katuga: Ni chombo gani kina mamlaka ya mwisho?

Mhe. Lissu: Mahakama ya Rufani.

Katuga: Naishia Kwenye Mahakama mimi.

Lissu: Hilo ni lako mimi langu ni Mahakama ya Rufani.

Katuga: Basi kwa mujibu wa ibara ya 108 inasemaje?

Lissu: Ndio ni Mahakama ya Tanzania.

Katuga: Kwahiyo Mahakama haipangiwi na mtu yeyote?

Lissu: Haipangiwi

Katuga: Wewe ni Mwenyekiti wa Chadema?

Lissu: Sahihi

Katuga: Je uliiambiwa mahakama hii kuwa mwenyekiti wa Chadema ni kinga kushtakiwa?

Lissu: Sijaiambia na sina kinga hiyo.

Katuga: ulisema sifa nyingi zinazokuhusu ambazo mimi sizipingi. Je hizo tuzo zilikuwa kwenye utaratibu gani?

Lissu: Zipo ambazo zina maandishi na zingine unapewa kitu kama kombe la Dunia hivi.

Katuga: Hebu wambie Majaji haya matuzo yote haya?

Lissu: sijaleta na sina wajibu

Katuga: Ukienda hivyo tutaenda siku saba.

Lissu: nimekaaa jela mwaka mzima nitaogopa week moja yako kweli?

Katuga: Sasa ulileta ushahidi wako huo wa tuzo.

Lissu: Sijaleta sio kazi yangu ni kazi yako wewe.

Katuga: Sasa usilete ujuaji.

Lissu: Mimi ni mjuaji kweli kweli. Unataka nisilete kivipi sasa?

Katuga: Kamati gani ilisema uachiwe?

Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya kimataifa

Katuga: Kuna sehemu yoyote umekanusha kuwa maneno yale ya kukinukisha, kuhamasisha uasi na sanasana .... umesema maneno hayo wameyatoa kwenye video yako. Je ulisema sio yako?

Lissu: Mimi nilisema mkitaka kuyaelewa sikiliza hotuba yote.

Katuga: Wewe ni kaka yangu siwezi kukuuliza lile swali la una akili au huna kama unavyowaulizaga watu

Lissu: Ukiona unaweza kusema nani amekukataza. Kama unaona sina akili sema tu au niulize nitakujibu.

Katuga: Haya maneno ni ya kwako au sio ya kwako?

Lissu: Hayo maneno sijawahi yakataa ni yakwangu sana.

Katuga: Historia pia umewahi kuisoma?

Lissu: Nimewahi.

Katuga: Waliwahi kuwalaghai babu zetu kihistoria hebu nikumbushe?

Lissu: Hawakulaghai waliingia nao mikataba.

Katuga: mikataba ya kilaghai ilikuwa?

Lissu: hiyo mikataba ilikuwa ya faida kwa hao viongozi wa kiafrika waliyoingia. Kwao waliiona ina faida.

Katuga: Si walikuwa wakoloni hao?

Lissu: Walikuwa wakoloni walioiumiza afrika kama ambavyo Samia ameiumiza nchi sasahivi.

Katuga: Wewe ni mtetezi wa mali za umma. Unakumbuka ulisemaje kuhusu makinikia. Ulisema hayatoki?

Lissu: Huna unachojua kama unataka niulize nitakwambia nilivyosema

Katuga: Si ulisema Tanzania ilishitakiwa je ilishitakiwa kweli mbona mimi sijui kama ilishitakiwa?

Lissu: Nani kakwambia kuwa kwenye international abitration imeshitakiwa unataka nikupeleke nitafanya hivyo hakuna shida.

Katuga: Kama nilikusikia wewe ni mtaalamu wa Sheria za Uchaguzi?

Lissu: Ni kweli

Katuga: Tanzania kupinga sheria fulani utaratibu wake ukoje?

Lissu: Uko namna nyingi? Mfano kupinga kwa njia ya maandamano kuhamaasisha wanachi waipinge hiyo sheria

Sehemu ya 285

Katuga: Usiende huko

Mhe. Lissu: Naenda kote tu, maandamano najua wewe unataka njia ya Mahakama.

Katuga: Sheria ya maandamano umetaja sheria yako?

Mhe. Lissu: Ibara ya 20(1) ya Katiba inasema tupinge kwa mikusanyiko na maandamano.

Jaji Taratibu jamani tafadhali. Naandika.

Mhe. Lissu: Haya mikutano ya hadhara imeruhusiwa kisheria.

Katuga: Haya nikupe usome?

Mhe. Lissu: Nipatie nisome. Anapatiwa Lissu na anasoma. Inaitwa freedom of association and assembly.

Katuga: unamfahamu Francis Dyanabo

Mhe. Lissu: Julius Ishengoma Francis Dyanabo namjua alienda Mahakamani kupinga sheria za uchaguzi

Katuga: Alishinda?

Jaji hebu rudia hapo kwa Dyanabo.

Mhe. Lissu: Namfahamu personally Julius Ishengoma Dyanabo personally kwasababu alifungua kesi za kupinga sheria ya uchaguzi kwamba kabla ya kufungua kesi ya uchaguzi unapaswa kuweka kiasi cha pesa.

Katuga: Kuhusu Mtikila na mgombea binafsi ilikuwaje?

Mhe. Lissu: Sasa usiniingilie nikujibu umekuja vizuri. Mtikila alishinda Mahakama kuu, Mahakama ya rufani ilitengua na baadae akaenda Mahakama ya afrika na wakasema huko kuwa Tanzania iruhusu mgombea binafsi. Hii serikali unayotumikia haijawahi kurekebisha hilo hadi leo.

Katuga: Sasa nakuuliza ulisema kifungu cha 39 cha Penal Code umesema mambo ya overt act kinasemaje kuhusu njia ngapi za manifestation.

Mhe. Lissu: Ziko mbili.

Katuga: Ipi na ipi?

Mhe. Lissu: Publication of a writing or printing na overt act or deed.

Katuga: inapotumika neno or inamaanisha haya maneno yanatumika in alternative?

Mhe. Lissu: yanaweza kufanana na yanaweza yasifanane. In this case yanafanana ni matendo.

Katuga: Kwahiyo similarities inamaanisha.
Kwamba yako similar. Kwahiyo kati ya neno or au and lipi lilipaswa kutumika.

Mhe. Lissu: Kwamba ingesomeka by overt act and overt act. Maana yake nini?

Katuga: Haya soma hapo.

Mhe. Lissu: Sasa hiki umenipa nini? Chukua haya makaratasi yako.

Katuga: Wewe ni Kaka angu umenitangulia kwenye taaluma si ungesoma eneo lenyewe kama nimekufunulia ukurasa tofauti.

Mhe. Lissu: Sio kazi yangu mimi ungefungua unapotaka wewe.

Katuga: Sasa soma kifungu cha 13 cha Intepretation Act

Mhe. Lissu: Anasoma.

Katuga: Kwahiyo tuamini nini?

Mhe. Lissu: Sheria haitungwi ili iwe absurd

Katuga: Ulisema kuna mambo yamekukuta kwenye mapambano yako? Nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ni mtu mwenye chuki dhidi ya serikali.

Mhe. Lissu: Nina chuki na serikali ya nchi hii kwasababu imeonea watu wengi.

Katuga: Kwahiyo ulisema yote hayo una chuki na serikali?

Mhe. Lissu: Nina chuki dhidi ya uonevu wa serikali. Ninayo chuki dhidi ya serikali sahihi kabisa. Wanaonea sana watu.

Katuga: Kama Mwanasiasa nia ya Chama cha siasa ni kushika dola?

Mhe. Lissu: Sio nia pekeee ni nia mojawapo.

Katuga: Tutakuwa hatumalizi.

Mhe. Lissu: Tutamaliza tu.

Katuga: mihimili mitatu ya dola ni ipi?

Mhe. Lissu: executive, Bunge na Mahakama.

Katuga: Kwenye sheria majukumu ya hii mihimili mitatu ni nini? Tuanze na Bunge?

Mhe. Lissu: Kutunga Sheria

Katuga: sasa mbona ulitaka kusema mengine

Mhe. Lissu: Sikutaka uishi kwenye ujinga wa kudhani kazi ya Bunge pekee ni kutunga sheria ziko nyingi sana.

Katuga: Kazi ya mahakama je?

Mhe. Lissu: Kutafsiri sheria na kutengua sheria.

Katuga: Jibu maswali yangu usinielimishe?

Mhe. Lissu: Wewe ndio umesema mimi ni kaka yako unataka nikuelimishe hutaki tena muda huu nikuelimishe?

Katuga: Kazi ya Serikali ni ipi?

Mhe. Lissu: Serikali inaisimamia sheria. Kwahiyo?

Katuga: Umenipa jibu?

Mhe Lissu: kwahiyo kama nimekupa jibu hivi nyie mnasoma sheria wapi?

Katuga: Turudi tena Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu. Pale kanuni ya adhabu iliposema mtu akitengeneza kitendo kwa nia ya kutishia serikali. Je tafsiri kuna takwa kuwa lazima iwe imetishika?

Sehemu ya 286

Mhe. Lissu: Hiyo Section haipo hiyo lakini kifungu cha 10(2) ipo.

Katuga: Tutakesha hapa.

Mhe. Lissu: Nimekaa mwaka na miezi mitano. Naogopaje kukesha hapa?

Katuga: Anacheka. Haya twende kwenye mapesi. Wametumwa na wambura na kingai ulisema hivyo?

Mhe. Lissu: Ndio nimesema hao akina Wambura kuwa wamenionea muda mrefu.

Katuga: Kwahiyo wametumwa si ndio? Umesikia au umejuaje?

Mhe. Lissu: Wamesema kwa maandishi wenyewe. Wameni persecute kwa muda mrefu sana. Waliaomuru nikamatwe na Kingai na Wambura. Wamesema kwasababu ya maandishi yaliyopo mahakamani.

Katuga: Umewataja kama mashahidi wako akina Wambura na Kingai?

Mhe. Lissu: ndio

Katuga: Kumbe ni wema?

Mhe. Lissu: Nimewaita waje waseme ukweli tu. Habari ya wema au sio wema ni mengine. Najua wewe huwezi kuwaleta. Wataletwa na Mahakama.

Katuga: Ulisema wakati unakamatwa?

Mhe. Lissu: Nilikamatwa. Wewe ambae hujawahi kukamatwa huwezi jua nilikamatwa au vipi?

Katuga: umejuaje?

Mhe. Lissu: Wewe unawafungulia watu makesi ya uongo utajuaje mambo ya kukamatwa.

Katuga: Ulisema waliokukamata hawajaja kwasababu wanaogopa kuja kusema ukweli?

Mhe. Lissu: Ndio

Katuga: Dhumuni la Preliminary hearing ni nini?

Mhe. Lissu: kupambanua maswala ambayo yanabishaniwa na ambayo hayabishaniwi.

Katuga: Wewe je ulifanyiwa hoja za awali?

Mhe. Lissu: Ndio nakumbuka.

Katuga: Unajua mambo ambayo hayabishaniwi hayatakiwi kuleta proof?

Mhe. Lissu: Sahihi.

Katuga: Je ukamataji haukuwa na ubishani?

Mhe. Lissu: Suala la nilikamatwa mbinga ndio lilikuwa halina ubishani lakini mengine yana ubishani.

Katuga: Kwakuwa halikubishaniwa. Wakati unawaambia waheshimiwa majaji kuwa hawakuletwa kwasababau maalumu ulikuwa unataka waje kufanya nini?

Mhe. Lissu: Lugano mwenyewe kwenye maelezo yake alisema kuhusu ukamataji ulikuwaje. Kukamatwa Mbinga sio inshu ila ilikiwa halali au la ni jambo lingine tofauti. Huwezi kutofautisha mambo madogo hivi?

Katuga: Unasema ulitoa hotuba kwa watia nia wa Chadema ile Tarehe 03/04 na ukasema ulitoa hotuba hii mbele ya waandishi wa habari?

Mhe. Lissu: Ni kweli kabisa.

Katuga: Je katika ushahidi wako wote kama umewaambia kuwa niliongea mbele ya waandishi wa habari kwamba wasizipeleke kwa umma?

Mhe, Lissu: Sikuwaambia kabisa. Niwaambie ili iweje sasa wakati nilitaka iende kwa umma.

Katuga: Ulitaka iende kwa wananchi?

Mhe. Lissu: Sana tena sana nilitaka iende. Ilikuwa ni habari muhimu sana.

Katuga: Ulitaka hotuba yako isambae kwa wananchi.

Mhe. Lissu: Ni kweli kabisa.

Katuga: Je ulisema ulitoa mipaka kuwa ulitoa mipaka?

Mhe. Lissu: Sikutoa mipaka.

Katuga: Ulisababisha au uliruhusu?

Mhe. Lissu: sikuruhusu mimi

Katuga: P17 alisema walifanya live streaming na kama maneno hayo ya tarehe 03/04 uliwapa prior yaani kabla?

Mhe. Lissu: Sikuwapa kwasababu sikuzungumza nao.

Katuga: Wangejuaje unaenda kuzungumza nini?

Mhe. Lissu: Unataka niseme walikuwa hawajui? Itakusaidia nini sasa? Ndio walikuwa hawajui nitaenda kuongea nini.

Katuga: Kwakuwa hawakuwa wanajua nitakuwa sahihi nikisema haya maneno kuwa tunaenda kukinukisha, tunaenda kuzuia uchaguzi. Walikuwa hawajui kabla?

Mhe. Lissu: Sahihi.

Katuga: Mashahidi wa Jamhuri walikuwa wanasema ulikuwa umevaa Kombati?

Mhe. Lissu: Walisema ndio.

Katuga: Kuna sehemu ulikanusha kuhusu utambuzi wa appearance yako siku hiyo uliyokuwa umevaa?

Mhe. Lissu: Nakanushaje vazi rasmi la Chama. Ni vazi langu.

Katuga: Kwahiyo ulivaa hivyo siku hiyo?

Mhe, Lissu: Sahihi kabisa.

Katuga: Nitakuwa sahihi mashahidi wa Jamhuri walikutambua kwa usahihi kwenye hiyo video kwa nguo hizo?

Mhe. Lissu: Mashahidi wa Jamhuri wananifahamu siku zote.

Katuga: Unajua una akili nyingi sasa nijibu tu swali

Mhe. Lissu: Kweli akili ninazo.

Katuga: Turudi kwenye masuala ya wanasheria sasa. Unaijua principle ya constructive possession unaifahamu?

Mhe. Lissu: Siifahamu labda niiambie.

Katuga: Kwamba mtu anaweza kukutwa na kitu ambacho hana lakini amekihifadhi kwa mtu fulani.

Mhe. Lissu: inawezekana ndio

Katuga: Unajua case laws unajua kitu kinaitwa constructive publication kwamba una knowledge na control?

Mhe. Lissu: Sasa mimi sikuwa na control ya publication hiyo ya Jambo.

Huyu KATUGA anapitia wakati mgumu sana. Majibu ya shahidi utadhani yeye ndio Wakili anamuuliza. Watu wanacheka

Katuga: Nani alisababisha publication?

Mhe. Lissu: Ni PW 17. Hakuna aliyemlazimisha kufanya publication. Angeweza kuamua asipublish.

Katuga: PW 17 alisema kwamba tulipaswa sisi kupitia wewe?

Mhe. Lissu: Sasa tatizo nyie Serikali mnasema nilipublish mimi wakati shahidi wenu alisema walipublish wao kupitia mimi. Huoni shida hapo wewe?

Naomba nikae mvua ya maswali ni kubwa. Watu wanacheka. Anakaa Mh. Lissu. Hajapoteza tabasamu lake lote.

Katuga: Ukitoa hotuba kila mtu ana haki ya kuitafsiri anavyoona mwenyewe?

Mhe. Lissu: Kweli.

Katuga: Maneno kwamba tutazuia uchaguzi, kila mtu ana haki ya kuzuia kwa kadri atakavyoona? Kuvuruga uchaguzi si kila mtu atavuruga anavyoona yeye inafaaa?

Mhe. Lissu: Kila mmoja abebe mzigo wake. Sio kazi yangu.

Katuga: Unakumbuka P3 alivyosema.

Mhe. Lissu: P3 ni nani wewe sema ni PW ngapi huyo P3 wako?

Katuga: PW 13 unakumbuka anasema walipanga kurushia watu mawe na kuzuia uchaguzi

Mhe. Lissu: Alisema ndio hayo ni yake.

Katuga: Uchaguzi upo kisheria?

Mhe. Lissu: Ndio lakini uchaguzi sheria zake zinasimamiwa na tume.

Katuga: Je kuwarushia mawe na kuwapiga watu ni uvunjifu wa amani?

Mhe. Lissu: Sio tu amani ni uvunjifu wa sheria pia.

Katuga: Hiyo mihimili mitatu nani ni custodian wa amani?

Mhe. Lissu: Ni jeshi la Polisi wako chini ya Serikali.

Katuga: Unapotishia kuivunja amani hivyo vitisho huwa vimelengwa kwa nani?

Mhe. Lissu: Swali lako ni la hovyo.

Katuga: Unapotishia unakuwa umelenga nani?

Mhe. Lissu: Nikimlenga huyu Bwana anamuonesha Dr. Nshala kuwa nikimtishia ninakuwa nimelitishia Jeshi la Polisi? Hapana.

Katuga: Waheshimiwa wameelewa tuache.

Mhe. Lissu: Lazima wawe wameelewa nafikiri sio vilaza.

Katuga: Kwenye hayo maneno kwamba mtazuia uchaguzi ulisema itakwua kidemokrasia?

Mhe. Lissu: Ungeleta masaa matatu yote ya hotuba ungeona hiyo Demokrasia.

Katuga: Upo tayari ikuamini unachokisema hiyo video uko tayari tukuoneshe?

Mhe. Lissu: Umeleta takataka mahakama ilikataaa. Mimi siwezi kuwasafishia takataka zenu. Mlileta mambo kienyeji yakakataliwa.

Katuga: Kwahiyo uko tayari tuyalete?

Mhe. Lissu: Mngeleta wenyewe. Mimi nitaitoa wapi hadi nilete.

Katuga: Sasa iambie mahakama demokrasia unayoifahamu wewe kila mtu ana haki ya kufanya anachoona kinamfaaa kwamba siku ya kupiga kura aende anayetaka na asiyetaka asiende. Ni sahihi?

Mhe. Lissu: Demokrasia yangu mimi inasema ukiwa hutaki jambo chukua hatua kulizuia kwa njia halali ndio maana maandamano yameruhusiwa kisheria.

Katuga: Demokrasia ipi hiyo?

Mhe. Lissu: Katiba inasema ukifanya maandamano na kuuzuia uchaguzi ni demokrasia kabisa. Niambie wapi sheria imekataza?

Katuga: Haya sawa mjanja wewe. 😂

Katuga: Katiba ndio imekupa mamlaka kufanya kuzuia? Soma ibara ya 30. Kwamba huwezi kutumia haki yako kuzuia haki ya mtu mwingine?

Mhe. Lissu: Kwanza nimesema kufanya fujo sio kosa lilipo mahakamani. Na katiba sio ibara 30 pekeee. Ziko ibara nyingi humo.

Katuga: haya maswali hayana nia yoyote mbaya si ndio Kaka angu?

Mhe. Lissu: Umenishtaki kwa uhaini unasema maswali yako hayana nia yoyote. Wewe vipi wewe?

Katuga: Tuendelee au tuishie hapa shahidi?

Mhe. Lissu: Unaniomba ushauri? Mnyonga na Mnyongwaji tushauriane nini?

PART 288​


KATUGA: Pale ambapo kifungu cha Sheria kinatoa adhabu, maneno kuwa “shall be liable”. Ni discretion ya Mahakama?

MHE. LISSU: Hakuna discretion, adhabu ni hiyo hiyo.

KATUGA: Je, uko aware na kesi ya Shed Mhagama?

MHE. LISSU: Wewe mwenyewe hapo unaangalia kwenye laptop, mimi unataka niangalie wapi sasa?

KATUGA: Omission na Contradiction maana yake nini?

MHE. LISSU: Nipe kamusi nitakupa.

KATUGA: Unataka hadi kamusi?


MHE. LISSU: Sasa umesema ni maneno ya kisheria. Sheria huwa inajibiwa kwa nyaraka, nipe kamusi nikujibu.


KATUGA: Unaweza kutupa tafsiri ya mkanganyiko na kutokuwepo?


MHE. LISSU: Mkanganyiko ni jambo moja lina maelezo tofauti mawili, na omission ni kitu hakikuwepo ila kimeletwa.


KATUGA: Anaenda kupiga soga na wenzake pale. Sasa tusaidie tafsiri ya kifungu cha 163 cha Evidence Act. Je, contradicting ipo hapo?


MHE. LISSU: Ipo ndiyo.


KATUGA: Umewahi kufungua kesi kwa jina lako?


MHE. LISSU: Nimefungua kupitia chama changu.


KATUGA: Nimekuuliza wewe.


MHE. LISSU: We have done things, we have fought. Zipo vita nyingi tumepambana.


KATUGA: Mambo ya Jaji Chande umesema mengi.


MHE. LISSU: Yapi, ya haki jinai au Oktoba 29?


KATUGA: Ya 29 nilisema. Alisema kuwa matukio ya tarehe 29 yalipangwa, na kupangwa kulitokana na masuala ya uchaguzi.


MHE. LISSU: Ndiyo, tume huru na mengine.


KATUGA: Nakuheshimu, kuna jambo sitaki kukwambia.


MHE. LISSU: Unaniheshimu wapi? Acha umbea. Unataka kuninyonga unasema unaniheshimu. Msingenishtaki kwa uhaini kama unaniheshimu.


KATUGA: Taarifa ya Jaji Chande, tume ile ilisema machafuko yale yalilenga kuzuia uchaguzi?


MHE. LISSU: Hilo sijui, nikumbushe.


KATUGA: Je, unakumbuka sana ulisema watatukamata, watanifungulia kesi ya uhaini?


MHE. LISSU: Sikumbuki. Nioneshe.


KATUGA: Ulisema Majaji ni MaCCM.


MHE. LISSU: Nakumbuka.


KATUGA: Nitakuwa sahihi hapo, ndiyo nia ilianza kujengwa kwa sababu mlisema muandamane ili mchukue dola.

MHE. LISSU: Sasa si yangekuwepo kwenye hati ya mashitaka hapo? Mbona hamkuyaweka hayo maneno?


KATUGA: Waheshimiwa Majaji, tunaomba D1 na zingine hadi D16, sasa muda umeisha. Sijui tunafanyaje?

MAJAJI: Majaji wanaandika.

JAJI NDUNGURU: Tunahairisha kesi hadi kesho saa tatu asubuhi.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini, anatarajiwa kuhitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wa utetezi wake, yaani ushahidi mkuu, ikiwa ni siku ya tatu katika mfululizo wa utetezi wake.


Leo Jumatano, Agosti 26, 2026, Lissu anatarajiwa kuhitimisha kwa kuangazia ushahidi wa upande wa mashtaka, kwa kuuchambua anachokiita udhaifu wake kuishawishi mahakama kuwa haukuweza kuthibitisha shtaka linalomkabili kwa kiwango kinachotakiwa kisheria, yaani bila kuacha mashaka yoyote.

Hatua hiyo itahitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wake, yaani ushahidi mkuu, na kuingia sehemu ya pili ya ushahidi wake, yaani ushahidi wa nyongeza (cross examination).

Katika hatua hii, atahojiwa na waendesha mashtaka maswali mbalimbali ya dodoso kuhusiana na ushahidi wake wa msingi.

Lissu anakabiliwa na kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, Dunstan Ndunguru akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
Sisi tuna jambo letu, mazuzumagic endeleeni na cinema za machinjachinja wauao ili wapate kutamalaki
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini, anatarajiwa kuhitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wa utetezi wake, yaani ushahidi mkuu, ikiwa ni siku ya tatu katika mfululizo wa utetezi wake.


Leo Jumatano, Agosti 26, 2026, Lissu anatarajiwa kuhitimisha kwa kuangazia ushahidi wa upande wa mashtaka, kwa kuuchambua anachokiita udhaifu wake kuishawishi mahakama kuwa haukuweza kuthibitisha shtaka linalomkabili kwa kiwango kinachotakiwa kisheria, yaani bila kuacha mashaka yoyote.

Hatua hiyo itahitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wake, yaani ushahidi mkuu, na kuingia sehemu ya pili ya ushahidi wake, yaani ushahidi wa nyongeza (cross examination).

Katika hatua hii, atahojiwa na waendesha mashtaka maswali mbalimbali ya dodoso kuhusiana na ushahidi wake wa msingi.

Lissu anakabiliwa na kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, Dunstan Ndunguru akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Updates za Mahakamani

Dada wa Tundu Lissu akiongoza maombi muda huu mahakamani kabla ya Kesi kuanza.

Haya ndio mambo tunataka sasa sio michezo ile ya jana
 
Back
Top Bottom