Pre GE2025 Tundu Lissu alisema Mbowe ana idara ya usalama na ujasusi anayotumia kuwadhuru watu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo mnamo Januari 21, 2025 amkimshinda Freeman Mbowe ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 20.

Licha ya uchaguzi huo kuwafanya viongozi hao kutofautiana na kuwa na misimamo tofauti katika masuala mbalimbali jambo ambalo lilisababisha wakati wa kampeni baadhi ya wanachama kufuata misimamo hiyo na kutofautiana lakini mara baada ya uchaguzi Mbowe alikubali kushindwa na kumpongeza Lissu huku akiwataka wanachama kumuunga mkono.

Kumekuwapo na kipande cha Video kinachosambaa mtandaoni kikimuonesha Lissu akisema “wanaua watu halafu wanasingizia wengine ili wao wasiwajibike kwa udhalimu wao sasa mimi nawasema hadharani ni watu, Mbowe kwa sababu anagombania madaraka na idara yake ya ujasusi”


Je ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa video hiyo ilipotoshwa kwa kukata na kuunganisha vipande vidogovidogo kutoka kwenye video halisi iliyochapishwa katika chaneli ya televisheni ya mtandaoni ya Jambo TV youtube.

Katika video halisi Lissu alizungumza mnamo tarehe 17 mweze Disemba 2024, mara baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi ya uenyekiti. Pamoja na mambo mengine aligusia juu ya taarifa alizopewa juu ya baadhi ya watu kuwa na nia ya kutaka kumuumiza kisha kumsingizia Mbowe aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho tofauti na video iliyopotoshwa inavyoeleza.

“...wanaua watu halafu wanasingizia wengine ili wao wasiwajibike kwa udhalimu wao, sasa mimi nawasema hadharani, siyo habari ya Mbowe, Huyu baba aliyeniambia maneno haya hajasema ameambiwa ni Mbowe atakayefanya haya, kwa hiyo likitokea la kutokea tusije tukaambizana ni mambo ya Mbowe…”

Kuhaririwa kwa kipande hicho cha video kunadhihirika kutokana na kuruka kwa picha pamoja na sauti ambazo zimeungwa sehemu zisizo stahili.​

Attachments

  • Screenshot 2025-01-26 163009.png
    234.3 KB · Views: 6
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…