Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aliwahi kuisaidia nini Tanzania? Mwenye uelewa atuelezee

Kwa upande wangu, kiongozi ni yule mwenye sifa za kuongoza watu hata kama sijui kama alishawahi kusaidia nchi au la. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba 'we should never judge people according to memory (what we remember about them), but according to what they are'. Hata Mwalimu Nyerere alisisitiza tuwachague watu ambao 'tukiwaona tuamini kwamba wanasimamia kile wanachokiamini'. Hivyo, siku ya kupiga kura ikifika kila mtu ajitafakari anaenda kumpigia nani (ambaye ni siri yake) kwa kuamini kwamba huyo ambaye ni siri yake ndiye anayemwona kwa wakati huo kuwa anafaa kuwa kiongozi wake.
 
AMELIPA kodi , kwanza ya uwakili na pili ya biashara zake tofauti na WEWE UNAISHI kwa shemeji yako, unakula na kulala bure hata kodi ya 100 hujawahi kulipa, yaani dada yako anasuguliwa ndio upate mlo, shemeji akimfukuza dada yako na wewe huna chako hapo.
 
Labda tukuulize wewe kwanza umeanza kumjua Tundu Antipas Lissu lini???

Nenda Buzwagi na Nyamongo nenda kawaulize Tundu Antipas Lissu ni nani? Watakwambia

Nenda kawaulize kipindi wanasumbuliwa na uchafu uliokuwa unatoka migodini ni mwanasheria gani alijitoa kuwapambania tena iyo ni 2000-2004.
 
Mkuu wale wa upande wa pili utaona reply nyingi zikiwataka wapiga kura wamjaribu Lissu kwa kumpigia kura, Jpm ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Yeye mwl Nyerere wakati anapewa alikuwa na ameifanyia nini tanganyika?
 
huyo hata jimboni kwake hawajui alikuwa nani kwenye maisha yao. ila jf tu[emoji38][emoji38]
 
Hivi nyie shuleni mlienda kujifunza ujinga? Ndio nini hii umeandika? Shubamitii walah.!
Umewlewa lakini, huyo mtu wenu hafai kabisa,
Kama angekuwa ana nia ya kuwa raisi angeepuka kutetea kesi zinzoibana nchi, lakini yeye akawa ananufaisha tumbo lake tu.
Sasa masuala ya kuongoza nchi awaachie wenye machungu na nchi
 
Atasaidia kujua 1.5 trl zimeenda wapi maana hatujui mpaka sasa
 
Wew ni mamluki,, Aliwahi kutufanyia nin kwan aliwahi kushika madaraka ayo unayoyasemea,. Subiri achukue kiti ndio atufanyie ayo mambo..

..
 
Ni wakati muafaka kwa watanzania,kumuuliza ndugu Lissu ,JE amewahi kuifanyia au kuisadia nini Tanzania mpaka agombea cheo kikubwa kama urais?
We ulitaka awasaidie nini ? Yeye ndio anakusanya kodi ? Shenzi kweli
 
Unauliza wakati tayari una majibu yako binafsi, sasa itakufaa nini hata ukijibiwa. Mjuage namna ya kuandika hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…