Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amejaribu aguswe lakini wametegua hawajamgusa

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amejaribu aguswe lakini wametegua hawajamgusa

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Tangu Mh Lissu arejee nchini AMEJARIBU serikali na vyombo vyake ili aguswe lakini hajaguswa.

Siku alipokuwa akirejea nchini aliwaandamanisha watu kutoka Uwanja wa ndege mpaka Ufipa bila barua ya polisi. Alifanya hivyo makusudi akitegemea Polisi watamgusa. Polisi walibaini mtego WAKAUTEGUA kwa kukaa kimya.

Alipoanza Safari ya kutafuta wadhamini AMEFANYA mikutano mikubwa ikiwepo kufanya matembezi lakini hata kutoa lugha kali. Alifanya makusudi akijua Polisi watamgusa ili apate hoja za kuwaeleza wale jamaa lakini Polisi waliona mtego WAKAUTEGUA tena Morogoro ndo wakamsindikiza kabisa.

Juzi akiwa anaenda kurudisha fomu alianza kuiattack tume kuwa imepanga kumuondoa kwenye mchakato. Alifanya hivyo akiwa anaitafutia tume kuwa ilimuondoa kwenye mchakato. Tume wakanasua mtego na wakamwambia tutahakiki majina ya wadhamini mbele yako hata kama ulikiuka taratibu. Pale ilikuwa sawa na kupigwa buti la shingo.

Leo ameenda kwa RPC DODOMA kujaribu kumgusa, alipofika RPC akamsikiliza bila kumfanya chochote. Alienda pale makusudi ili kutafuta kick ya kuguswa. Walitegua mtego.

Ni dhahiri alichokuwa Akiwaaminisha wazungu kabla hajarudi Tanzania hakuna hata moja Ambalo amefanikiwa.

Ombi langu asiguswe wala msishughulike naye kwani WATANZANIA TUNA JAMBO LETU 28/10/2020. Tutamjibu yeye na wanaomtuma kwa vitendo.
 
Waliomshambulia wakamatwe bila kuleta ubabaishaji.
 
  • Dislike
Reactions: UCD
Tangu Mh Lissu arejee nnchini AMEJARIBU serikali na vyombo vyake ili aguswe lakini hajaguswa...

Msiyempenda kaja!

Ila kwa vitisho mlivyokuwa mnampa jamaa kama angerudi, inabidi uwaulize wakubwa zako inakuwaje wameamua ku stand down?
 
Lisu afanye nini ndugu zangu, alisema anakuja watu wakatoka majumbani kwao kwenda kumpokea bila shuruti. Kosa la lisu lipo wapi hapo?

Kama alipata fununu za kukatwa jina akapaza sauti yake kosa lake nini? Kaenda kufuatilia gari lake hilo pia kosa, au alimkwida kamanda Muroto hapo ofisini kwake? Ama hilo gari ndo basi tena alishakula risasi za kutosha akapona hivyo hana haki ya kupata gari lake kwakua kapona?

Ni vyema tutende haki kwa wengine hata kama hatumpendi si sahihi kumsema vibaya akidai haki yake.
 
Baba mwenye nyumba alieyumba anahema kama mbwa aliekosa pumzi kipindi hiki!
 
Ccm wote wanamuogopa Lissu. Mguseni muone. Hajarudi kijinga, jiwe na ubabe wake amefyata mkia, anaugulia maumivu ya makombora anayoporomoshewa na hana la kufanya. Lissu anatamba anavyotaka.
 
Wakati yuko ughaibuni si mlisema akikanyaga mguu tu hapa TZ mtampeleka Segerea siku hiyo hiyo ya ujio wake, sasa kulikoni tena mnamwacha atanue tu apendavyo. CCM mnakwama wapi?
 
Back
Top Bottom