Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amepewa adhabu na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ya kutofanya kampeni kwa siku 7 halafu anajirekodi malalamiko yake kwa kiingereza


Mzee nikuulize swali dogo Sana,
Hivi boss wako ambae anakulipa salary, yy anakupa madawa ili upone ww na familia yako, anakuongezea ela kwenye bajeti yako ya chakula

Do you think huyo boss anaweza kumkod mtu aje hakudhuru?

I'm sure hawez coz kitu ambacho atafanya ni kukunyima Ile Misaad anayokupa na bila shida utakufa tu

Unashangaa Lisu kuongea kizungu mbona kigwangala huwa anaongea kizungu kwenye press zake arusha?
 
Anataka beberu wake Amsterdam amsikie!

Alafu alivyo mbumbumbu anafikiri atamsaidia, kumbe hatamsaidia kwa chochote,

Yani Lisu sijui hana washauri?
 
Kama hujui, basi unapaswa kutambua kuwa Kiswahili na Kiingereza zote ni lugha rasmi za mawasiliano hapa nchini. Kwa hiyo wala haijalishi kama unachukizwa na lugha aitumiayo Lissu kufikisha ujumbe wake alioukusudia kwa hadhira yake lengwa, kwa kuwa hilo la wewe kutokukielewa Kiingereza ni tatizo lako binafsi.
 
Kama wewe hujui kiingereza au unaumia kuona Lissu ameandika kwa kiingereza ni bora kukaa kimya. Usiandike ujinga na kupotosha watu hapa.

Usahihi ni kwamba, karibu kila official statement anayoitoa Lissu kwa Kiswahili huitoa pia kwa lugha ya kiingereza and vice versa. Ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa sasa. Hii pia husaidia kuondoa upotoshaji wa kimakusudi unaoweza kufanywa na wale wasiomtakia mema Lissu.

Kama unataka jambo lako liwafikie watu wengi duniani huwezi kukwepa kukitumia kiingereza kama sehemu ya lugha ya kuwasilisha. Ndio maana hata wasanii wa nyimbo za injili, bongo flavour na bongo movie hutoa kazi zao kwa kiswahili lakini huweka tafsiri ya kiingereza (English subtitles) ili kuifikia dunia.
 
Pesa ndio inawafanya mnunuliwe na mabeberu.

Stupid!!

Beberu au wahisani wa maendeleo?
Gomeni basi kuwa hamtaki misaada muone kama ndugu zetu wenye Hiv kama wote hawatokufa

Acheni kujifanya ni doner country while hata condom tunapata msaada
 
Na huyo Mwigulu Nchemba yumo kwenye list ya wauaji ngoja kitabu cha 27 pages kitoke. Liwe jua au Mvua, muwe Tanzania au wapi mtaishi kama mashetani. I swear, hata jiwe halitabakia
 
Kwako Rose au sijui mzee nani sijui....

1. NEC haioni Mtukufu anavyofanya kampeni kwa kisukuma, hii inaruhusiwa?
2. NEC haioni Mtukufu anavyobadili ratiba za kampeni atakavyo, hii inaruhusiwa?
3. NEC haioni Mtukufu anavyotumia kofia ya urais kutawanya pesa za miradi na za kawaida kipindi cha kampeni, hii inaruhusiwa?
4. Una uhakika mikataba ya gesi imefutwa?
5. Una uhakika sasa hivi mabeberu hawasombi madini?
6. Aliyeingia mikataba ya kufua umeme waliyokuwa wanakwapua hizo pesa ni Chadema na ACT au CCM?
7. Sasa hivi tumenunua ndege zetu, je ni sisi ndio tunatawala bishara ya utalii? Umewahi kupitia makampuni makubwa yanayoleta watalii Tanzania kuna ya serekali pale?
8. ' NEC iachwe itimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria na wote waliopata nafasi ya kugombea wafuate sheria, taratibu na miongozo ya NEC. Haiwezekani mtu alete varangati halafu aachwe, huo sio utaratibu hata kidogo'. Wakati unaandika hii sentensi, uliifikiria mara 2?
9. Unahisi kupewa adhabu kupumzika siku 7 ni ishu sana? Yule anaekwenda kuwa nje ya kampeni kwa siku 8 kapewa adhabu na nani?
10. Umetaja waliouwawa recently (Hakika kuuwana ni kitu kibaya sana na inatakiwa kupigwa vita na kila mtu) lakini akili yako, moyo wako na mikono yako imekataa kabisa kuwataja na kina Gwanda, Ben Saanane na wengine?
 
Nenda anakoishi Amsterdam akakuongoze wewe na familia yako sisi watz utuachie JPM wetu, msituletee huu ujinga wenu hapa nchini.
 
Sheria ndio imemzuia,Lakini bado anakaidi.

Anachokitafuta atakipata.
Sheria hiyo ingekuwa inafanya kazi hata magufuli angekuwa amefungiwa tangu mwanzo wa kampeni.

Tulieni sindano ziwaingie
 
Anataka beberu wake Amsterdam amsikie!

Alafu alivyo mbumbumbu anafikiri atamsaidia, kumbe hatamsaidia kwa chochote,

Yani Lisu sijui hana washauri?

Na ww hujui, ni shabiki ambae hujui kitu chochote, Lisu Alifanya press ya kizungu ni kwa sababu alialikwa kwenye Ile African debate ambayo Rais wa Ghana na wengine walishiriki

Sasa ulitaka aongee kiswahili?
 
Mleta mada hutaeleweka...kiuhalisia watanzania wameichoka ccm, sio kwamba wanampenda sana Lissu au kumchukia sana Magufuli. Tatizo hapa ni CCM.

Kwenye hali hii ukileta hoja yoyote kinzani unaweza kupigwa mawe!
 
NECCM, na bado hadi ifike trh 28, mtaita maji maaa
 
Nia ya hiki Chama cha Mbowe kina nia ovu kabisa na mama Tanzania. Mabeberu washawapanda kichwani hawa watu, na wanachotafuta ni nchi iparaganyike kwa kukosa Amani na mshikamano ndio raha yao.Chadema kama mpekula vya watu,na kuwaahidi rasilimali zetu mtajibeba mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…