Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amepewa uhuru uliopitiliza

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amepewa uhuru uliopitiliza

Jane Lowassa

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
4,955
Reaction score
9,041
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa Tundu Lissu tangu mchakato wa kampeni uanze. Kiwango cha Uhuru aliopewa na Serikali ni kikubwa sana.

Hata yeye mwenyewe nina uhakika wala hakutarajia. Yaani imekuwa kama surprise kwake. Haiwezekani ametua airport hajabughudhiwa. Amefanya kampeni kipindi cha kukusanya saini hajabughudhiwa. Ameenda kurudisha fomu tume ya uchaguzi hajabughudhiwa. Na kibaya zaidi kipindi hiki cha kampeni anatoa lugha ya matusi kwa Rais lakini hajabughudhiwa.

Sasa ni wakati wa kusema enough is enough. Upole huu wa serikali utatufikisha pabaya tusipokuwa makini kama nchi. Lazima huyu mtu awe held responsible kwa maneno na matendo yake
 
Sasa uhuru wa Lissu anaoupata na kuupigania si upo kikatiba? Nchi hii ni huru kwa miaka 59 sasa kama huna habari.

Hakuna matusi yoyote aliyoyatukana Lissu, polisi hawana sababu ya kumkamata zaidi ya kumpatia ulinzi kama mwananchi mwingine wa kawaida. Au unaona polisi wamemzawadia uhuru kwa kutokumkamata tu alivyotua airport? Uhuru ni haki ya kila Mwananchi!!
 
Wewe kama wewe au hata hicho chama chako cha Ccm, unadhani mna uwezo wowote ule wa kupambana na Lissu? Au umeshasahau huyo Tundu Lissu ni Wakili na Mwanasheria nguli kuliko hata Mkufunzi wake Paramagamba Kabudi?

Hamna cha kumfanya!! Hilo msisahau. Siku zote atabakia kuwa kiumbe pekee nchini mwenye uthubutu wa kumwambia mfalme yuko u.c.h.i.
 
Mleta mada alitaka Lissu akitua airport abughudhiwe!

Akienda kuchukua saini za wadhamini abughudhiwe!

Akifanya kampeni abaghudhiwe!

Mleta mada anashangaa imekuwaje kuwaje Lissu hajabughudhiwa?
Hivyo anaishauri serikali imbughudhi!

Hivi bughudha za risasi 16, kunyimwa matibabu na kunyimwa kiinua mgongo chake cha ubunge bughudha hizo hazikutoshi?
 
Na yule mwingine je yeye afanywe nini?
Zamani sikuwahi kuuamini usemi huu,
kwa kuwa kuku,mbwa,paka na wanyama na ndege wanaofugwa wameizoea hali ya kufugwa na utumwa kwa binaadam,ikitokea kuwa Binaadamu akawapa uhuru na kuwarudisha wote polini nini kitatokea, wote watarejea kwa binaadamu na kudai haki yao ya utumwa.

hiki ndicho ninakiona kwa watanzania kwa sasa wanadai wanyimwe uhuru wa kutoa maoni,kufikiri. unashindwa kuelewa kuwa kwa sasa nchi iko katika kipindi gani,walinyamaza kwa muda wa miaka mitano sasa ndio muda wao wa kufanya siasa napo pia hamtaki?
 
Weka hapa matusi aliyotukanwa Magufuli tuyaone , mlizoea kusikia ya upande mmoja kwa miaka mitano " TUNATEKELEZA " sasa zamu yenu ya kuumbuka imefika , na nakutahadharisha kwamba ikifika octoba mosi utajificha uvunguni , maana shughuli rasmi ndio inaanza
 
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa Tundu Lissu tangu mchakato wa kampeni uanze. Kiwango cha Uhuru aliopewa na serikali ni kikubwa sana.

Hata yeye mwenyewe nina uhakika wala hakutarajia. Yaani imekuwa kama surprise kwake. Haiwezekani ametua airport hajabughudhiwa. Amefanya kampeni kipindi cha kukusanya saini hajabughudhiwa. Ameenda kurudisha fomu tume ya uchaguzi hajabughudhiwa. Na kibaya zaidi kipindi hiki cha kampeni anatoa lugha ya matusi kwa Rais lakini hajabughudhiwa.

Sasa ni wakati wa kusema enough is enough. Upole huu wa serikali utatufikisha pabaya tusipokuwa makini kama nchi. Lazima huyu mtu awe held responsible kwa maneno na matendo yake
Sindano zinawaingia vizuri mno
 
Back
Top Bottom