SI KWELI Tundu Lissu amesema hakubaliani na lolote litakalozungumzwa na Mbowe

SI KWELI Tundu Lissu amesema hakubaliani na lolote litakalozungumzwa na Mbowe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wanajamvi salaam

Leo nimekutana na hii taarifa inasema Tundu Lissu amesema hakubaliani na lolote litakalozungumzwa na Mbowe, nafikiri haya yanaibuka baada ya vikao vya kamati kuu ya CHADEMA, Je ni uhalisia katika taarifa hii wakulungwa?
JAMII CHECK SI KWELI.jpg
Gd3zrcNXAAA6wOJ.jpeg
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ambapo mwaka 2017 Alikuwa ni Rais wa chama cha wanasheria Tanzania (TLS) kwa miezi mitano kabla ya kushambuliwa kwa risasi. Mwaka 2010 mpaka 2020 alikuwa ni mwakilishi wa wananchi Bungeni wa jimbo la Singida Mashariki. Tundu Lissu amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa walio mstari wa mbele katika kukosoa serikali. Mara kadhaa kumekuwapo na upotoshaji kuhusu kiongozi huyo ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali dhidi ya masuala mbalimbali, tazama hapa, hapa na hapa.

Kumeibuka chapisho linalodaiwa kutolewa na televisheni ya mtandaoni ya Watetezi TV likirejelea ujumbe wa Lissu unaoonekana kuchapishwa kupitia mtandao wa X ukidai amesema hakubaliani na lolote litakalozungumzwa na Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA.


Je ni upi uhalisia wa chapisho hilo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Tundu Lissu hakuchapisha ujumbe huo kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X (Twitter) kama inavyoonekana katika chapisho hilo, aidha tarehe iliyotajwa 03/12/2024 kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Watetezi TV hazikuchapisha taarifa hiyo.

Kadhalika yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo, ambayo yanalitofautisha dhidi ya machapisho ambayo hutolewa kupitia kurasa rasmi za mitandao ya Watetezi TV, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutofautiana kwa lugha ilitumika kutaja mwezi Disemba ambapo chapisho hilo imetumia lugha ya kiswahili tofauti na machapisho rasmi ya Watetezi ambayo hutumia lugha ya kiingereza ambapo pia tarehe na mwaka hutenganishwa na mkato bila kuacha nafasi tofauti na ilivyo katika chapisho hilo. Hata hivyo Watetezi TV haitumii rangi ya bluu habari (light blue) kama utambulisho wake lakini chapisho hilo limetumia rangi hiyo.

Hivyo mapungufu hayo yanathibitisha kuwa chapisho hilo si la kweli na lina lengo la kupotosha.​
Back
Top Bottom