- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu kuna hii inasambaa Twitter je, ni ya kweli?
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na amekuwa mwenyekiti wa chama hicho kuanzia mwaka huu 2025, hivi karibuni amekuwa na ziara nyumbani kwao Ikungi Singida. Safari hiyo imekuwa ni ya kwanza kuanzia alipopata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama hiko.
Madai
Kumekuwepo na grafiki inayoonekana kufanana na ya Millard Ayo inayosambaa ikionesha kuwa Tundu Lissu rasmi ametangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2025, alipokuwa Ikungi Singida, Tazama hapa na hapa
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa Taarifa hiyo si ya kweli. Lissu alipokuwa Ikungi Singida. Ufuatiliaji wa kimtandao kwa kuangalia hotuba alizozitoa Lissu alipokuwa mkoani Singida umebaini kuwa hakuna mahali ambapo Lissu alisema atagombea urasi mwaka huu.
Lissu alipokuwa Ikungi, Singida alipokelewa na wananchi ambapo alizungumza nao, licha ya mambo mengine Lissu alizungumzia kuhusu changamoto za uchaguzi zilizojitokeza mwaka 2019, 2020 na 2024. Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa Febuari 15, 2025 alisema kuwa uchaguzi umekuwa na madhaifu mengi ikiwemo wizi wa kura na mambo mengine mengi ambapo alisema watajtahidi wazuie uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu 2025, tazama hapa.
Aidha hotuba ya pili aliitoa alipopokelewa kijijni kwao kwa ajili ya maombi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wanachama katika eneo hilo ambalo ndipo nyubani kwao alipozaliwa na kukulia na hakuzungumzia pia kuhusu nia ya kugombea nafasi ya Urais, tazama hapa.
Ufuatiliaji wa kimtandao pia umebaini grafiki hiyo pamoja na taarifa hiyo haikuchapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Millard Ayo.