MWAISEMBA CR
Member
- Apr 21, 2014
- 87
- 81
✳️HUYU TUNDU LISSU ANA NINI KWANI ? MBONA KAMA KUNA HOFU KUBWA AMEILETA KWA WATAWALA NA WANANCHI ?
🔵Na: Shujaa Charles Richard Mwaisemba ( ©️®️ M )
Ni muda mrefu sana ulipita karibu miaka mitatu hivi tangu September 7, 2017, mhe Tundu Lissu apigwe risasi na kuwa kwenye hatari ya kifo, lakini kwa Neema za Mwenyezi Mungu alilizuia hilo na hivyo kuwa katika matibabu kwa kipindi chote alianzia Nairobi na mpaka Ubeligiji.Kwa shambulio la hatari la namna ile wananchi wote walikata tamaa kama atapona au kama ipo siku atainuka tena na kutembea na kurudi nchini mwake.Hivyo wengi wetu tulishasahau habari zake kwa maana hatukuwa tunapewa taarifa zozote kutoka katika serikali yetu kuhusu hali ya Mgonjwa wetu kwa kipindi chote
Mara baada ya Tundu Lissu kupigwa Risasi zile na kupotea nchini kwa muda mrefu hivyo, wananchi wengi walikata tamaa na kujua upinzani nchini ndio umekufa kabisa, maana Tundu Lissu ndiye alikuwa mtu pekee aliyebaki mwenye uwezo na ujasiri wa kipekee wa Kuikosoa Serikali hii ya magufuli hadharani na kuzungumza bila uwoga kuonyesha mapungufu ya serikali hii.Maana ni wengi waliokuwa wanafanya hivyo waliishia kutekwa na watu wasiojulikana, wengine waliuliwa na kutupwa katika fukwe za bahari, wengi walisingiziwa kesi na mpaka leo walitupwa gerezani, wengine walifirisiwa mali zao, Wengi walitishwa na kulazimisha kufanya wasiyoyataka baada ya kufanyiwa vitendo vya ajabu...
Mara baada ya Tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, nchi zima ilizizima, hofu ilitanda kila mahali kwa kila mwananchi na viongozi wote wa ngazi zote, Kutokea watu wote waliogopa tena kuonekana wanaikosoa serikali kwa kuhofia maisha yao maana hata Jeshi la Polisi, Jeshi la wananchi tena halikuwa linalinda tena usalama wa raia bali lilikuwa linailinda serikali.Hivyo nchi iliingia kuongozwa katika hofu, kila kiongozi ilibidi awe anasifia na kuunga mkono ndio salama yake, Vyombo vyote vya habari vilikuwa ni lazima viandike mazuri tu ya serikali hii kuhofia kufungiwa.Hofu iliingia kila mahali mpaka kila stori unazosikia ni watu tu wanazungumzia Serikali ya Magufuli Kufanya ujenzi wa miundombinu ya nchi hii, mpaka ikaonyesha kama Upinzani haupo tena na umeshakufa, maana tulishuhudia viongozi wote wa upinzani kupewa kesi rukuki na kufungwa ndani, Hatukuona mikutano tena ya kisiasa ya upinzani kwa karibu miaka 5.
Hivyo Serikali ya Magufuli kwa kipindi chote hicho baada ya kutandaza hofu ya kudhulika, kuuliwa au kushambuliwa ukionekana unaikosoa, iliifanya serikali kuendelea na shughuli zake na kufanya mikutano wao wenyewe kwa wananchi na kuleta maendeleo ya vitu bila kubughudhiwa tukiamini upinzani Umekufa....Vyombo vyote kwa miaka 5 vilimtangaza magufuli na miradi mikubwa yote aliyoifanya...
Lakini, Kinyume na matarajio ya wengi, Mara yule mtu( Tundu Lissu) alipotangaza kuwa atarudi nchini tena akiwa na nguvu na anatembea kuja kugombea Urais, tayari nikaanza kusikia Jeshi la Polisi kuanza tena kutoa vitisho vya hali ya juu kwa wananchi kuwa wasiende Kumpokea Tundu Lissu kwani wanaweza kudhulika na kupigwa vibaya na jeshi la polisi. Nikajiuliza Kwanini Wanazuia Tundu Lissu Asipokelewe na wananchi?. Kwanini Jeshi la polisi wanaogopa mapokezi yake? .
Jambo kubwa lililoshangaza Ulimwengu, ni Ule umati wa watu usiokuwa wa kawaida Uliojitokeza Siku ya MAPOKEZI YA TUNDU LISSU katika Uwanja wa ndege wa Mwl Julius Nyerere, Dar ambao haukutegemewa maana tulifikiri Wapinzani hawapo tena, Tulifikiri kutokana na hofu na vitisho vya muda mrefu vya Polisi vinaweza vikawafanya watu wasitokee Kumpokea kabisa.Lakini jambo lililotokea Siku ile ndio Lilinifanya NIMJUE ZAIDI LISSU NI NANI NA KWANI WANA MHOFU NAMNA HIYO?
Kwa Tukio lile, ndio lilitoa picha kwa ulimwengu mzima kuwa KUMBE SI TU UPINZANI HAIJAFA BALI KUMBE WATU WANA IMANI NA MAPENZI NA TUNDU LISSU kiasi cha kutohofia maisha yao tena kuwa huenda wangepigwa na polisi mpaka kufa kama yaliyokeaga kipindi cha kina akwilina, Lakini walitoa ujumbe kwa jeshi la Polisi kuwa hawapo tayari kuogopa tena ikiwa wanachokifanya hakivunji sheria za nchi , hivyo watu maelfu walijotokeza kumpokea Mhe Tundu Lissu, Na kwa wingi wa umati ule hata polisi wenyewe waliogopa hivyo wakashindwa kufanya waliyokuwa wamekusudia kufanya....Hiyo ndio nguvu ya Umma...
Lakini pamoja na yote, Kumeanza kuwa na maswali mengi kwa watu " LISSU NI NANI NA ANA NINI?". Mbona Serikali inamuogopa kiasi hicho wakati wao wametuaminisha watanzania Serikali ya Magufuli imefanya mazuri, Sasa wanaogopa nini kuruhusu taarifa za Tundu Lissu kutangazwa katika vyombo vya habari na magazeti?. Naanza kuona Vyombo vyote vya habari kupigwa faini na serikali ya sh mil 15 ikiwa tu zitaandika taarifa za Tundu Lissu. Hivi mnaogopa nini, Ikiwa Taarifa zake ni za Kipindi hichi tu kifupi cha kampeni na taarifa zenu juu ya mambo mliyotufanyia watanzania siku zote mmeshatuonyesha na kututajia.Kwanini tunahofia kurusha taarifa za mhe Tundu Lissu? Kwanini ana nini? Au hastahili kulingana na sheria zetu? . Naona Jeshi la polisi Kupitia IGP anadai kukusudia Kumkamata Tundu Lissu kama Mwarifu, Kwani amefanya nini?
Nimegundua Hofu kubwa iliyopo kwa Serikali ya Magufuli na Polisi ni kwasababu Tundu Lissu ndiye Mgombea Pekee wa Upinzani mwenye mvuto na watu wengi kwa Tiketi ya Chadema. Hii hofu inanipa Picha KUJUA HUYU TUNDU LISSU ANA NGUVU NA UWEZO KIASI GANI DHIDI YA SERIKALI YA MAGUFULI!!.Maana huwezi kumuhofu mtu ambaye hana madhara makubwa kwako.Huwezi kutumia Nguvu kubwa ya Dola kushindana na mtu mmoja Tundu Lissu ambaye hana madhara kwako? .Kama hana madhara na mna hakika kuwa mlichowafanyia watanzania ni mazuri kwanini msiwaache na wao na kuwapa uhuru wa haki sawa wa kutumia vyombo vyetu vya habari kujinadi na taarifa zao kurushwa?
Haihitaji akili nyingi kujua kwamba TUNDU LISSU ANA NINI MPAKA SERIKALI YOTE NA POLISI WOTE WANAANGAIKA KUTAFUTA KUMZUIA SI TU ASICHAGULIWE NA TUME YA UCHAGUZI BALI HATA TAARIFA ZAKE ZISISIKIKE KWA WATU...Hii picha ya wazi na kutoonyesha usawa katika uhuru wa habari kwa watanzania kwa wagombea wote wa urais kwa vyama vyote vya siasa ndio unaoleta mashaka kwa watu KWANINI HAMTAKI ASIKIKE AKIZUNGUMZA? MNAOGOPA NINI AMBACHO MNADHANI WATANZANIA WAKIKIJUA KUTOKA KWAO WATAWAPENDA?...Tunahitaji haki sawa , Tume huru ya uchaguzi......Mungu awabariki
🔵 Na Shujaa CRM
stmwaisembac@gmail.com
0712-054498/0759-420202